Upoteaji wa majina ya asili ya Waafrika

Upoteaji wa majina ya asili ya Waafrika

Tunaogopa kuwapa watoto majina ya asili kwa sababu wenye majina hawapo, wamekufa wengine tushagombana n koo z afamilia kwa kushikana uchawi, wengine tangu tuondoke uko vijijini tangu tuondoke hatujarudi tunaogopa kulogwa sasa nani atawafanyia mambo ya asili endapo jambo likitokea usicheze na mambo ya asili kama ujui utajuta

Mnasema watoto wenu hawana akili darasani, mabinti mnalalamika hamzai wengine hamuolewi unazani shida inaanzia wapi shida ni hayo majina hayo mtoto unamwita kinjekitile, mkwawa, kashindye ujui mila na matambiko
Ndo manabii wa siku hizi wanawadanganya,
 
hongera sana kwa uzi huu mzuri. Hili jambo huwa nalifikiria sana aisee. Yaani tumepoteza identity yetu kabisa. Na hili kwa kiasi kikubwa linachagizwa na dini za kigeni tulizoletewa. Mfano, Kwa wakristo wanakwambia kabisa mtoto wakati wa kubatizwa apewe jina la kikristo, hapa wanakuwa washakulimit kutumia jina lako la asili kwa kisingizio cha dini. Kwani tujiulize, huwezi kuwa mkristo au muislam na ukatumia jina lako la asili.? Je jina lako ndo tiketi ya kuiona pepo?
Mbona west africans ni waumini wa hizi dini tulizoletewa na wengi wao wanatumia majina yao ya asili?

Pili, haya majina yanachagizwa na ulimbukeni wa wazazi ambao wanadhani jina la kizungu ni superior kwa jina kiafrica. Wapo radhi kulikejeli na kulicheka jina la asili na kulitukuza jina la kigeni. Huu ni upotokaji wa kiwango kikubwa sana. Yaani mtu yuko proud kuitwa jina la muarabu au mzungu ila asiitwe jina ala asili yake!

Hivi wazungu/ waarabu tuliwa jiuliza huwa wanatufikiriaje wakisikia tunajiita majina yao?
 
Ushawahi kuchukua muda na kutathmini utofauti wa majina mengi ya Sasa na kipindi Cha nyuma? Au unaona kila kitu Ni sawa?

Wengi wetu tumekuwa tukilalamika kuwa tamaduni zetu zimekuwa zikiharibiwa na wazungu na tamaduni za kigeni, lakini wakati mwingine tumekuwa tukichangia wenyewe katika upoteaji wa tamaduni hizi. Tumekuwa tukichukulia kuwa majina yetu ya kitamaduni kuwa Ni majina ya kishamba, magumu kwa wengine kushika, mabaya, hayana ladha na sababu zingine zisizokuwa na msingi. Wakati tukiyachukulia na majina ya kizungu Kama Jackline, Sara, Joseph, kuwa ni fahari zaidi kwakuwa tunakuwa tunaenda na wakati.

Jambo tunalo shindwa kutambua ni kwamba kadri tunavyo zidi kuyakataa majina yetu na kutumia majina ya wenzetu ndivyo majina yetu yanavyozidi kusahaulika na kupotea. Zamani watu walitumia majina ya kikabila, kuanzia jina lake la kwanza, la kati hadi la Babu au la ukoo yalikuwa ya ni majina ya kikabila. Ikaja wakati majina asili yakabaki tu kuwa ni majina ya baba na Babu.

Na kwasasa wengi wetu majina yetu ya kitamaduni tuliyonayo Ni majina ya ukoo tu, mfano Jackline Celestine Kitale, majina mawili ya kwanza Ni ya kizungu la mwisho ndo la kitanzania. Kuna wakati utafika hatutakuwa na jina hata moja la kitamaduni, Kuna wengine wakati huo umeshawafikia, unakuta mtu anaitwa Janet Lucas Joseph.

