Ups and down miaka 8 ya kubet (addiction) bila ya mafanikio

Nashukuru kubet kumenipita kushoto.

Sina mzuka kabisa na kubet

Nachukia kupoteza Hela bila sababu ya msingi.

Niko tayari kupoteza hadi laki5 ila kwasababu ya msingi yenye mashiko.
Kama mimi tuu, yaani nitumie 10 milioni ziliwe kwenye kubeti, nitaumia kwa kipindi kirefu sana...
 
Hii kitu ainuke mtawala aipige pin nchini.

Huu ni ulevi kama tu WA kuangalia pornography au punyeto.

Betting ni laanatul!!
 
Kwa huo upumbavu wako ni lazima wengi waone km michezo ya kubahatisha haifai.
Ndio,kwa watu wenye vichwa vidogo km wewe haifai. Kwani ulishindwa kusubiri kila upewapo mshahara wako utenge ijapo 20K kwa ajili ya betting na ikiisha unasubiri mwezi unaofuata?
 
Vipi tathmini yako betting imekutoa kimaisha au ndio majuto kama mleta uzi? Huko kitaa vijana huwaambii kitu kuhusu kubeti..
Binafsi kamari imekula hela zangu nyingi. Sio chini ya milioni 30.
Ila imenifanya niwe mtafutaji wa pesa.
Hata mjengo ninaomiliki ulitokana na juhudi za kusaka pesa baada ya kuliwa kwenye kamari.
Ninataka niache soon. I can do that
 
Betting ni Uraibu.. Ni Uraibu unaotibika.. Sijui kama hapa kwetu vipo vituo vya kutibu watu wenye Uraibu huu..

Ila mimi nilishindwa.. Kila anayebet unamsikia Dah Man U kanichania mkeka.. Nikajitahidi kuwatafuta wanaoshinda sikuwapata.. Nikajionea ujinga huu bora hela yangu nikavutie bangi..
 
Nafkir tabia ya betting kwa vjana una be caused by lack ya mchongo ktaaa

Kuacha kubet n jambo linaloezekana kbsa haswa kwa kjana kurdhka na kpato cha Kaz unayo fanya ila hata io Kaz ndg ukikosa Kuacha ndo bas tena😢
 
Kweli kabisa unavosema mtoa mada peer pressure kitu kibaya sana vichocheo vya marafiki.. mimi nilikua najua kabisa kamari sio kitu kizuri na nilikua sina shobo kabisa ila mshkaj wa karibu enzi tuko A level alipga hela akanunua Noka N series hizo tambo sasa..

Niliweka 2000 ya kwanza nikaliwa , siku ya pili nikaweka buku nikaliwa ndo ukawa mwisho wangu hadi leo! ila nakiri laiti ningekula ata elf 3 tu ningeendelea sana nashkuru kukosa mwanzoni
 
Dah we Dah pole sana mkamaria! We acha tu mi nimesumbuliwa na huu uraibu kwa takribani miaka kadhaa hv. Nilianza kama kimasihara hivi ..nilibeti 15000 nikala 48000 ...first day! Ndio ilikuwa ufunguzi rasmi. Nikaona hii ndio shortcut ya kutoboa ..aisee nikaja kupoteza pesa nyingi aisee. Kisaikolojia nikawa nimeharibikiwa, kiuchumi na mahusiano yangu kijamii yakawa hayaeleweki. Inafika kipindi unajilaumu sana kuijua kamari ila bado unashindwa kujinasua.

Ila namshukuru sana Mungu...kwasasa nina miezi kadhaa sijishughulishi na masuala ya kamari.

Niliamua kutoka moyoni nikamuomba Mungu kwa dhati aninasue. Nilifuta apps zote za mipira na live score, nikafuta apps zote za kubeti. Kila kampuni ya kubeti nilikuwa na account. Nimezifuta zote.

Na hiyo haitoshi nikafuta vitabu vyote vinavyofundisha mbinu mbalimbali za kubeti. Kifupi sijishughulishi tena na kamari. Na sas hivi naona afya yangu ya akili ikiimarika siku baada ya siku.

Kwani ilifika kipindi silali usiku mzima mimi nabeti mechi za akerica kaskazini n kusini, asubuhi nipo ligi za japan,australia,newzealand...mchana nipo ligi za china,iran,india,kazakhstan..jioni nipo ligi za uturuki,uarabuni, uingereza,ujerumani,n.k ndio ilikuwa cycle yangu.

Nilikuwa mtu wa kujitenga peke yangu tu, kazi kubwa ilikuwa ni kubeti tu.

Sasahivi namshukuru sana Mungu ,im clean from dat demon.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…