Uchaguzi 2020 Upinzani watoe Ilani zao za Uchaguzi yaani “Election Manifesto" acheni porojo hazina Tija

Vyama vya upinzani hawana mpango wa kukamata dola wamepanga kumpa heka heka tuu magufuli
Mkuu pengine ni mgeni kwenye siasa. Opposition nyingi sana duniani huwa zina malengo ya kuchukua dola lakini kwa gradual process sio spontaneous.

Mfano chama kikuu cha upinzani sauzi kinaitwa DA kilikua na lengo la kupunguza ushindi wa ANC walau ufike 50%. Na ichukue majimbo 100+. Na kiukweli malengo yapo realistic na walifanikiwa kiasi.

Je walikua wapumbavu? Mifano ipo mingi hta Kenya kule tuliona kuna vyama vilishiriki ili tu kuretain Majimbo na County walizomiliki na sio kuongeza. Case ya Wiper n.k

Ila Tanzania sijawahi ona chama kikisema kinagombea ili kishinde tu majimbo 100 na urais wafike 30%!!! Sasa ni lini hao wapinzani hawajawahi kuitaka dola?
 
Tatizo jingine ni kwamba wapinzani wanashindwa kutofautisha kati ya harakati za mitandaoni na zile za ardhini kwenye eneo la tukio.

Kwa kiingereza tunasema hiyo yaitwa "asymmetrical warfare" yaani vita kati ya jeshi ambalo limekamilika kwa kila kitu linalopigana na waasi au wanamgambo wa kukusanya.

Hivyo chama tawala kina mbinu na mikakati ya ushindi wakati chama cha upinzani kinatumia mbinu ya kutafuta udhaifu wa chama tawala ilhali wanafahamu kwamba hawakiwezi kwa ubora , uzoefu na umakini.
kwani polepole anasemaje mkuu au ni yeye
 
Ilani ya uchaguzi au kwa kiingereza huitwa election manifesto ni kabrasha litolewalo na chama cha siasa ambalo limesheeni mawazo na sera zote.

Mara nyingi chama cha siasa kikishinda uchaguzi huweza kupimwa mafanikio yake kutokana na utekelezwaji wa ilani yake ya uchaguzi.

Kwa miaka mitano ilopita haitii shaka yoyote kwamba CCM imesimamia ilani yake ya uchaguzi na kuhakikisha inatekelezwa kwa asilimia 80 au zaidi.

Sasa bila kuoindapinda kona Chadema na vyama vingine vya upinzani wanatakiwa watoe ilani zao za uchaguzi kila mmoja kwa wakati wake.

Ilani ya uchaguzi huandaliwa na kundi la watu ambao wote hukaa pamoja na kwa lengo moja kushinda uchaguzi na kushika dola.

Dalili zote kwamba upinzani unaenda kwenye uchaguzi kupoteza viti vingi bungeni zajionyesha.

Ni makosa yaleyale ya miaka nenda rudi tangu sheria ya vyama vingi ipitishwe mwaka 1992.

Mpaka sasa Agustino Mrema ndie kiongozi pekee wa upinzani ambae alitoa ilani ya uchaguzi ya NCCR mageuzi na akatoa upinzani wa kutosha kwa mgombea wa CCM mwaka 1995 marehemu Benjamin Mkapa.

Sasa basi, mwaka huu hali si kama ile ya 1995 hali ni ngumu na ni vigumu kuishinda CCM, tusiwe wanafiki.

Ila bado Chadema ya Tundu Lissu na vyama vingine toeni ilani zenu za uchaguzi ili wananchi angalau waone mmejitahidi.

Hata kama ni mdahalo mnaouhitaji lakini kwenye mdahalo mtakinzana kwenye ilani zenu za uchaguzi na si shutuma za yule kafanza nini ama yule vipi.

Ndo maana ni vigumu kwa Tanzania kufanya midahalo kama hakuna sera kila upande.

Acheni porojo na blahbla za oh! mara jogoo kanunuliwa na kadhalika.

Karibu.

