JACKLINE CELESTINE KITALE
Member
- Jul 29, 2021
- 81
- 158
Ushawahi kuchukua muda na kutathmini utofauti wa majina mengi ya Sasa na kipindi cha nyuma? Au unaona kila kitu Ni sawa?
Wengi wetu tumekuwa tukilalamika kuwa tamaduni zetu zimekuwa zikiharibiwa na wazungu na tamaduni za kigeni, lakini wakati mwingine tumekuwa tukichangia wenyewe katika upoteaji wa tamaduni hizi. Tumekuwa tukichukulia kuwa majina yetu ya kitamaduni kuwa Ni majina ya kishamba, magumu kwa wengine kushika, mabaya, hayana ladha na sababu zingine zisizokuwa na msingi. Wakati tukiyachukulia na majina ya kizungu Kama Jackline, Sara, Joseph, kuwa ni fahari zaidi kwakuwa tunakuwa tunaenda na wakati.
Jambo tunalo shindwa kutambua ni kwamba kadri tunavyo zidi kuyakataa majina yetu na kutumia majina ya wenzetu ndivyo majina yetu yanavyozidi kusahaulika na kupotea. Zamani watu walitumia majina ya kikabila, kuanzia jina lake la kwanza, la kati hadi la Babu au la ukoo yalikuwa ya ni majina ya kikabila. Ikaja wakati majina asili yakabaki tu kuwa ni majina ya baba na Babu.
Na kwasasa wengi wetu majina yetu ya kitamaduni tuliyonayo Ni majina ya ukoo tu, mfano Jackline Celestine Kitale, majina mawili ya kwanza Ni ya kizungu la mwisho ndo la kitanzania. Kuna wakati utafika hatutakuwa na jina hata moja la kitamaduni, Kuna wengine wakati huo umeshawafikia, unakuta mtu anaitwa Janet Lucas Joseph.
Najua kuna mtu hatoona kuwa hili Ni tatizo, kwasasa unaweza usilione kama ni tatizo, lakini sote tunajua kuwa siku zote mbuyu huanza kama mchicha. Nchi zetu za kiafrika na hata nchi za nje tunakumbwa na changamoto kubwa ya tamaduni zetu kupotea. Na tunaweza tukaiona kwenye ishu ya utoaji wa majina kwa watoto wetu. Zamani Ilikuwa mtu akikutajia jina lake tu, unaweza ukasema huyu mtu ametokea Nchi gani, mkoa gani na kabila lake ni lipi. Hii ilileta ufahari ndani ya mtu na utambuzi wa tutokapo. Lakini Sasa tumekuwa tukikataa majina yetu kisa ni mabaya na haya endi na wakati. Lakini tukumbuke kuwa, “Mkataa kwao ni mtumwa”.
Mwingine atasema majina hayo ni mabaya na yana maana mbaya. Kwanza nataka nikuulize Nani aliyekuambia hivyo? Nani amekuambia kuwa jina Shubira au Ntogwisangu ni baya, alafu jina Jackline Ni zuri? Kuna msemo ambao mtu aliusema, na nukuu, “ You don’t love your Culture because you have been Brainwashed” ambao kwa kiswahili unamaanisha, “ Hupendi Tamaduni yako kwasababu umepumbazwa”.
Hivi unadhani kwanini kiingereza na Tamaduni za Kimarekani zimeweza kupenya na kusambaa dunia nzima? Sababu moja wapo na nadhani hii ndio sababu kuu, ni kwamba waliweza kutupumbaza sisi na kutuaminisha ya kuwa tamaduni zetu kuanzia lugha zetu za kikabila (indigenous languages), majina yetu ya kitamaduni, nywele zetu, mawazi yetu, vyakula vyetu hazina thamani kulinganisha na vya kwao, na ndio maana hata wazazi hawako tayari kuwapa watoto wao majina ya kitamaduni.
Umeona siku hizi jinsi nchi nyingine zinavyotumia nguvu nyingi kuhakikisha lugha na tamaduni inasambaa duniani kote. Mfano ni Korea, hasa Korea ya kusini, wanatumia nguvu nyingi sana kuanzisha center za Kikorea Afrika nzima na kufundisha lugha, na pia wanawapa majina ya Kikorea wanafunzi wao ambao wanajifunza lugha hiyo na wanahakikisha wanatumia majina waliyowapa. Na sio Korea tu, Kuna wachina pia, nchi zote hi zinajitahidi kusambaza tamaduni zao kwetu, kwasababu wanajua wasipo fanya hivi tamaduni zao zitapotezwa na hili wimbi la utandawazi.
Ukweli Ni kwamba majina yetu tunayopewa au tuliyopewa ya kikabila huwa yana maana zake, mfano Shubira maana yake ni Tegemeo, Byela maana yake Ni Furaha, Munishi maana yake ni mwenye Shamba, Kitale (Chitale) maana yake ni Simba.
NINI KIFANYIKE KUTATUA TATIZO:
Kwakuwa fikra zetu potofu ndio zilitupelekea kuingia katika changamoto hii, basi hatuna budi kutumia fikra kujiengua.
Tumeekewa fikra mtazamo ya kuwa majina yetu ya asili Ni mabaya, basi tunatakiwa tubadili mtazamo huo mbaya.
Wewe uliye na jina lako la asili lipende na ulionee fahari maana si wengi waliokuwa nalo, na unaweza kuchukua hatua zaidi na kutafuta maana ya jina Hilo kama hufaamu. Unaweza kuuliza wazazi waliokupa jina lako la asili, au mtu yeyote anayeweza kuwa na huo utambuzi.
Pia, kwakuwa sisi ni wazazi na kwa wengine wanategemea kuwa wazazi hapo baadae, tuchukue muda wa kuangalia majina yetu ya asili ambayo tunaweza kuwapa watoto wetu, lakini tuwe makini pia katika uchaguzi huo, kwasababu, kama majina ya kizungu, majina yetu ya asili pia, mengine huwa yanatolewa kulinganisha na mambo yaliyotokea, na mambo hayo huwa sio mazuri. Mfano mtoto anapewa jina linalo maanisha Msiba, Ukame, Mafuriko na mengine.
Je, wewe unajina la Asili? Unalionea fahari au unalionea haya?