Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maskini na Wasiosoma ndio huita watoto wao majina ya Gooogle lkn watu wanaojielewa majina ya Kooo zao yapo mpaka kesho. Hongera sana WACHAGA kwa hili. Ukitaka kuamini Vuta Majina ya Wanafunzi FEDHA SCHOOLS au ST. JOSEPH linganisha na Majina ya MADENGE au MBURAHATI S/M utapata majibu. Anyway
Wizara ya utamaduni isaidie kuweka kwenye TOVUTI makabila yote ya Nchi, Majina ya Makabila yote na Maana zake hakika tutaacha Urithi mkubwa sana kwa Vizazi vijavyo, maaana uwekaji wa Majina hayo kwenye maandishi kutafanya mimi MUHA ninayeitwa NDIKWEGA nimuite mwanangu NJOVU lenye asili ya RUVUMA kwa maaana nitakua ninajua Njovu inamaanisha nini.
Lkn Wizara ipo ipo tuuu haina Vision wala Mission kuhusu Utamaduni wa Mtanzania.
Tovuti yao huwezi pata hata majina ya Ngoma za Asili za Makabila yetu zinaitwaje. Lizombe huikuti, Rirandi huikuti, Kizangara ya Wafipa huikuti unabaki kusema Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Wakina yohana na wakina hamis walikufa kitamboTunaogopa kuwapa watoto majina ya asili kwa sababu wenye majina hawapo, wamekufa wengine tushagombana n koo z afamilia kwa kushikana uchawi, wengine tangu tuondoke uko vijijini tangu tuondoke hatujarudi tunaogopa kulogwa sasa nani atawafanyia mambo ya asili endapo jambo likitokea usicheze na mambo ya asili kama ujui utajuta
Mnasema watoto wenu hawana akili darasani, mabinti mnalalamika hamzai wengine hamuolewi unazani shida inaanzia wapi shida ni hayo majina hayo mtoto unamwita kinjekitile, mkwawa, kashindye ujui mila na matambiko
Hii kitu bana iliwahi kunitokea mwaka 2017 nilienda nchi flan za mbali, ukaguzi immigration yao aliekuwa counter akaniambia "when i saw your name i thought you are a white man" nikamwambia ni majina ya kikristo akaniambia kabla ya ukristo aliekuwa anaitwa John alibadili jina? Shortly ni fedheha kiasi chake na haya sio ya kikristo au Islamic ni majina ya wazungu na waarabu.. Kutokea pale nimewapa watoto wangu majina ya kilugha maana mm kubadilisha siwezi yapo kwenye documents muhimuhongera sana kwa uzi huu mzuri. Hili jambo huwa nalifikiria sana aisee. Yaani tumepoteza identity yetu kabisa. Na hili kwa kiasi kikubwa linachagizwa na dini za kigeni tulizoletewa. Mfano, Kwa wakristo wanakwambia kabisa mtoto wakati wa kubatizwa apewe jina la kikristo, hapa wanakuwa washakulimit kutumia jina lako la asili kwa kisingizio cha dini. Kwani tujiulize, huwezi kuwa mkristo au muislam na ukatumia jina lako la asili.? Je jina lako ndo tiketi ya kuiona pepo?
Mbona west africans ni waumini wa hizi dini tulizoletewa na wengi wao wanatumia majina yao ya asili?
Pili, haya majina yanachagizwa na ulimbukeni wa wazazi ambao wanadhani jina la kizungu ni superior kwa jina kiafrica. Wapo radhi kulikejeli na kulicheka jina la asili na kulitukuza jina la kigeni. Huu ni upotokaji wa kiwango kikubwa sana. Yaani mtu yuko proud kuitwa jina la muarabu au mzungu ila asiitwe jina ala asili yake!
Hivi wazungu/ waarabu tuliwa jiuliza huwa wanatufikiriaje wakisikia tunajiita majina yao?
Tuko pamoja kwenye hili...Licha ya mimi kupewa jina la kukopa toka Ujerumani kwa kisingizio eti ni jina la kikristo (ujinga wa aina yake), baada ya kuokoka toka kwenye utumwa huo wa fikra, watoto wangu wote wanapewa majina ya asili toka sehemu mbalimbali Afrika. Nimegombana na ndugu zangu lakini sijali, watanielewa siku na wao wakiokoka.
