Upungufu wa Saruji: Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aagiza uchunguzi wa kijinai kufanyika

Hoja ya Msingi ni ukosefu & upungufu & Kuongezeka kwa bei ya saruji Nchini na umuhimu wa kufanya uchunguzi wakina ili kubaini tatizo

Suala la Itifaki kwenye uandishi au utoaji maelekezo sio hoja ya Msingi

Hongera Serikali kwa kuchukua hatua stahiki kwa Maslahi ya Umma.
 
Huko ni kuongoza nchi kipumbavu sijawahi kuona. Hatujajifunza matokeo ya ujinga kama huu kweli?
 
Nchi inaongozwa na washamba waliozoea kuswaga ng'ombe na wanadhani kila kitu ni kutumia bakora kama wanavyoswaga wanyama!
 
Hakuna mfanyabiashara au mzalishaji awezeae kufanya hujuma ya kuficha bidhaa na aache pesa. Haya ni mawazo ya wajamaa washindwapo mambo ukimbizia lawama kwa wengine. Ni sawa na kuwalaumu wakoloni dhidi ya kushindwa kwetu kujiletea maendeleo
 
Hakuna mfanyabiashara au mzalishaji awezeae kufanya hujuma ya kuficha bidhaa na aache pesa. Haya ni mawazo ya wajamaa washindwapo mambo ukimbizia lawama kwa wengine. Ni sawa na kuwalaumu wakoloni dhidi ya kushindwa kwetu kujiletea maendeleo
Umri wako na elimu yako tafadhari? Je unaishi Tanzania au upo Alaska? Huwajuhi wafanyabiashara wa Tanzania wewe...nimekuuliza umri maana angalau kwa wale wenzangu na mimi tunakumbuka Opresheni Wahujumu na Walanguzi ya Hayati Sokoine....hujuma kwa wafanyabiashara wa Tanzania ni kama uji na mgonjwa!
 
Wafanyabiashara wa Sasa sio wale wa zamani.
Serikali Ina nguvu ni aibu kukimbizana na wafanyabiashara.Ichukulie Kama uzalishaji ndio ndogo itoke kibali cha kuagiza nje
 
Mkuu unadhani ili la uchunguzi wa kijinai, kwenye Mambo ya biashara,ambapo mlishaji sokoni anategemea malighafi za kuzalisha hicho amezipata kwa gharama gani itasaidia Sana,? Vipo vitu wenda vikawa vidogo na haviitaji tumia nguvu ,why serikali isiitishe kikao na wazalishaji wote wa cement, wenda unaweza kuta kutokana na corona baadhi ya malighafi toka nje zimepanda ,labda na tozo za malighafi hizo hapa nchini zikawa sio rafiki so ukikaa nao zipo changamoto zinawezatatuliwa kwa araka
Ila hii chunguza ,chunguza, utashanga kwa hasira mtu anapewa kesi ya uhujum uchumi na ikitoka hapo jua ataondoka zake na kuacha biashara hiyo hapa tz,
Haya Mambo tuwe makini Sana,tutaumia Sana ,tutakimbiwa na wafanyabiashara wengi tusipokua makini
 
Wafanyabiashara wa Sasa sio wale wa zamani.
Serikali Ina nguvu ni aibu kukimbizana na wafanyabiashara.Ichukulie Kama uzalishaji ndio ndogo itoke kibali cha kuagiza nje
Mkuu unakumbuka uchakachuaji wa mafuta...hadi mafuta ya taa yakapandishwa bei karibia na petroli, majuzi tu hapa! Jana nimenunua kifaa cha milion 1 nimepewa risiti ya sh laki moja naambiwa nikitaka risiti halali malipo yataongezeka!
 
Ni maamuzi sahihi ingawa yamechelewa. Tunayo tume ya ushindani hizi ni miongoni mwa kazi zake lakini wapo kimya kabisa si ajabu wakaibuka baada ya hili tamko.
Cag angeweza kufanya hii kazi vizuri kuliko polisi na pccb kwa sababu ana wataalamu wenye ujuzi sawa na hao waliotumia mbinu za kutengeneza ili bei ipande lakini kuwakomesha serikali ingeruhusu saruji toka nje kama wakati ule saruji ilipotoka Pakistan wenyewe walipunguza bei.
 
Mkuu unakumbuka uchakachuaji wa mafuta...hadi mafuta ya taa yakapandishwa bei karibia na petroli, majuzi tu hapa! Jana nimenunua kifaa cha milion 1 nimepewa risiti ya sh laki moja naambiwa nikitaka risiti halali malipo yataongezeka!
Chukua risiti halali kwa usalama wako hicho kifaa kama ni kibovu kitakula kwako
 
The main reason to cement price hikes is a temporary problem of under production to demand. The cement production facilities are under normal annual maintenance. There is no need for legal intervention. It is a wastage of time. Heri DPP ashughulikie kesi za watu wanaoozea mahabusu bila kufikishwa mahakamani kuliko kupambana na nguvu ya soko la saruji. The market is self-regulating under the law of supply and demand.
 
Ndiyo maana wanafanya Uchunguzi ili kujua uzalishaji na Soko vinaendana!? ua Nani anamuelemea mwenzake! Report itasema hayo yote!!
Nahisi tatizo lipo katika uzalishaji.Viwanda vimepunguza uzalishaji sababu vinajiendeshe kwa hasara.Huenda mali ghafi zimepanda bei
 
Haya mambo ya kutumia vitisho na nguzu badala ya akili ndio yataharibu zaidi mambo. jibu ni control " Demand and supply"
 
Ni malpractice ipi wanayoitegemea kuivumbua kwenye investigation yao?

Anzieni viwandani huko cement inapozalishwa. Principle moja ya biashara ni kubalance supply na demand. Otherwise ni kutafutana uchawi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…