Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
MAJIBU KWA MTU ANAYEJIITA JOSHUA GUYAHAMBI ANAVYOPOTOSHA UMMA WA WATANZANIA KUHUSU ADDO NA USIMAMIZI WA MADUKA YA DAWA NCHINI
Na Prof Patrick Kobono (MD, MMED, MPH, MBA, PhD in Human Anatomy)
Wasalaam!
Kwa kawaida hua sipendi kabisa kujibishana na wajinga wachache wanaopotosha umma ima kwa makusudi ili kukidhi tamaa na haja zake binafsi au kikundi fulani au ni ujinga unaotokana na yeye kutoelewa kwa sababu huenda hajui chochote au kuna tatizo mahali.
Kwanza amejiita Darasa la saba B, hii inadhihirisha ni jinsi gani alivyo na uelewa finyu kuhuhusu kozi ya famasia na utabibu au Uuguzi pamoja na huduma ya utoaji dawa nchini. Huwezi kua Darasa la saba halafu ukapata Moral authority ya kufanya simple analysis kumjibu profesa na mwalimu wa chuo kikuu. Kama wewe ni darasa la saba B ndio useme darasa la saba wanasomea wapi Famasia. Huu ni ujinga mtupu kutaka kupotosha umma wa watanzania bila kujali kua tunahangaika na afya zao. Unaleta porojo badala ya kuja na Details na majibu sahihi?
UKWELI NI HUU KUHUSU KOZI YA UDAKTARI, FAMASI NA UUGUZI NA NI NANI ANASTAHILI KUTOA DAWA?
Naomba kusema kwamba silengi kutweza taaluma za watu, ninaziheshimu sana lakini propaganda na upotoshaji unapozidi unatakiwa kujibiwa kwa hoja na ukweli kwani mwisho wa siku anayeumia ni mwananchi wa kawaida.
Kwa kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba Famasia chanzo chake ilikua ni sehemu au tawi la kozi Mama ya udaktari baada ya kuona kwamba daktari atakua na kazi nyingi za kutafiti, kutengeza dawa na kutibu, ulitolewa uamuzi baadaye kua masuala ya dawa yajitegemee ndio likaibuka somo la Pharmacology as a branch of Medicine ambaye mwanzilishi wake alikua Mjerumani Oswald Schmiedeberg. Huyu alikua ni daktari wa binadamu na ndiye mwanzilishi wa kwanza wa kozi ya Famasia karne ya 18. Unapokuja na kujitutumua kutaka kupotosha umma wa watanzania na bila kujali unamjibu nani ni utovu wa nidhamu.
Mwanzilishi na mgunduzi wa dawa Duniani Hippocrates, alikua daktari wa binadamu. He was the father of medicine. Ndiye aliyesababisha leo kuwepo na kozi ya Famasia, ndiye aliyekuja kuwazalisha kina Dr Oswald Shmiedeberg. Huwezi kupotosha umma wa watanzania bila kujali kua ushauri wangu ulijikita zaidi katika kuishauri Serikali ispotoshwe na kikundi cha watu wachache wachumia tumbo kwa maslahi yao binafsi bila kujali unyeti wa eneo hili.
ANAYETAKIWA KUTOA DAWA KWA MGONJWA NI NANI?
Ninarudia tena, kuna kitu kinaitwa drugs Administration na dispensing. Hapa ndiko hawa wanaojiita wafamasia wanajichanganya huenda ndio matatizo haya .
Hivi mtu anaposema Mfamasia anafanya drugs Administration ana akili sawa sawa? Katika routes zote za drugs Administration ukitoa oral, ni route gani ambayo wafamaia wanafundishwa darasani na kufanya practises?
Wanafundishwa kutoa sindano kwa I.V au I.M? Mimi ninataka nijue pamoja na kua hizi njia huwezi kutolea kwenye pharmacy. Ukweli ni routes zote zinafanywa na madaktari au manesi.
Miaka 6 mtu anahangaika na magonjwa na dawa leo unasema hana uhalali wa kutoa dawa kwa mgonjwa kweli?