Kuna jamaa yangu ana watoto 8 na watoto 7 wana majina ya asili sasa hawa watoto wote hakuna aliyemzima ni mwendo wa kuumwa kila wakati hebu tazama kuna kipindi watoto 3 walilazwa kwa pamoja kuna aliyekuwa bugando, Sekwao Toure (Seketule) na Mhimbili na wengine nyumbani baadhi wanalipuka mapepo n.k ila huyu mwingine 1 asiye na hayo majina hana shida yoyote akaja gundua baba yake na mama yake dada zake shangazi zake wengi ni wachawi wa kutupwa hivyo wanachezea watoto tangu nilipoona hili tukio la huyu bwana tena kwa macho yangu na wala si kusimuliwa HAKUNA MWANANGU ATAITWA HAYO MAJINATunaogopa kuwapa watoto majina ya asili kwa sababu wenye majina hawapo, wamekufa wengine tushagombana n koo z afamilia kwa kushikana uchawi, wengine tangu tuondoke uko vijijini tangu tuondoke hatujarudi tunaogopa kulogwa sasa nani atawafanyia mambo ya asili endapo jambo likitokea usicheze na mambo ya asili kama ujui utajuta
Mnasema watoto wenu hawana akili darasani, mabinti mnalalamika hamzai wengine hamuolewi unazani shida inaanzia wapi shida ni hayo majina hayo mtoto unamwita kinjekitile, mkwawa, kashindye ujui mila na matambiko
Mkuu hawezi kukuelewa majina ya kurithi mabaya sana,Kuna jamaa yangu ana watoto 8 na watoto 7 wana majina ya asili sasa hawa watoto wote hakuna aliyemzima ni mwendo wa kuumwa kila wakati hebu tazama kuna kipindi watoto 3 walilazwa kwa pamoja kuna aliyekuwa bugando, Sekwao Toure (Seketule) na Mhimbili na wengine nyumbani baadhi wanalipuka mapepo n.k ila huyu mwingine 1 asiye na hayo majina hana shida yoyote akaja gundua baba yake na mama yake dada zake shangazi zake wengi ni wachawi wa kutupwa hivyo wanachezea watoto tangu nilipoona hili tukio la huyu bwana tena kwa macho yangu na wala si kusimuliwa HAKUNA MWANANGU ATAITWA HAYO MAJINA
Tatizo africa ktk koo zetu kuna mambo machafu na ya ajabu ila hatupendi hata kuyajadili unaweza jikuta unateseka ktk maisha yako yoote ya hapa duniani kisa majina ambayo kwa hakika hatujui hao wahenga wetu walikuaje. Mfano kuna jamaa alimaliza form 6 1992 PCB kutoka shule kubwa flani hapa nchini alipata division 1.5 yaani alikuwa BBA kabla ya kujiunga na MUHAS aliumwa miaka 3 yupo home na baadae akajiunga MUHAS akaumwa tena mwisho akaambiwa ili apone inabidi awe mganga wa kienyeji na kweli alipokubali akapona sasa hivi anatibu watu huko kijijini ana manywele mareefu kama jini lililofufuka hana mbele wala nyuma.
Kwani lazima liwe jina la kurith?Mkuu hawezi kukuelewa majina ya kurithi mabaya sana,
Kwaiyo unaitaji balyugaba aitwe uchagani siyo au masawe aitwe usukumani, au boke aitwe uzaramuniKwani lazima liwe jina la kurith?
Hakuna uhusiano wa majina ya asili na hayo uliyoyataja.kwasababu ata hayo majina ya kigeni tunayoyatumia ni majina ya asili ya uko yalikotoka.Leo unaona matambiko mabaya kwasababu umeletewa Mungu mwingine ukamwamini tofauti na yule wa zamani.Umaskini wetu unatokana na ujinga.Mambo mengi ya asili yanaendana na uchawi.Majina ya asili yapo connected na mizimu na matambiko. Mizimu na matambiko ndo chanzo jinsi waafrika tulivyo, matatizo, umasikini, magonjwa chanzo ni mizimu. Mizimu haitaki maendeleo, hofu watu wakiwa na maendeleo wataelimika wataacha kutambika mizimu.
