This kind of reasoning is regression. Ni kama kusema kwa vile x aliiba hukusema, y ameiba, naye usiseme. Au kama ulishindwa kumtibu mgonjwa p, kwa vile s ni mgonjwa naye usimtibu. Kwanza una uhakika gani kwamba hajakemea? Pili, tuseme kwamba hakukemea, unamaanisha maisha yake yote asikemee akiona mambo hayaendi au tuseme asikosoe jambo ambalo anaona halijafanyika vizuri? Kwa maneno mengine, Dr Kitima hana haki tena ya kukosoa au kutaka jambo lolote analoona halijafanyika vizuri lisifanywe vizuri/lisiboreshwe? Kwa nini? Sababu yake ni kwamba hujamsikia akikosoa Padri Elipidius Rwegoshora kutuhumiwa kushiriki kumuua mtoto mwenye albnism na tuhuma nyingine unazotoa. Sasa wewe unayemkosoa, tuonyeshe pia wapi ulimkosoa Fr Elipidius Rwegoshora, Padri wa Bunda kuwaibia masista, na Padri Stanslaus Sala wa Jimbo la Moshi kulawiti. Au wewe una haki ya kumkosoa Fr Kitima kama hujawakosoa hao wengine unaodai Fr Kitima hakuwakosoa? Nasubiri majibu ili kujiridhisha jinsi ulivyo 'consequent' na usiye na upofu kama Fr Kitima.