Hiyo ilani ilisemaje kuhusu maisha ya watanzania, ajira na nyongeza ya mishahara ilisemaje kuhusu mazao ya kilimo kama korosho ilisemaje kuhusu wafanya biashara ilisemaje kuhusu uhuru wa wananchi kujiamulia mambo yao ilisemaje kuhusu uhuru wa vyombo vya habari ilisemaje kuhusu haku ya kuishi ya watanzani ilisemaje kuhusu ubora wa elimu na upatikaji wa madawa hospitalini, ilisemaje kuhusu pembejeo na nini kimafanyika katika hayo yote ni asilimia ngapi kama siyo sifuri
 
Ilani ya uchaguzi au kwa kiingereza huitwa election manifesto ni kabrasha litolewalo na chama cha siasa ambalo limesheeni mawazo na sera zote.

Mara nyingi chama cha siasa kikishinda uchaguzi huweza kupimwa mafanikio yake kutokana na utekelezwaji wa ilani yake ya uchaguzi.

Kwa miaka mitano ilopita haitii shaka yoyote kwamba CCM imesimamia ilani yake ya uchaguzi na kuhakikisha inatekelezwa kwa asilimia 80 au zaidi.

Sasa bila kuoindapinda kona Chadema na vyama vingine vya upinzani wanatakiwa watoe ilani zao za uchaguzi kila mmoja kwa wakati wake.

Ilani ya uchaguzi huandaliwa na kundi la watu ambao wote hukaa pamoja na kwa lengo moja kushinda uchaguzi na kushika dola.

Dalili zote kwamba upinzani unaenda kwenye uchaguzi kupoteza viti vingi bungeni zajionyesha.

Ni makosa yaleyale ya miaka nenda rudi tangu sheria ya vyama vingi ipitishwe mwaka 1992.

Mpaka sasa Agustino Mrema ndie kiongozi pekee wa upinzani ambae alitoa ilani ya uchaguzi ya NCCR mageuzi na akatoa upinzani wa kutosha kwa mgombea wa CCM mwaka 1995 marehemu Benjamin Mkapa.

Sasa basi, mwaka huu hali si kama ile ya 1995 hali ni ngumu na ni vigumu kuishinda CCM, tusiwe wanafiki.

Ila bado Chadema ya Tundu Lissu na vyama vingine toeni ilani zenu za uchaguzi ili wananchi angalau waone mmejitahidi.

Hata kama ni mdahalo mnaouhitaji lakini kwenye mdahalo mtakinzana kwenye ilani zenu za uchaguzi na si shutuma za yule kafanza nini ama yule vipi.

Ndo maana ni vigumu kwa Tanzania kufanya midahalo kama hakuna sera kila upande.

Acheni porojo na blahbla za oh! mara jogoo kanunuliwa na kadhalika.

Karibu.
Ilani yao inasema "tuonyesheni sheria inayokataza kubadili wimbo wa taifa" afu wanataka tuwape nchi, hawana adabu kabisa!
 
Mkuu unless sijaelewa..... Mbona kila chaguzi tokea 2005 CHADEMA wanatoa ilani za uchaguzi ama unaongelea kuisambaza/ kuifikisha kwa wananchi kupitia medium tofauti?

Nakumbuka ilani ya 2015 iliandaliwa na kina Dr Bashiru Ally na ilisheheni malengo kibao kama chama kingeshika dola. Hata ya 2020 imekua presented jana vizuri sana na Mrema, imechambua kila sekta kuanzia kilimo mpka Elimu na ina mashiko sana.

Ndo nnachokimaanisha wananchi hawana ideas nini manifesto za upinzani.
 
Ni kweli kabisa.
Naona CHADEMA are basking in the sunshine ya kumuona Lissu tena.
Wanasahau kuwa mwishowe Lissu atachusha na matatizo ya wananchi yako pale pale.
Hatujasikia siasa mbadala ambazo zimejengwa na sera zinazoeleweka.

