Upoteaji wa majina ya asili ya Waafrika

Upoteaji wa majina ya asili ya Waafrika

Majina ya kitamaduni za Kiarabu nayo ndio balaa, mtu anajiona wa maana sana kujiita au kumpa mwanae jina kama Farhiya, Masoud, Mohammed, Juma, Abdulmalik n.k anajiona kama kaisha fika mbinguni!

Upande mwingine sasa kuna jina watoto wa kike sasa hivi wanapewa kabla hata hawajazaliwa Precious "Preshaz"!!

Ni ujinga unaoenda kwenye upumbavu!

Tumeiga kila kitu cha wageni, nguo, majina, nyumba, pombe, majina, miungu n.k
Kipi tulichobuni tukitumie.Ni nature kitu dhaifu ni lzm kife dhidi ya kitu bora
 
Hayo majina ya asili yatatusaidia nini? au yataturejesha uchumi wa kati?

Niache kumpa mtoto wangu majina mazuri ya kiislamu rashid, abdul, said, hassan n.k, eti nimpe majina ya ajabu ajabu yasiyo na mbele wa nyuma 😁
 
Tunaogopa kuwapa watoto majina ya asili kwa sababu wenye majina hawapo, wamekufa wengine tushagombana n koo z afamilia kwa kushikana uchawi, wengine tangu tuondoke uko vijijini tangu tuondoke hatujarudi tunaogopa kulogwa sasa nani atawafanyia mambo ya asili endapo jambo likitokea usicheze na mambo ya asili kama ujui utajuta

Mnasema watoto wenu hawana akili darasani, mabinti mnalalamika hamzai wengine hamuolewi unazani shida inaanzia wapi shida ni hayo majina hayo mtoto unamwita kinjekitile, mkwawa, kashindye ujui mila na matambiko
nani alikwambia hayo majina ya kizungu sio ya watu waliokufa. Au bado uko kwenye mzingo wa kuwa wazungu wamebarikiwa kuliko ww mweusi[emoji23][emoji1787]
 
Baada ya wa marekani weusi kuacha majina ya asili na kuanza kutumia ya kizungu ilibidi [emoji723] card zao zianze kutaja na rangi ya mwenye hiyo [emoji723] kama huyo John McCain ni black au Caucasian
At least black american naweza kuwapa pass kwa hili sababu babu zao hawakubadili kwa kupenda majina bali kwa MIJELEDI. Ila sisi huku hata bunduki hawakushika. Walishika tu kitabu cha dini na kutuambia kuwa "nyie mmelaaniwa" then tukaamini tukarithishana ujinga kizazi mpk kizazi. Kwamba majina ya wazungu yamebarikiwa[emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji1787] Na yetu eti ni full yamelaaniwa[emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787]Hadi mapadri/wachungaji walikuwa wanagoma kubatiza mtoto akipewa jina la kiafrica. Mpk utaje la kizungu..... UTUMWA WA FIKRA.....poor us.
 
Mambo mengi ya asili yanaendana na uchawi.Majina ya asili yapo connected na mizimu na matambiko. Mizimu na matambiko ndo chanzo jinsi waafrika tulivyo, matatizo, umasikini, magonjwa chanzo ni mizimu. Mizimu haitaki maendeleo, hofu watu wakiwa na maendeleo wataelimika wataacha kutambika mizimu.
nani alikwambia wazungu na majna yao hawana Mizimu uitajayo? Mtu anaitwa DICKSON .....serious[emoji1787][emoji23]
 
Kuna jamaa yangu ana watoto 8 na watoto 7 wana majina ya asili sasa hawa watoto wote hakuna aliyemzima ni mwendo wa kuumwa kila wakati hebu tazama kuna kipindi watoto 3 walilazwa kwa pamoja kuna aliyekuwa bugando, Sekwao Toure (Seketule) na Mhimbili na wengine nyumbani baadhi wanalipuka mapepo n.k ila huyu mwingine 1 asiye na hayo majina hana shida yoyote akaja gundua baba yake na mama yake dada zake shangazi zake wengi ni wachawi wa kutupwa hivyo wanachezea watoto tangu nilipoona hili tukio la huyu bwana tena kwa macho yangu na wala si kusimuliwa HAKUNA MWANANGU ATAITWA HAYO MAJINA

Tatizo africa ktk koo zetu kuna mambo machafu na ya ajabu ila hatupendi hata kuyajadili unaweza jikuta unateseka ktk maisha yako yoote ya hapa duniani kisa majina ambayo kwa hakika hatujui hao wahenga wetu walikuaje. Mfano kuna jamaa alimaliza form 6 1992 PCB kutoka shule kubwa flani hapa nchini alipata division 1.5 yaani alikuwa BBA kabla ya kujiunga na MUHAS aliumwa miaka 3 yupo home na baadae akajiunga MUHAS akaumwa tena mwisho akaambiwa ili apone inabidi awe mganga wa kienyeji na kweli alipokubali akapona sasa hivi anatibu watu huko kijijini ana manywele mareefu kama jini lililofufuka hana mbele wala nyuma.
We unajua wahenga wa kizungu walikuwaje. Unajua wao walikuwa wapagani waabudu washetani kuliko sisi.
 
