Upo chuo au hauna ajira ila unamiliki simu ya laki tatu na kuendelea? Tumia mbinu hii kupata pesa ya kujikimu kimaisha (nunua camera)

Upo chuo au hauna ajira ila unamiliki simu ya laki tatu na kuendelea? Tumia mbinu hii kupata pesa ya kujikimu kimaisha (nunua camera)

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Biashara ya kupiga picha inafaa sana kwa mtu yeyote anayepitia changamoto ya kukosa pesa ya kujikimu iwe mtaani au chuoni.

Kama unamiliki simu inayoanzia laki tatu na kuendelea ila hauna ajira, ni kheri kuuza simu na kununua DIGITAL CAMERA ya kisasa ambayo utapiga picha za aina zote kwa gharama ya Tsh 1000 au 2000 kulingana na event. Passport size 1500 mpaka 3000.

Kwa aliye chuo hii biashara inalipa kipindi cha usajili wa wa wanafunzi pia hata baada ya usajili.

Watu wengi siku hizi wanapenda kupost picha nzuri mtandaoni ila wanamiliki simu zisizo piga picha nzuri hii ni fursa.

Kwq aliye mtaani sehemu zenye mkusanyiko wa watu, kwenye masherehe, misiba n.k kote huko huwezi kukosa dili.

Mkakati wa kupata wateja

unatafuta mtu ambaye ni kibarua ktk biashara ya kukodisha TENT unamfanya awe informer wako kila wakipereka TENT sehemu akakustua wewe unampa ya soda, hawa ma infomer unakuwa nao kila palipo na biashara ya kukodisha TENTS.

Matangazo yote ya harusi kanisani yote hakikisha hayakupiti, rekodi tarehe husika na sehemu harusi itakapofanyika. Misiba yote hudhuria na camera yako.

Birthday party ukisikia ipo sehemu hudhuria na camera yako.

Ratiba zote za graduu kuanzia day care, shule ya msingi, sekondari hata chuo hakikisha unataarifa nazo, hudhuria na camera yako.

Siku zote za ibada, hasa hasa ROMAN CATHOLIC tega nje wakati wa kutoka utapata wateja wa kutosha
(Mengine mtaongezeq wadau)

Siku hauna dili unakaa popote hata kijiwe cha boda boda lazima utaokota wateja wawili watatu.

JILIPUE
Nunua camera yenye ubora mzuri mfano hii
GridArt_20240517_074513848.jpg

Ina wi-fi, app, video recorder n.k kwq bei ya amazon ni kama laki 6 na nusu, au hata kariakoo unaweza kupata ya bei nzuri hata kwa laki nne au tatu.
(Wataalam mtatoa elimu kwenye hiki kipengere)

Uzuri wa hii biashara unaweza kuifanya hata ukiww ndani ya ajira.

KABLA HAUJAANZA RASMI FANYA HIVI.
Muislam nenda msikitini ukasomewe dua na camera yako

Mkristo nenda kanisani kaombewe na camera yako ridhiki ifunguke

Wa kwa babu nenda akafanye yake

Kwq asiye na dini azame mzigoni hivo hivo.

JIFUNZE MAMBO MBALI MBALI KUHUSU UPIGAJI PICHA
Zama mtandaoni, download vitabu na video mbali mbali namna ya kupiga picha nzuri na kurecord video zenye ubora

Jielimishe zaidi

Ongeza ubunifu

FAIDA ZA HII KAZI KWA KIJANA MSOMI
Haikufanyi uchakae, pamba utatupia kama kawa

Haidhalilishi kama kazi zingine kama vile kubeba zege, kuzibua mitalo, kusaidia fundi, kuuza nyanya

Inaweza kukupa connection kwa kukutanisha na watu mbali mbali

Hautaweza kulala njaa wala kukosa elfu tano kwa siku

Ukitembea hutembei bure mawazo yanakuwa ni kusaka pesa.


Wakuu ongezeeni mnayojua kuhusu hii kazi ili wadau wajifunze

Ahsante
 
Shukrani sana mkuu ubarikiwe sana maelezo mazuri na yanajitosheleza ingekuwa Dunia nzima watu Wana akili kama wewe aisee tungeupiga chini umaskini.. Huna roho mbaya kama mimi
 
Shukrani sana mkuu ubarikiwe sana maelezo mazuri na yanajitosheleza ingekuwa Dunia nzima watu Wana akili kama wewe aisee tungeupiga chini umaskini.. Huna roho mbaya kama mimi
Mimi hua sio mchoyo hasa hasa hapa JF huwa nawapa watu ukweli kisha wataamua wao wenyewe
 
Back
Top Bottom