Lissu si chakula cha kuliwa mezani.
Mbona jana ilani zimechambuliwa. Na sera ya wanawake imezinduliwa jana!! Mfano

1. devolution ili kuzipa mamlaka kadhaa serikali za majimbo/halmashauri kujiendesha.
2. Kuwekeza kwenye kampeni ya kuendeleza miji ili watu wasikimbilie mjini, na kupunguza regional disparities.
3. Kuhusisha zaidi sekta binafsi kwenye kusogeza uchumi mbele na serikali ibaki kma regulator tu. (Ikumbukwe agenda kuu ya chadema ni uchumi wa soko/market economy)
4. Kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kurahisisha access ya mitaji kwa graduates wasio na collaterals kuombea mkopo (Wamesema watasusha makato ya HESLB mpka 3%)
5. Kuongeza purchasing power ya wananchi kwa kupunguza mrundikano wa makato (target iwe 30% pekee ndio ikatwe kwenye mshahara/income ya mfanyakazi sio sasa ambapo inafika 48%+).

Summary tu ila ilani ilichambuliwa jana vizuri tu
 
Ndo nnachokimaanisha wananchi hawana ideas nini manifesto za upinzani.
Imezinduliwa jana tu so tuipe muda kufikia kampeni itakua imeshasambazwa sana.

Pia si kweli kuwa ilani ya CCM imetekelezwa zaidi ya 80%. Mie binafsi nlifanya kautafiti kadogo nikagundua ni below 60%
*Mfano meli tano kubwa za uvuvi
*Kuongeza mara 2 eneo la kilimo cha kisasa
*Kutengeneza ajira mamilion kupitia viwanda
*Kutengeneza ajira za moja kwa moja 6000 kwa kupitia shughuli za uvuvi bahari kuu (kutumia hizo meli 5)

Sasa ukipima multitude ya hizo ahadi na utekelezaji wake huwezi sema ni 80%. Niko tayari twende kipengele kwa kipengele kuprove nachosema
 
Tusema ni 50%

Na CCM ikishinda october 28 itakamilisha hizo 40%

Wapinzani wakipewa nchi hii wataivuruga sana na kutatokea machafuko halafu mabeberu ndo watakuja kuamua.

CCM na JPM wao wapimwe baada ya miaka 10 kama wengine walopita.

Nafahamu maumivu ni makali lakini ni bora iwe hivyo ili kurekebisha kabisa baadhi yetu watanzania wenye kitu chaitwa " Thick Mentality".

President Magufuli is the right man to take that charge.

Mentality yetu iko thick sana kiasi cha kushindwa kutambua kuwa unakaa meza moja na mkoloni wa zamani kupanga njama dhidi ya nchi yako tena ukiwa nje.
 
Tusema ni 50%

Na CCM ikishinda october 28 itakamilisha hizo 40%

Wapinzani wakipewa nchi hii wataivuruga sana na kutatokea machafuko halafu mabeberu ndo watakuja kuamua.

CCM na JPM wao wapimwe baada ya miaka 10 kama wengine walopita.
Mkuu ilani ni miaka mitano tu na wao wanajua hivyo ndio maana mpango wa taifa wa maendeleo ni miaka 5 pia so hawana excuse kushindwa kutekeleza ilani yao.

2. Pia unaonyesha bias kwenye analysis yako kwamba kutatokea machafuko. Je unatumia basis gani kusema hivo? Mbona halmashauri zaidi ya 25 zilikua chini ya upinzani ila hayakutokea machafuko? Mbona kule zanzibar CUF iliunda SUK 2010-15 haikutokea hayo machafuko? Je nini kimebadilika?

3. Hapana chaguzi ni baada ya miaka 5 ndio maana anapimwa sahivi kupitia alichoahidi 2015. Mfano Tz ya viwanda mpaka sasa hakuna dalili. Imagine TFDA hawa standards za kugrade "Food Supplements za Korosho" ndio sembuse viwanda?.

Magufuli kafanikiwa kwenye miundombinu pekee kma Kikwete tu alivyojenga barabara nchi nzima (Hayana ubaya wowote maana ni uwekezaji wa muda mrefu) . Ila tukiwa wakweli kabisa kiuchumi bado sana, inatakiwa investment i-focus kwa human capital zaidi ili tupate kwanza purchasing power, hayo mengine yatapanuka tu kutokana na multiplier effect.
 