Mfamasia anachoweza kufanya ni ni dispensing kwa maelekezo au maagizo ya daktari. Drugs Administration is not Dispensing! Wafamasia muelewe, hii ndiyo ilikua maana yangu. 👇👇
Dispensing includes all of the steps necessary to translate a medication order (prescription) into an individualized medication supply that is both safe and appropriate.
SWALI: Kama wewe ni Mfamasia upo kwenye duka la dawa, amekuja mgonjwa hana cheti cha daktari utatoaje dawa wakati wewe siyo daktari? Ni nani aliyetufundisha kufanya History taking na kutoa Diagnosisi?
Ni Pharmacy ngapi Tanzania zinauzwa dawa kwa maelekezo ya Prescriptions za madaktari?
Unafikiri ni kwanini dawa kali zote zinatakiwa kuuzwa kwa vyeti vya madaktari na wakati huo huo unasema ili daktari huyo huyo auze dawa lazima awe na ADDO? Hii ni akili ya wapi?
Yaaani Daktari huyu huyu ambaye ndiye mwanzilishi na mwasisi wa kozi ya Famasia unasema awe na ADDO ndio afanye Dispensing?
Kwahiyo narudia maelezo yangu pale pale kwamba serikali kuondoa kozi ya ADDO ilifanya vizuri kuondoa ulaji wa kikundi cha watu wachache lakini ni KOSA KUBWA sana kuwaacha wafanasi wauze na kutoa dawa wao wenyewe, ni kosa la kitaalam. Ni lazima awepo na daktari au nesi ambaye ana utaalam wa kubaini magonjwa kama alivyofundishwa.
NI KOSA KUBWA SANA kusema huyu daktari ambaye ndiye mwasisi na mwanzilishi wa kozi ya famasia eti ili auze dawa kwa mgonjwa ni lazima awe na ADDO au si ruhusa yeye kuuza dawa. Ni kosa gani la kiufundi analoweza kufanya daktari ikiwa atatoa dawa aliyoandika yeye bila uwepo wa Mfamasia kama si ukiritimba na ukuaji wa baadhi ya watu kutaka kujipa uhalali na mamlaka ya kumiliki maduka ya madawa na kutaka kufanya kila kitu nje ya uwezo wao?
Hata viwandani kwenye zile karatasi wanazoweka maelezo mwisho hua wanaandika...as directed by Physician, who is physician? Why not Pharmacist?
NI UVIVU MKUBWA WA KUFIKIRI KUA MFAMASIA ANASOMA ILI BAADAYE CHETI CHAKE KITUMIKE KUSIMSMIA PHARMACY.
Wakati wenzetu wanasoma Pharmacy ili kwenda kufanya tafiti na kutengeneza dawa mbalibali viwandani, Tanzania kijana anayesoma Pharmacy anawaza amalize ili cheti chake kikazimamie Pharmacy. Huu ni mfumo mbovu wa elimu na ndio unaozalisha hii migongano inayotokea mara ADDO leo usikie imesitishwa.Yote haya ni kwa sababu ya uvivu wa watu kujishughulisha kutaka akae akunje nne aweke cheti chake dukani alipwe milion moja kwa mwezi maisha yaendelee. Tuendelee kuhamasishwa serikali ilete na ivujitie wawekezaji wa viwanda vya kutengeneza dawa ili kelele na njaa hizi ziishe.
HITIMISHO: Mfamasia atengeneze dawa kiwandani, ahifadhi dawa,atoe na kusambaza dawa. Si kazi yake kuchukua history na kubaini ugonjwa kisha atoe dawa. Atoe dawa kwa maelekezo ya daktari kama taratibu zinavyosema, Pharmacies ziuze dawa kwa vyeti vya madaktari. Awepo daktari au nesi katika Pharmacy yeyote ile ili wasaidie kutoa dawa moja kwa moja kwa wagonjwa, huu ndio wajibu wao. Hakuna tatizo lolote nesi au daktari kuuza dawa maana hakuna hoja ya msingi ya kuzuia hili. Hata mahospitali za Wilaya nyingi tu na vituo vya Afya nchini Tanzania Nurse assistants ndio dispensers na hawana mafunzo ya ADDO.
Prof Patrick Kobono (MD, MMED, MPH, MBA, PhD in Human Anatomy)