Upungufu wa maadili ni ishara kuwa taasisi ya dini imeanguka

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Ukiingia kwenye mitandao ya kijamii utashuhidia lugha chafu zisizo na staha pamoja na matusi mazito ya nguoni.
Hii ni ishara ya kuwa ushawishi wa taasisi zetu za dini kwa jamii umeshuka sana na upo ICU.
Ina maana watoto hawana mafunzo ya chuo(madrasa) au mafundisho na hivyo hawaoni kutenda dhambi kama ni tatizo.
Kwenda kanisani na msikitini imebaki kama fashion tu na hakuna la maana wanalopata au kutoka nalo wanajamii kutoka hizi nyumba za ibada.
Viongozi wa dini wameiangukia siasa na kusahau role yao katika jamii.
Kwa muelekeo huu Familia zina wajibu wa kipekee kuitengeneza jamii wakati huu kuliko wakati mwingine.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Jana ulifikisha target ya kuleta nyuzi uliopewa? Na je huyo anayekupangia score za target amerdhika na matokeo tarajiwa? Maana siku hizi chache umejaza severs za JF Ili kumridhisha bwana Ako anaekueka mjini.

Halafu kuwa mkali hata kiunafki basi hao viongozi wakata vichwa vya watu mnaowasapoti waziwazi huko mitandaoni.
 
Taasisi za dini sio chanzo cha Imani safi,matokeo ya Imani safi ni mahusiano binafsi ya mtu na Mungu, na hofu ya kujitenga na uovu na hofu za Mungu katika maisha ya mtu.

Yakobo 1: 27
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
 
Kwako maadili ni kuungana na watesi wa taifa hili na kudunisha imani?
 
Ukiingia kwenye mitandao ya kijamii utashuhidia lugha chafu zisizo na staha pamoja na matusi mazito ya nguoni.
Hii ni ishara ya kuwa ushawishi wa taasisi zetu za dini kwa jamii umeshuka sana na upo ICU.
Ina maana watoto hawana mafunzo ya chuo(madrasa) au mafundisho na hivyo hawaoni kutenda dhambi kama ni tatizo.
Kwenda kanisani na msikitini imebaki kama fashion tu na hakuna la maana wanalopata au kutoka nalo wanajamii kutoka hizi nyumba za ibada.
Viongozi wa dini wameiangukia siasa na kusahau role yao katika jamii.
Kwa muelekeo huu Familia zina wajibu wa kipekee kuitengeneza jamii wakati huu kuliko wakati mwingine.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Screenshot_20251122-091801~2.png
 
Jana ulifikisha target ya kuleta nyuzi uliopewa? Na je huyo anayekupangia score za target amerdhika na matokeo tarajiwa? Maana siku hizi chache umejaza severs za JF Ili kumridhisha bwana Ako anaekueka mjini.

Halafu kuwa mkali hata kiunafki basi hao viongozi wakata vichwa vya watu mnaowasapoti waziwazi huko mitandaoni.
Umeosoma mada na kuielewa?Mbona unaongelea vitu vilivyo nje ya mada?
Wewe umejigeuza moderator kufuatilia idadi ya threads na posts zangu!!
 
Taasisi za dini sio chanzo cha Imani safi,matokeo ya Imani safi ni mahusiano binafsi ya mtu na Mungu, na hofu ya kujitenga na uovu na hofu za Mungu katika maisha ya mtu.

Yakobo 1: 27
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
umeitendea haki mada hii Mtu wa Mungu
 
Ukiingia kwenye mitandao ya kijamii utashuhidia lugha chafu zisizo na staha pamoja na matusi mazito ya nguoni.
Hii ni ishara ya kuwa ushawishi wa taasisi zetu za dini kwa jamii umeshuka sana na upo ICU.
Ina maana watoto hawana mafunzo ya chuo(madrasa) au mafundisho na hivyo hawaoni kutenda dhambi kama ni tatizo.
Kwenda kanisani na msikitini imebaki kama fashion tu na hakuna la maana wanalopata au kutoka nalo wanajamii kutoka hizi nyumba za ibada.
Viongozi wa dini wameiangukia siasa na kusahau role yao katika jamii.
Kwa muelekeo huu Familia zina wajibu wa kipekee kuitengeneza jamii wakati huu kuliko wakati mwingine.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Watu wa dini wapo bize na siasa,hata maadili Yao wao yamewashinda
 
Maadili hayaanzi ngazi ya dini bali ni mdogo hujifunza kwa mkubwa.

Kuna kitu kinaitwa moral compass , yaani uwezo wa kutambua jambo zuri na baya sasa wote tulipokuwa watoto tulijufunza kipi sawa kipi si sawa hayo ndio maadili.

Unataka vipi vijana wawe na maadili kama wakubwa hawana maadili??

Ufisadi uliokithiri kama walio juu hawaukemei wa chini wakikemea wanatekwa kutakuwepo na maadili?

Maadili hayahusiani na dini wapo watu hawaamini katika dini yoyote ila wana maadili sana sababu ya kupata moral compass.

Mfano wa kutokuwepo na maadili juu ni kama juzi hapa jaji mkuu mstaafu anakubali kuwa sehemu ya tume ya kuchunguza mauaji iliyoundwa na muuaji ambaye kamuweka muuaji mmoja ndani ya tume batili.

Hapa nakupa mfano wa jaji mkuu mstaafu wa Kenya akikemea mauaji na utekaji bila hofu sababu anayo maadili.

View: https://x.com/dkmaraga/status/1934532813639881205?t=kQGPGxF8Vv9C7qh7FVCOcg&s=19

Jaji mkuu mstaafu wa Tanzania lini umemsikia akikemea matukio ya utekaji na mauaji?.. jibu ni hakuna anaogopa kupoteza ulaji wa pesa za ustaafu [anajali tumbo lake] kwa lugha nyingine hivyo hana maadili.

Angekua na maadili angekataa uteuzi batili chini ya rais batili kwenye tume batili badala yake kakubali kwenda kuhalalisha uhuni kwa sababu ya tumbo lake .

Umeelewa jinga lao?
 
Back
Top Bottom