Ilani ya uchaguzi au kwa kiingereza huitwa election manifesto ni kabrasha litolewalo na chama cha siasa ambalo limesheeni mawazo na sera zote.

Mara nyingi chama cha siasa kikishinda uchaguzi huweza kupimwa mafanikio yake kutokana na utekelezwaji wa ilani yake ya uchaguzi.

Kwa miaka mitano ilopita haitii shaka yoyote kwamba CCM imesimamia ilani yake ya uchaguzi na kuhakikisha inatekelezwa kwa asilimia 80 au zaidi.

Sasa bila kuoindapinda kona Chadema na vyama vingine vya upinzani wanatakiwa watoe ilani zao za uchaguzi kila mmoja kwa wakati wake.

Ilani ya uchaguzi huandaliwa na kundi la watu ambao wote hukaa pamoja na kwa lengo moja kushinda uchaguzi na kushika dola.

Dalili zote kwamba upinzani unaenda kwenye uchaguzi kupoteza viti vingi bungeni zajionyesha.

Ni makosa yaleyale ya miaka nenda rudi tangu sheria ya vyama vingi ipitishwe mwaka 1992.

Mpaka sasa Agustino Mrema ndie kiongozi pekee wa upinzani ambae alitoa ilani ya uchaguzi ya NCCR mageuzi na akatoa upinzani wa kutosha kwa mgombea wa CCM mwaka 1995 marehemu Benjamin Mkapa.

Sasa basi, mwaka huu hali si kama ile ya 1995 hali ni ngumu na ni vigumu kuishinda CCM, tusiwe wanafiki.

Ila bado Chadema ya Tundu Lissu na vyama vingine toeni ilani zenu za uchaguzi ili wananchi angalau waone mmejitahidi.

Hata kama ni mdahalo mnaouhitaji lakini kwenye mdahalo mtakinzana kwenye ilani zenu za uchaguzi na si shutuma za yule kafanza nini ama yule vipi.

Ndo maana ni vigumu kwa Tanzania kufanya midahalo kama hakuna sera kila upande.

Acheni porojo na blahbla za oh! mara jogoo kanunuliwa na kadhalika.

Karibu.
Porojo ni kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi wapinzani kutafuna trilion 1.5 kisha kumtoa CAG kafara?
 
Mkuu ilani ni miaka mitano tu na wao wanajua hivyo ndio maana mpango wa taifa wa maendeleo ni miaka 5 pia so hawana excuse kushindwa kutekeleza ilani yao.

2. Pia unaonyesha bias kwenye analysis yako kwamba kutatokea machafuko. Je unatumia basis gani kusema hivo? Mbona halmashauri zaidi ya 25 zilikua chini ya upinzani ila hayakutokea machafuko? Mbona kule zanzibar CUF iliunda SUK 2010-15 haikutokea hayo machafuko? Je nini kimebadilika?

3. Hapana chaguzi ni baada ya miaka 5 ndio maana anapimwa sahivi kupitia alichoahidi 2015. Mfano Tz ya viwanda mpaka sasa hakuna dalili. Imagine TFDA hawa standards za kugrade "Food Supplements za Korosho" ndio sembuse viwanda?.

Magufuli kafanikiwa kwenye miundombinu pekee kma Kikwete tu alivyojenga barabara nchi nzima (Hayana ubaya wowote maana ni uwekezaji wa muda mrefu) . Ila tukiwa wakweli kabisa kiuchumi bado sana, inatakiwa investment i-focus kwa human capital zaidi ili tupate kwanza purchasing power, hayo mengine yatapanuka tu kutokana na multiplier effect.

Ni machafuko kwa sababu Upinzani unajiamini utashinda uchaguzi kinyume na matakwa ya wapiga kura ambao wanangojea kuwapa kura nyingi CCM.

Hiyo ndo hali halisi.

Wenzenu wamezunguka nchi nzima na wameimaliza kuwa kununua jogoo mmoja matata sana wa kitoweo.

Kisha wasingizie wameporwa kura.