Najua kuna mtu hatoona kuwa hili Ni tatizo, kwasasa unaweza usilione kama ni tatizo, lakini sote tunajua kuwa siku zote mbuyu huanza kama mchicha. Nchi zetu za kiafrika na hata nchi za nje tunakumbwa na changamoto kubwa ya tamaduni zetu kupotea. Na tunaweza tukaiona kwenye ishu ya utoaji wa majina kwa watoto wetu. Zamani Ilikuwa mtu akikutajia jina lake tu, unaweza ukasema huyu mtu ametokea Nchi gani, mkoa gani na kabila lake ni lipi. Hii ilileta ufahari ndani ya mtu na utambuzi wa tutokapo. Lakini Sasa tumekuwa tukikataa majina yetu kisa Ni mabaya na haya endi na wakati. Lakini tukumbuke kuwa, “ Mkataa kwao ni mtumwa”.

Mwingine atasema majina hayo ni mabaya na yana maana mbaya. Kwanza nataka nikuulize Nani aliyekuambia hivyo? Nani amekuambia kuwa jina Shubira au Ntogwisangu ni baya, alafu jina Jackline Ni zuri? Kuna msemo ambao mtu aliusema, na nukuu, “ You don’t love your Culture because you have been Brainwashed” ambao kwa kiswahili unamaanisha, “ Hupendi Tamaduni yako kwasababu umepumbazwa”.

Hivi unadhani kwanini kiingereza na Tamaduni za kimarekani zimeweza kupenya na kusambaa dunia nzima? Sababu moja wapo na nadhani hii ndio sababu kuu, Ni kwamba waliweza kutupumbaza sisi na kutuaminisha ya kuwa tamaduni zetu kuanzia lugha zetu za kikabila ( indigenous languages), majina yetu ya kitamaduni, nywele zetu, mawazi yetu, vyakula vyetu hazina thamani kulinganisha na vya kwao, na ndio maana hata wazazi hawako tayari kuwapa watoto wao majina ya kitamaduni.

Umeona siku hizi jinsi nchi nyingine zinavyotumia nguvu nyingi kuhakikisha lugha na tamaduni inasambaa duniani kote. Mfano ni Korea, hasa Korea ya kusini, wanatumia nguvu nyingi sana kuanzisha center za Kikorea Afrika nzima na kufundisha lugha, na pia wanawapa majina ya Kikorea wanafunzi wao ambao wanajifunza lugha hiyo na wanahakikisha wanatumia majina waliyowapa. Na sio Korea tu, Kuna wachina pia, nchi zote hi zinajitahidi kusambaza tamaduni zao kwetu, kwasababu wanajua wasipo fanya hivi tamaduni zao zitapotezwa na hili wimbi la utandawazi.

Ukweli Ni kwamba majina yetu tunayopewa au tuliyopewa ya kikabila huwa yana maana zake, mfano Shubira maana yake ni Tegemeo, Byela maana yake Ni Furaha, Munishi maana yake ni mwenye Shamba, Kitale (Chitale) maana yake ni Simba.

NINI KIFANYIKE KUTATUA TATIZO:
Kwakuwa fikra zetu potofu ndio zilitupelekea kuingia katika changamoto hii, basi hatuna budi kutumia fikra kujiengua.

Tumeekewa fikra mtazamo ya kuwa majina yetu ya asili Ni mabaya, basi tunatakiwa tubadili mtazamo huo mbaya.

Wewe uliye na jina lako la asili lipende na ulionee fahari maana si wengi waliokuwa nalo, na unaweza kuchukua hatua zaidi na kutafuta maana ya jina Hilo kama hufaamu. Unaweza kuuliza wazazi waliokupa jina lako la asili, au mtu yeyote anayeweza kuwa na huo utambuzi.

Pia, kwakuwa sisi Ni wazazi na kwa wengine wanategemea kuwa wazazi hapo baadae, tuchukue muda wa kuangalia majina yetu ya asili ambayo tunaweza kuwapa watoto wetu, lakini tuwe makini pia katika uchaguzi huo, kwasababu, kama majina ya kizungu, majina yetu ya asili pia, mengine huwa yanatolewa kulinganisha na mambo yaliyotokea, na mambo hayo huwa sio mazuri. Mfano mtoto anapewa jina linalo maanisha Msiba, Ukame, Mafuriko na mengine.

Je wewe unajina la Asili? Unalionea fahari au unalionea haya?

Watoto wangu nimewapa majina ya kiafrika tu. Na hapa niliamua kuwa mbabe kidogo. Wake zangu nimewakataza kuwapa watoto majina sijui za kikristu au kizungu.

Huwa nawapa wake zangu nafasi ya kuchagua majina ila kwa maelekezo na sharti moja tu, lazima majina yawe ya kiafrika la sivyo natumia turufu yangu kutoa jina na hakuna mjadala katika hilo.