Tambiko lina faida gani, waafrika wameanza kutambika hata kabla ya ujio wa wageni,nini wamepata.Wenzetu weupe wapo vile sababu hawana connection na upumbavu.Hakuna uhusiano wa majina ya asili na hayo uliyoyataja.kwasababu ata hayo majina ya kigeni tunayoyatumia ni majina ya asili ya uko yalikotoka.Leo unaona matambiko mabaya kwasababu umeletewa Mungu mwingine ukamwamini tofauti na yule wa zamani.Umaskini wetu unatokana na ujinga.
Dini ndio chanzo cha Mabadiliko ya tamaduni za jamii mbalimbali.Dini zimechangia sana hili tatizo
Bado nawalaani wakoloni, yaani mzungu na mwarabu.Ushawahi kuchukua muda na kutathmini utofauti wa majina mengi ya Sasa na kipindi Cha nyuma? Au unaona kila kitu Ni sawa?
Wengi wetu tumekuwa tukilalamika kuwa tamaduni zetu zimekuwa zikiharibiwa na wazungu na tamaduni za kigeni, lakini wakati mwingine tumekuwa tukichangia wenyewe katika upoteaji wa tamaduni hizi. Tumekuwa tukichukulia kuwa majina yetu ya kitamaduni kuwa Ni majina ya kishamba, magumu kwa wengine kushika, mabaya, hayana ladha na sababu zingine zisizokuwa na msingi. Wakati tukiyachukulia na majina ya kizungu Kama Jackline, Sara, Joseph, kuwa ni fahari zaidi kwakuwa tunakuwa tunaenda na wakati.
Jambo tunalo shindwa kutambua ni kwamba kadri tunavyo zidi kuyakataa majina yetu na kutumia majina ya wenzetu ndivyo majina yetu yanavyozidi kusahaulika na kupotea. Zamani watu walitumia majina ya kikabila, kuanzia jina lake la kwanza, la kati hadi la Babu au la ukoo yalikuwa ya ni majina ya kikabila. Ikaja wakati majina asili yakabaki tu kuwa ni majina ya baba na Babu.
Na kwasasa wengi wetu majina yetu ya kitamaduni tuliyonayo Ni majina ya ukoo tu, mfano Jackline Celestine Kitale, majina mawili ya kwanza Ni ya kizungu la mwisho ndo la kitanzania. Kuna wakati utafika hatutakuwa na jina hata moja la kitamaduni, Kuna wengine wakati huo umeshawafikia, unakuta mtu anaitwa Janet Lucas Joseph.
Najua kuna mtu hatoona kuwa hili Ni tatizo, kwasasa unaweza usilione kama ni tatizo, lakini sote tunajua kuwa siku zote mbuyu huanza kama mchicha. Nchi zetu za kiafrika na hata nchi za nje tunakumbwa na changamoto kubwa ya tamaduni zetu kupotea. Na tunaweza tukaiona kwenye ishu ya utoaji wa majina kwa watoto wetu. Zamani Ilikuwa mtu akikutajia jina lake tu, unaweza ukasema huyu mtu ametokea Nchi gani, mkoa gani na kabila lake ni lipi. Hii ilileta ufahari ndani ya mtu na utambuzi wa tutokapo. Lakini Sasa tumekuwa tukikataa majina yetu kisa Ni mabaya na haya endi na wakati. Lakini tukumbuke kuwa, “ Mkataa kwao ni mtumwa”.
Mwingine atasema majina hayo ni mabaya na yana maana mbaya. Kwanza nataka nikuulize Nani aliyekuambia hivyo? Nani amekuambia kuwa jina Shubira au Ntogwisangu ni baya, alafu jina Jackline Ni zuri? Kuna msemo ambao mtu aliusema, na nukuu, “ You don’t love your Culture because you have been Brainwashed” ambao kwa kiswahili unamaanisha, “ Hupendi Tamaduni yako kwasababu umepumbazwa”.
Hivi unadhani kwanini kiingereza na Tamaduni za kimarekani zimeweza kupenya na kusambaa dunia nzima? Sababu moja wapo na nadhani hii ndio sababu kuu, Ni kwamba waliweza kutupumbaza sisi na kutuaminisha ya kuwa tamaduni zetu kuanzia lugha zetu za kikabila ( indigenous languages), majina yetu ya kitamaduni, nywele zetu, mawazi yetu, vyakula vyetu hazina thamani kulinganisha na vya kwao, na ndio maana hata wazazi hawako tayari kuwapa watoto wao majina ya kitamaduni.
