Uchaguzi 2020 Upinzani watoe Ilani zao za Uchaguzi yaani “Election Manifesto" acheni porojo hazina Tija

Vyama vya upinzani hawana mpango wa kukamata dola wamepanga kumpa heka heka tuu magufuli
Mkuu pengine ni mgeni kwenye siasa. Opposition nyingi sana duniani huwa zina malengo ya kuchukua dola lakini kwa gradual process sio spontaneous.

Mfano chama kikuu cha upinzani sauzi kinaitwa DA kilikua na lengo la kupunguza ushindi wa ANC walau ufike 50%. Na ichukue majimbo 100+. Na kiukweli malengo yapo realistic na walifanikiwa kiasi.

Je walikua wapumbavu? Mifano ipo mingi hta Kenya kule tuliona kuna vyama vilishiriki ili tu kuretain Majimbo na County walizomiliki na sio kuongeza. Case ya Wiper n.k

Ila Tanzania sijawahi ona chama kikisema kinagombea ili kishinde tu majimbo 100 na urais wafike 30%!!! Sasa ni lini hao wapinzani hawajawahi kuitaka dola?
 
kwani polepole anasemaje mkuu au ni yeye
 

Hiyo ilani ilisemaje kuhusu maisha ya watanzania, ajira na nyongeza ya mishahara ilisemaje kuhusu mazao ya kilimo kama korosho ilisemaje kuhusu wafanya biashara ilisemaje kuhusu uhuru wa wananchi kujiamulia mambo yao ilisemaje kuhusu uhuru wa vyombo vya habari ilisemaje kuhusu haku ya kuishi ya watanzani ilisemaje kuhusu ubora wa elimu na upatikaji wa madawa hospitalini, ilisemaje kuhusu pembejeo na nini kimafanyika katika hayo yote ni asilimia ngapi kama siyo sifuri
 
Ilani yao inasema "tuonyesheni sheria inayokataza kubadili wimbo wa taifa" afu wanataka tuwape nchi, hawana adabu kabisa!
 

Ndo nnachokimaanisha wananchi hawana ideas nini manifesto za upinzani.
 
Mbona jana ilani zimechambuliwa. Na sera ya wanawake imezinduliwa jana!! Mfano

1. devolution ili kuzipa mamlaka kadhaa serikali za majimbo/halmashauri kujiendesha.
2. Kuwekeza kwenye kampeni ya kuendeleza miji ili watu wasikimbilie mjini, na kupunguza regional disparities.
3. Kuhusisha zaidi sekta binafsi kwenye kusogeza uchumi mbele na serikali ibaki kma regulator tu. (Ikumbukwe agenda kuu ya chadema ni uchumi wa soko/market economy)
4. Kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kurahisisha access ya mitaji kwa graduates wasio na collaterals kuombea mkopo (Wamesema watasusha makato ya HESLB mpka 3%)
5. Kuongeza purchasing power ya wananchi kwa kupunguza mrundikano wa makato (target iwe 30% pekee ndio ikatwe kwenye mshahara/income ya mfanyakazi sio sasa ambapo inafika 48%+).

Summary tu ila ilani ilichambuliwa jana vizuri tu
 
Ndo nnachokimaanisha wananchi hawana ideas nini manifesto za upinzani.
Imezinduliwa jana tu so tuipe muda kufikia kampeni itakua imeshasambazwa sana.

Pia si kweli kuwa ilani ya CCM imetekelezwa zaidi ya 80%. Mie binafsi nlifanya kautafiti kadogo nikagundua ni below 60%
*Mfano meli tano kubwa za uvuvi
*Kuongeza mara 2 eneo la kilimo cha kisasa
*Kutengeneza ajira mamilion kupitia viwanda
*Kutengeneza ajira za moja kwa moja 6000 kwa kupitia shughuli za uvuvi bahari kuu (kutumia hizo meli 5)

Sasa ukipima multitude ya hizo ahadi na utekelezaji wake huwezi sema ni 80%. Niko tayari twende kipengele kwa kipengele kuprove nachosema
 

Tusema ni 50%

Na CCM ikishinda october 28 itakamilisha hizo 40%

Wapinzani wakipewa nchi hii wataivuruga sana na kutatokea machafuko halafu mabeberu ndo watakuja kuamua.

CCM na JPM wao wapimwe baada ya miaka 10 kama wengine walopita.

Nafahamu maumivu ni makali lakini ni bora iwe hivyo ili kurekebisha kabisa baadhi yetu watanzania wenye kitu chaitwa " Thick Mentality".

President Magufuli is the right man to take that charge.