Sasa kama wasema utaingiza watu barabarani unakuwa watania au?

Hizo si ni vurugu hizo?
 
Porojo ni kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi wapinzani kutafuna trilion 1.5 kisha kumtoa CAG kafara?

Hizi hoja sasa hivi zimefifia sana mkuu.
 
Tatizo jingine ni kwamba wapinzani wanashindwa kutofautisha kati ya harakati za mitandaoni na zile za ardhini kwenye eneo la tukio.

Kwa kiingereza tunasema hiyo yaitwa "asymmetrical warfare" yaani vita kati ya jeshi ambalo limekamilika kwa kila kitu linalopigana na waasi au wanamgambo wa kukusanya.

Hivyo chama tawala kina mbinu na mikakati ya ushindi wakati chama cha upinzani kinatumia mbinu ya kutafuta udhaifu wa chama tawala ilhali wanafahamu kwamba hawakiwezi kwa ubora , uzoefu na umakini.
Kwenye eneo la tukio ndipo utasikia mengi zaidi kwani magufuli alizuia mikutano ya siasa kinyume cha Sheria kwa miaka mitano akajiona ni mjanja sana, sasa wamekusanya madhambi yake yote watayaanika live kwenye kampeni
 
OK

Ila kusema alijiona mjanja unakuwa "too extreme".

Kwani si alifahamu miaka mitano itaisha?
 
Ni machafuko kwa sababu Upinzani unajiamini utashinda uchaguzi kinyume na matakwa ya wapiga kura ambao wanangojea kuwapa kura nyingi CCM.

Hiyo ndo hali halisi.

Wenzenu wamezunguka nchi nzima na wameimaliza kuwa kununua jogoo mmoja matata sana wa kitoweo.

Kisha wasingizie wameporwa kura.

Sasa kama wasema utaingiza watu barabarani unakuwa watania au?

Hizo si ni vurugu hizo?
Mkuu mbona uko biased sana, unaposema walio wengi wapo unatumia basis gani? Ulifanya poll yoyote kufikia hilo hitimisho?

Kuhusu wapinzani kudai kuibiwa ingekua solved kwa uchaguzi kuwa huru na haki. Mfano uwazi uwepo tokea kuhesabu kura hadi kutangaza, tallying center za vyama zisiingiliwe, kampeni ziwe fair sio chama kimoja kunyimwa kiwanja cjui kuzuiwa na polisi n.k

Trust me upinzani utakubali matokeo mapema sana hakutokua na excuse.
 
Mbona jana ilani zimechambuliwa. Na sera ya wanawake imezinduliwa jana!! Mfano

1. devolution ili kuzipa mamlaka kadhaa serikali za majimbo/halmashauri kujiendesha.
2. Kuwekeza kwenye kampeni ya kuendeleza miji ili watu wasikimbilie mjini, na kupunguza regional disparities.
3. Kuhusisha zaidi sekta binafsi kwenye kusogeza uchumi mbele na serikali ibaki kma regulator tu. (Ikumbukwe agenda kuu ya chadema ni uchumi wa soko/market economy)
4. Kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kurahisisha access ya mitaji kwa graduates wasio na collaterals kuombea mkopo (Wamesema watasusha makato ya HESLB mpka 3%)
5. Kuongeza purchasing power ya wananchi kwa kupunguza mrundikano wa makato (target iwe 30% pekee ndio ikatwe kwenye mshahara/income ya mfanyakazi sio sasa ambapo inafika 48%+).

Summary tu ila ilani ilichambuliwa jana vizuri tu
Devolution mmecopy Kenya sio mawazo yenu.so hakuna mpya, hata hizo zingine am sure mmecopy hahaa.
 
Hpn mkuu hiyo sera ipo toka 2004 huko miaka 10 kabla Kenya hawajaanza kutumia mfumo wa majimbo.

Pia hta kucopy sio kitu kibaya maana unakua umejifunza kitu kipya. Mfano ''CHADEMA digital'' ni lazima tu itaigwa na vyama vingine hpa Africa mashariki na kati!! Maana inaendana na wakati uliopo
 
Back
Top Bottom