Pia nimekataa, hakuna mwanangu kuniita sijui daddy, mimi ni baba. Full stop.

Lugha pia za asili na kiswahili ndo nawafundisha watoto. Kiingereza wanajifunzia shuleni.

Huu ni msimamo wangu kama binadamu ninayejitambua.
 
Je wewe unajina la Asili? Unalionea fahari au unalionea haya?
Master wazungu wametuletea system yakijinga sana na kwa kweli wametuweza kw asilimia zote kwakuwa hata milima ,maziwa,mbuga za wanyama walibatiza wao ,angalia mlima kilimanjaro,tizama olduvai george,chekshia ziwa victoria ,geukia amboni tanga,
Haya njoo kwenye vitu vya asili angalia hata kuku wameleta chotara,ng'ombe ,nguruwe,mbuzi,mbegu za mazao zote ,miti ya muda mfupi,angalia hata lugha sasa uzungu ndio ujanja........yote wamegeuza na kuleta uzungu hybrid,,,,wametung'oa mazima yote kwa yote tuwaombee Maasai waendelee na utamaduni wa asili uliobaki wakiafrika japo watatoweka nao au kubadlishwa mojakwamoja,utashangaa watoto wanaozaliwa sasa wakiitwa Putin,Zulensky na mengineyo.....tumekwisha
 
Baada ya wa marekani weusi kuacha majina ya asili na kuanza kutumia ya kizungu ilibidi 🆔 card zao zianze kutaja na rangi ya mwenye hiyo 🆔 kama huyo John McCain ni black au Caucasian
 
Maskini na Wasiosoma ndio huita watoto wao majina ya Gooogle lkn watu wanaojielewa majina ya Kooo zao yapo mpaka kesho. Hongera sana WACHAGA kwa hili. Ukitaka kuamini Vuta Majina ya Wanafunzi FEDHA SCHOOLS au ST. JOSEPH linganisha na Majina ya MADENGE au MBURAHATI S/M utapata majibu. Anyway
Wizara ya utamaduni isaidie kuweka kwenye TOVUTI makabila yote ya Nchi, Majina ya Makabila yote na Maana zake hakika tutaacha Urithi mkubwa sana kwa Vizazi vijavyo, maaana uwekaji wa Majina hayo kwenye maandishi kutafanya mimi MUHA ninayeitwa NDIKWEGA nimuite mwanangu NJOVU lenye asili ya RUVUMA kwa maaana nitakua ninajua Njovu inamaanisha nini.
Lkn Wizara ipo ipo tuuu haina Vision wala Mission kuhusu Utamaduni wa Mtanzania.
Tovuti yao huwezi pata hata majina ya Ngoma za Asili za Makabila yetu zinaitwaje. Lizombe huikuti, Rirandi huikuti, Kizangara ya Wafipa huikuti unabaki kusema Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Wasukuma na wamasai kwa hili wamejitahidi ila wachaga na wahaya wanaongoza kuita watoto ,majina ya kizungu
 
Mtu mweusi anaitwa
Peter John Jacob.
Antony Peter Petro.
Antonio John Mathias.
Elizabeth Eliah Michael.
Mariam Michael John
Esau John Peter...

Huku ni kuendeleza ukoloni...

Tulipaswa kuitwa..
Ulimwengu Tanzania Tabora.
Chamtuchake Dodo Achimwene.
Msambwanda Ndiowangu urithi.
Mboondefu Mkazuzu Meza.
Fungameza Muganyizi rweyemamu.
Rweyemamu kashaija nyaishozi.
Akiba haiozi wa lindi.
Masawe marandu

Majina yetu yaasili yangetusaidia sana kulinda asili yetu duniani na ingekuwa rahisi dunia kutambua watanzania...

Hapa ndio tunasema pia tumetawaliwa kiutamaduni....
Ongezea pia mtu mweusi anaitwa Abdoul razack majid au fatma masoud
 
Kuna haja kama taifa kuliangalia hili swala kwa ssa mpaka mtu ataje mpaka jina la 3 ndipo utagundua ni mtu wa sehemu gani mfano mimi ...NOEL ANTHONY KIMWERY kupitia jina langu la 3 ndipo utagundua ...aaahh kumbe [emoji12]
 
Back
Top Bottom