Mentality yetu iko thick sana kiasi cha kushindwa kutambua kuwa unakaa meza moja na mkoloni wa zamani kupanga njama dhidi ya nchi yako tena ukiwa nje.
 
Tusema ni 50%

Na CCM ikishinda october 28 itakamilisha hizo 40%

Wapinzani wakipewa nchi hii wataivuruga sana na kutatokea machafuko halafu mabeberu ndo watakuja kuamua.

CCM na JPM wao wapimwe baada ya miaka 10 kama wengine walopita.
Mkuu ilani ni miaka mitano tu na wao wanajua hivyo ndio maana mpango wa taifa wa maendeleo ni miaka 5 pia so hawana excuse kushindwa kutekeleza ilani yao.

2. Pia unaonyesha bias kwenye analysis yako kwamba kutatokea machafuko. Je unatumia basis gani kusema hivo? Mbona halmashauri zaidi ya 25 zilikua chini ya upinzani ila hayakutokea machafuko? Mbona kule zanzibar CUF iliunda SUK 2010-15 haikutokea hayo machafuko? Je nini kimebadilika?

3. Hapana chaguzi ni baada ya miaka 5 ndio maana anapimwa sahivi kupitia alichoahidi 2015. Mfano Tz ya viwanda mpaka sasa hakuna dalili. Imagine TFDA hawa standards za kugrade "Food Supplements za Korosho" ndio sembuse viwanda?.

Magufuli kafanikiwa kwenye miundombinu pekee kma Kikwete tu alivyojenga barabara nchi nzima (Hayana ubaya wowote maana ni uwekezaji wa muda mrefu) . Ila tukiwa wakweli kabisa kiuchumi bado sana, inatakiwa investment i-focus kwa human capital zaidi ili tupate kwanza purchasing power, hayo mengine yatapanuka tu kutokana na multiplier effect.
 
Porojo ni kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi wapinzani kutafuna trilion 1.5 kisha kumtoa CAG kafara?
 

Ni machafuko kwa sababu Upinzani unajiamini utashinda uchaguzi kinyume na matakwa ya wapiga kura ambao wanangojea kuwapa kura nyingi CCM.

Hiyo ndo hali halisi.

Wenzenu wamezunguka nchi nzima na wameimaliza kuwa kununua jogoo mmoja matata sana wa kitoweo.

Kisha wasingizie wameporwa kura.

Sasa kama wasema utaingiza watu barabarani unakuwa watania au?

Hizo si ni vurugu hizo?
 
Porojo ni kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi wapinzani kutafuna trilion 1.5 kisha kumtoa CAG kafara?

Hizi hoja sasa hivi zimefifia sana mkuu.
 
Kwenye eneo la tukio ndipo utasikia mengi zaidi kwani magufuli alizuia mikutano ya siasa kinyume cha Sheria kwa miaka mitano akajiona ni mjanja sana, sasa wamekusanya madhambi yake yote watayaanika live kwenye kampeni
 
Kwenye eneo la tukio ndipo utasikia mengi zaidi kwani magufuli alizuia mikutano ya siasa kinyume cha Sheria kwa miaka mitano akajiona ni mjanja sana, sasa wamekusanya madhambi yake yote watayaanika live kwenye kampeni

OK

Ila kusema alijiona mjanja unakuwa "too extreme".

Kwani si alifahamu miaka mitano itaisha?
 
Mkuu mbona uko biased sana, unaposema walio wengi wapo unatumia basis gani? Ulifanya poll yoyote kufikia hilo hitimisho?

Kuhusu wapinzani kudai kuibiwa ingekua solved kwa uchaguzi kuwa huru na haki. Mfano uwazi uwepo tokea kuhesabu kura hadi kutangaza, tallying center za vyama zisiingiliwe, kampeni ziwe fair sio chama kimoja kunyimwa kiwanja cjui kuzuiwa na polisi n.k

Trust me upinzani utakubali matokeo mapema sana hakutokua na excuse.
 
Devolution mmecopy Kenya sio mawazo yenu.so hakuna mpya, hata hizo zingine am sure mmecopy hahaa.
 
Devolution mmecopy Kenya sio mawazo yenu.so hakuna mpya, hata hizo zingine am sure mmecopy hahaa.
Hpn mkuu hiyo sera ipo toka 2004 huko miaka 10 kabla Kenya hawajaanza kutumia mfumo wa majimbo.

Pia hta kucopy sio kitu kibaya maana unakua umejifunza kitu kipya. Mfano ''CHADEMA digital'' ni lazima tu itaigwa na vyama vingine hpa Africa mashariki na kati!! Maana inaendana na wakati uliopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…