Inawezekana jamaa yako ana magonjwa au matatizo ya kiafya ya kurithi yaliyojificha.
Kuna jamaa yangu ana watoto 8 na watoto 7 wana majina ya asili sasa hawa watoto wote hakuna aliyemzima ni mwendo wa kuumwa kila wakati hebu tazama kuna kipindi watoto 3 walilazwa kwa pamoja kuna aliyekuwa bugando, Sekwao Toure (Seketule) na Mhimbili na wengine nyumbani baadhi wanalipuka mapepo n.k ila huyu mwingine 1 asiye na hayo majina hana shida yoyote akaja gundua baba yake na mama yake dada zake shangazi zake wengi ni wachawi wa kutupwa hivyo wanachezea watoto tangu nilipoona hili tukio la huyu bwana tena kwa macho yangu na wala si kusimuliwa HAKUNA MWANANGU ATAITWA HAYO MAJINA

Tatizo africa ktk koo zetu kuna mambo machafu na ya ajabu ila hatupendi hata kuyajadili unaweza jikuta unateseka ktk maisha yako yoote ya hapa duniani kisa majina ambayo kwa hakika hatujui hao wahenga wetu walikuaje. Mfano kuna jamaa alimaliza form 6 1992 PCB kutoka shule kubwa flani hapa nchini alipata division 1.5 yaani alikuwa BBA kabla ya kujiunga na MUHAS aliumwa miaka 3 yupo home na baadae akajiunga MUHAS akaumwa tena mwisho akaambiwa ili apone inabidi awe mganga wa kienyeji na kweli alipokubali akapona sasa hivi anatibu watu huko kijijini ana manywele mareefu kama jini lililofufuka hana mbele wala nyuma.
 
Ushawahi kuchukua muda na kutathmini utofauti wa majina mengi ya Sasa na kipindi Cha nyuma? Au unaona kila kitu Ni sawa?

Wengi wetu tumekuwa tukilalamika kuwa tamaduni zetu zimekuwa zikiharibiwa na wazungu na tamaduni za kigeni, lakini wakati mwingine tumekuwa tukichangia wenyewe katika upoteaji wa tamaduni hizi. Tumekuwa tukichukulia kuwa majina yetu ya kitamaduni kuwa Ni majina ya kishamba, magumu kwa wengine kushika, mabaya, hayana ladha na sababu zingine zisizokuwa na msingi. Wakati tukiyachukulia na majina ya kizungu Kama Jackline, Sara, Joseph, kuwa ni fahari zaidi kwakuwa tunakuwa tunaenda na wakati.

Jambo tunalo shindwa kutambua ni kwamba kadri tunavyo zidi kuyakataa majina yetu na kutumia majina ya wenzetu ndivyo majina yetu yanavyozidi kusahaulika na kupotea. Zamani watu walitumia majina ya kikabila, kuanzia jina lake la kwanza, la kati hadi la Babu au la ukoo yalikuwa ya ni majina ya kikabila. Ikaja wakati majina asili yakabaki tu kuwa ni majina ya baba na Babu.

Na kwasasa wengi wetu majina yetu ya kitamaduni tuliyonayo Ni majina ya ukoo tu, mfano Jackline Celestine Kitale, majina mawili ya kwanza Ni ya kizungu la mwisho ndo la kitanzania. Kuna wakati utafika hatutakuwa na jina hata moja la kitamaduni, Kuna wengine wakati huo umeshawafikia, unakuta mtu anaitwa Janet Lucas Joseph.

Najua kuna mtu hatoona kuwa hili Ni tatizo, kwasasa unaweza usilione kama ni tatizo, lakini sote tunajua kuwa siku zote mbuyu huanza kama mchicha. Nchi zetu za kiafrika na hata nchi za nje tunakumbwa na changamoto kubwa ya tamaduni zetu kupotea. Na tunaweza tukaiona kwenye ishu ya utoaji wa majina kwa watoto wetu. Zamani Ilikuwa mtu akikutajia jina lake tu, unaweza ukasema huyu mtu ametokea Nchi gani, mkoa gani na kabila lake ni lipi. Hii ilileta ufahari ndani ya mtu na utambuzi wa tutokapo. Lakini Sasa tumekuwa tukikataa majina yetu kisa Ni mabaya na haya endi na wakati. Lakini tukumbuke kuwa, “ Mkataa kwao ni mtumwa”.

Mwingine atasema majina hayo ni mabaya na yana maana mbaya. Kwanza nataka nikuulize Nani aliyekuambia hivyo? Nani amekuambia kuwa jina Shubira au Ntogwisangu ni baya, alafu jina Jackline Ni zuri? Kuna msemo ambao mtu aliusema, na nukuu, “ You don’t love your Culture because you have been Brainwashed” ambao kwa kiswahili unamaanisha, “ Hupendi Tamaduni yako kwasababu umepumbazwa”.

