Upoteaji wa majina ya asili ya Waafrika

Kweli kabisa
 
Hayo majina ya asili yatatusaidia nini? au yataturejesha uchumi wa kati?
Jambo kama hili la majina linaweza lisionekane kama Jambo kubwa la kuhitaji kupewa umuhimu lakini siku zote mbuyu huanza kama mchicha. Na tabia yetu sisi watu wa rangi nyeusi ya kudharau mambo madogo ndio hutusababisha kuja kupata maafa makubwa baadae. Ningeweza kukuelezea Ni jinsi gani Jambo kama hili linavyoweza kuchangia kushika kwa uchumi lakini itahitaji niandike uzi mwinge kabisa. Lakini Nina uhakika ukichukua muda na ukiwa na hamu ya kujua zaidi na kufanya uchunguzi, utagundua kuwa hata Jambo dogo Kama hili lisipotatuliwa mapema litatuletea shida, na shida zingine zimeshaanza kujidhihirisha.
 
Uko sahihi
 
Hiki kizazi cha nyoka hakitauelewa huu uzi kwa sasa. Ila siku zaja ambapo wajukuu, vitukuu na vilembwe vyetu vitaitafuta asili yao (utamaduni na mila) maana watajikuta majina yao ni kama ya wazungu lakini asili yao ni tofauti na wazungu.
Umesema kwel, tusipofanya juhudi ya kutunza asili zetu watoto wetu hawatapata nafasi ya kujua wao Ni akina Nani, chimbuko lao. Na kwahilo itakuwa ngumu kwao kusimama na kuwa imara Kama hata hawajujui wao wametokea wapi.
 
Uko sahihi sana. Tunahutaji watu wenye msimamo Kama wewe, hongera.
 
Ni kweli kwamba dini zimechangia Sana katika kukuza tatizo hili. Lakini tukumbuke kuwa hizi dini zililetwa na hao wakoloni wakiwa na lengo lao walilotaka kulitimiza, dini sio mbaya lakini tusiwe walimbukeni wakutumia dini kama kisingizio au kitu Cha kutukandamiza hata maandiko yametuambia kuwa tutumie maarifa yetu tuliyopewa na Mungu (wanadamu wanaang'amia kwa kukosa maarifa). Inabidi tutumie maarifa ya kutambua kuwa hatuhitaji kuyakana majina yetu I'll twende mbinguni, Mungu mwenyewe alikuwa na sababu zake za kutufanya tuzaliwe Tanzania na kuwa na tamaduni hizi. Tulinde tamaduni zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…