Umeona siku hizi jinsi nchi nyingine zinavyotumia nguvu nyingi kuhakikisha lugha na tamaduni inasambaa duniani kote. Mfano ni Korea, hasa Korea ya kusini, wanatumia nguvu nyingi sana kuanzisha center za Kikorea Afrika nzima na kufundisha lugha, na pia wanawapa majina ya Kikorea wanafunzi wao ambao wanajifunza lugha hiyo na wanahakikisha wanatumia majina waliyowapa. Na sio Korea tu, Kuna wachina pia, nchi zote hi zinajitahidi kusambaza tamaduni zao kwetu, kwasababu wanajua wasipo fanya hivi tamaduni zao zitapotezwa na hili wimbi la utandawazi.
Ukweli Ni kwamba majina yetu tunayopewa au tuliyopewa ya kikabila huwa yana maana zake, mfano Shubira maana yake ni Tegemeo, Byela maana yake Ni Furaha, Munishi maana yake ni mwenye Shamba, Kitale (Chitale) maana yake ni Simba.
NINI KIFANYIKE KUTATUA TATIZO:
Kwakuwa fikra zetu potofu ndio zilitupelekea kuingia katika changamoto hii, basi hatuna budi kutumia fikra kujiengua.
Tumeekewa fikra mtazamo ya kuwa majina yetu ya asili Ni mabaya, basi tunatakiwa tubadili mtazamo huo mbaya.
Wewe uliye na jina lako la asili lipende na ulionee fahari maana si wengi waliokuwa nalo, na unaweza kuchukua hatua zaidi na kutafuta maana ya jina Hilo kama hufaamu. Unaweza kuuliza wazazi waliokupa jina lako la asili, au mtu yeyote anayeweza kuwa na huo utambuzi.
Pia, kwakuwa sisi Ni wazazi na kwa wengine wanategemea kuwa wazazi hapo baadae, tuchukue muda wa kuangalia majina yetu ya asili ambayo tunaweza kuwapa watoto wetu, lakini tuwe makini pia katika uchaguzi huo, kwasababu, kama majina ya kizungu, majina yetu ya asili pia, mengine huwa yanatolewa kulinganisha na mambo yaliyotokea, na mambo hayo huwa sio mazuri. Mfano mtoto anapewa jina linalo maanisha Msiba, Ukame, Mafuriko na mengine.
Je wewe unajina la Asili? Unalionea fahari au unalionea haya?
Kwani tumeshatoka uchumi wa kati?Hayo majina ya asili yatatusaidia nini? au yataturejesha uchumi wa kati?
Usiwalaumu ni nature,ni kawaida ya itikadi dhaifu kufa inapopambana na itikadi yenye nguvu.Bado nawalaani wakoloni, yaani mzungu na mwarabu.
Matokeo yake ndio babu kurithi, baba kurithi na miye, kuanzia dini mpaka majina.
Msijali nilifanyia kazi wandugu
Ni Nchi gani hiyo ambayo institutional racism imetamaraki hivyo? Nchi nyingi za ulaya na America hata kusema Black man ni kosa. Utasikia wakisema coloured man, nkHii kitu bana iliwahi kunitokea mwaka 2017 nilienda nchi flan za mbali, ukaguzi immigration yao aliekuwa counter akaniambia "when i saw your name i thought you are a white man" nikamwambia ni majina ya kikristo akaniambia kabla ya ukristo aliekuwa anaitwa John alibadili jina? Shortly ni fedheha kiasi chake na haya sio ya kikristo au Islamic ni majina ya wazungu na waarabu.. Kutokea pale nimewapa watoto wangu majina ya kilugha maana mm kubadilisha siwezi yapo kwenye documents muhimu
Hii yote inatokana na ujinga wa kukumbatia dini na mila za watu kuwa ni zetu....mtu anaona ufahari kuitwa Mohammed au Daudi wakati hawa wote walikuwa vibaka tu. Yaani tunarithisha watoto wetu laana za watu wa kale wakati wangeweza kupewa majina ya kifahari toka kwa wazee wao.Ushawahi kuchukua muda na kutathmini utofauti wa majina mengi ya Sasa na kipindi Cha nyuma? Au unaona kila kitu Ni sawa?