Hivi unadhani kwanini kiingereza na Tamaduni za kimarekani zimeweza kupenya na kusambaa dunia nzima? Sababu moja wapo na nadhani hii ndio sababu kuu, Ni kwamba waliweza kutupumbaza sisi na kutuaminisha ya kuwa tamaduni zetu kuanzia lugha zetu za kikabila ( indigenous languages), majina yetu ya kitamaduni, nywele zetu, mawazi yetu, vyakula vyetu hazina thamani kulinganisha na vya kwao, na ndio maana hata wazazi hawako tayari kuwapa watoto wao majina ya kitamaduni.

Umeona siku hizi jinsi nchi nyingine zinavyotumia nguvu nyingi kuhakikisha lugha na tamaduni inasambaa duniani kote. Mfano ni Korea, hasa Korea ya kusini, wanatumia nguvu nyingi sana kuanzisha center za Kikorea Afrika nzima na kufundisha lugha, na pia wanawapa majina ya Kikorea wanafunzi wao ambao wanajifunza lugha hiyo na wanahakikisha wanatumia majina waliyowapa. Na sio Korea tu, Kuna wachina pia, nchi zote hi zinajitahidi kusambaza tamaduni zao kwetu, kwasababu wanajua wasipo fanya hivi tamaduni zao zitapotezwa na hili wimbi la utandawazi.

Ukweli Ni kwamba majina yetu tunayopewa au tuliyopewa ya kikabila huwa yana maana zake, mfano Shubira maana yake ni Tegemeo, Byela maana yake Ni Furaha, Munishi maana yake ni mwenye Shamba, Kitale (Chitale) maana yake ni Simba.

NINI KIFANYIKE KUTATUA TATIZO:
Kwakuwa fikra zetu potofu ndio zilitupelekea kuingia katika changamoto hii, basi hatuna budi kutumia fikra kujiengua.

Tumeekewa fikra mtazamo ya kuwa majina yetu ya asili Ni mabaya, basi tunatakiwa tubadili mtazamo huo mbaya.

Wewe uliye na jina lako la asili lipende na ulionee fahari maana si wengi waliokuwa nalo, na unaweza kuchukua hatua zaidi na kutafuta maana ya jina Hilo kama hufaamu. Unaweza kuuliza wazazi waliokupa jina lako la asili, au mtu yeyote anayeweza kuwa na huo utambuzi.

Pia, kwakuwa sisi Ni wazazi na kwa wengine wanategemea kuwa wazazi hapo baadae, tuchukue muda wa kuangalia majina yetu ya asili ambayo tunaweza kuwapa watoto wetu, lakini tuwe makini pia katika uchaguzi huo, kwasababu, kama majina ya kizungu, majina yetu ya asili pia, mengine huwa yanatolewa kulinganisha na mambo yaliyotokea, na mambo hayo huwa sio mazuri. Mfano mtoto anapewa jina linalo maanisha Msiba, Ukame, Mafuriko na mengine.

Je wewe unajina la Asili? Unalionea fahari au unalionea haya?
Kwa maeneo ya Pwani na Zenji ni shida..
Majina ya wenyeji yamepotea, ya Waarabu yanatamalaki🙄
 
Hiki kizazi cha nyoka hakitauelewa huu uzi kwa sasa. Ila siku zaja ambapo wajukuu, vitukuu na vilembwe vyetu vitaitafuta asili yao (utamaduni na mila) maana watajikuta majina yao ni kama ya wazungu lakini asili yao ni tofauti na wazungu.
Kula like
 
Kuna haja kama taifa kuliangalia hili swala kwa ssa mpaka mtu ataje mpaka jina la 3 ndipo utagundua ni mtu wa sehemu gani mfano mimi ...NOEL ANTHONY KIMWERY kupitia jina langu la 3 ndipo utagundua ...aaahh kumbe [emoji12]
Kimwery au Kimweri mbona mnaharibu majina nyie? Unakuta mtu anaitwa Mbala halafu anaweka double "l" (Mballa) ili iwaje sasa?
 
Mambo mengi ya asili yanaendana na uchawi.Majina ya asili yapo connected na mizimu na matambiko. Mizimu na matambiko ndo chanzo jinsi waafrika tulivyo, matatizo, umasikini, magonjwa chanzo ni mizimu. Mizimu haitaki maendeleo, hofu watu wakiwa na maendeleo wataelimika wataacha kutambika mizimu.
Vipi kuhusu South Africa?
 
Kwahiyo hayo majina ya wazungu wenye nayo wapo hawajafa si ndio? Hawakuwahi kugombana na koo zao si ndio? Walikuwa wako karibu sana na familia zao si ndio?

Hakuna watoto wa kizungu wasio na akili? Nawao hii inasababishwa nanini? Wamelogwa?

Hakuna wazungu ambao hawaolewi? Wamelogwa?

Hakuna wazungu ambao hawazai? Wamelogwa?
Jamaa katoa excuse ya kipumbavu
 
Back
Top Bottom