Upungufu wa Saruji: Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aagiza uchunguzi wa kijinai kufanyika

Hahaha wataifishe viwanda vya cement kisha wawapeleke uvcc a.k.a JESHI LA AKIBA wakazalishe cement viwandani.

Mbona bureau de change walitaifisha pesa na kuzifunga, hapa wanashindwa nini ma jemedari wa vita ya kiuchumi.

Huku kuna uhaba wa unga wa ugali, maharage, na mchele, leta uvcc wazalishe.
 
Sisi tuliositisha shughuli za ujenzi tunawaombea wote wanaochukua hatua kwa suala hili la bei kubwa ya bidhaa za ujenzi hasa simenti.
 
Aseme walionunua cement waje na receipt ili waliouza bei zaidi ya bei elekezi chap wakamatwe
 

watafutw sababu za kibiashara badala ya kuingiza siasa na ushabiki kwenye biashara.
 
Huwa tunasema kila siku,mambo yahusuyo uchumi tusiingize siasa.
Kwenye soko huria bei ya bidhaa huamuliwa na forces of demand and supply na hii ni principal,yeyote atakae onekana na hatia atakuwa kaonewa na utakuwa ni muendelezo wa ule tunaouita udikteta unaoendelea kwenye utawala wa awamu ya tano.

Kama wanataka government intervention basi serikali iamue yenyewe pekee ndio iwe msambazaji wa vifaa vya ujenzi.

Ukweli uko wazi kuna uhaba wa vifaa vya ujenzi na sababu ni miradi mingi ya serikali inayoendelea nchini wakati uzalishaji wa saruji na vifaa vingine vya ujenzi kiwango hakijaongezeka.

Kuwekeza tanzania kwa utawala huu ni risk Sana kwani serikali haitabiliki na kwenye hili watu wataogopa kiwekeza nchini.

Tafuteni mamna yakuongeza bidhaa sokoni hilo ndio suluhusho achaneni na ubabe na sifa kwa wapiga kura kama ni uchaguzi mlishashinda kwa hila acheni kuonea wafanyabjashara.

Kipindi cha sakata la kupanda kwa bei ya sukari kunawafanyabiashara wengi Sana walipata hasara na wengine kupata usumbufu wa polisi kwasababu ya ubabe wa serikali lakini mwisho wa siku bei ya sukari iliwashinda.

Ni vema mambo yahusuyo uchumi yakaamuliwa na wachumi sio nguvu ya dola eti kwasababu tu majeshi na polisi yapo chini yenu hii sio sawa.
 
Polisi nao walisema kuwa watapambana hadi saruji ibakie bei yake ya awali![emoji1782]
 
Teach a parrot ‘supply and demand’ and you have an economists.

Sukari sio saruji mmeshaambiwa matumizi ni tonne million 6 inayozalishwa na viwanda vilivyopo kutokana na demand. Halikadhalika at full capacity viwanda ivyo ivyo vinaweza zalisha 10 millioni tonnes kama hiyo demand ipo.

Wazalishaji wanasema order za wateja wao ni zilezile na zinawafikia on time wao wenyewe hawajui tatizo lilipo wanashauri serikali ichunguze kwenye value chain.

Mtu bado tu anakwambia ‘supply and demand’
 
Kanda ya ziwa ina majitu makatili mengi, Jiwe, Jaji Kaijage, Mahera, Mnyeti, DDP, Bashite n.k
 
Bila shaka uchunguzi utabaini mabeberu wanahusika, wimbo tunaoanza kuuzoea masikioni mwetu
 
Mbona na Mafuta ya kula yamepanda sana hawayaoni wamekalia saruji tu, au ni mchezo wa kuigiza.
 
Mkuu,

Mbona protocol iko poa;

1. DPP-Director of Public Prosecution
2. DCI-Director of Criminal Investigation

DPP-Mkurugenzi wa mashitaka hawezi kupeleka kesi mahakamani bila ya kuchunguzwa na kuonekana kosa lilitendeka na ushahidi upo
DCI-Mkurugenzi wa upelelezi hawezi kupeleka kesi mahakamani bila kupitia kwa mkurugenzi wa uendeshaji mashitaka

Baada ya uchunguzi kufanya na ofisi ya DCI faili linapelekwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali, ushahidi ulioambatanishwa kama utakidhi kosa kutendeka na kwamba kuna waathirika kutokana na matendo ya kijinai jarada hurejeshwa kwa wachunguzi wakati mapendekezo ya aina ya kosa la kushitakiwa liwe lipi chini ya kifungu kipi. Baada ya hapo wachunguzi wanapeleka kesi hiyo mahakamani kulingana na kosa ambako ndipo kesi nzima hubebwa na waendesha mashitaka ya umma. Kwa makosa makubwa yaliyoathiri maslahi ya umma, uchunguzi ukishakamilika, mwendesha mashitaka anachukua kijiti kufungua kesi mahakamani moja kwa moja.

Hao watu wanategemeana ila kila mmoja anatambua nafasi yake kwa hiyo alichokiagiza DPP ni sahihi
 
Ageukie na Tanesco pia, nadhani kuna mipango ya hujuma huko!.
 
We mwanafunzi wa certificate ya uchumi umehamia huku?
Unaposema sukari sio saruji unajielewa kweli?Eleza matunda ya nguvu ya dola kwenye bei ya sukari.Haya mambo ukiyajua hayahitaji nguvu ya dola kwani yanakanuni.

Tulipiga Sana kelele enzi za bei ya sukari tukaanza kupewa takwimu kwamba tunasukari yakutosha,sukari inapanda kwakuwa kunawafanyabiashara wameficha sukari ili wapandishe bei wapate faida kubwa,wakaagizwa polisi waingie mtaani kutafuta sukari,hatma yake ndio hii tunaendelea kuumia.

Ukienda tunduma leo wanatumia sukari ya Zambia wananunua 1kg/2000tsh tu wakati maeneo mengine nchini kwetu bei ni zaidi ya 2500.Sasa jiulize wazambia wananunu bei gani?

Tunaendelea kununua sukari bei kubwa kwa sababu wachumi wanaotuamulia mambo yahusuyo uchumi ni vilaza kama wewe.

Wakati raia wanaumia kuna watu wamebaki kutetea ujinga kwasababu wengine ni ama wajinga ama hawajui wanaongea nini.
 
Economy sio somo la kukariri kama unavyodhani unatakiwa uelewe applications kutokana na various factors za situation unayo analyse.

Mahitaji ya sukari Tanzania for human consumption ni tonne 545,000. Uwezo wa ndani wa kuzalisha at full capacity ni tonne 378,450. Kuna deficit ya uzalishaji ambayo lazima iagizwe.

Nyongeza ya hapo factors zingine kama seasonal variation, weather ambazo zinaongeza mahitaji ya muda mfupi au kupunguza uzalishaji kutokana na mazao kuaribika vinaweza disrupt supply kama hakuna risk management plans (ambazo hazipo).

Cement mahitaji ya nchi ni Tonne million 6, viwanda vyote kumi na tatu at full capacity vinauwezo wa kuzalisha tonnes million 10 kwa mwaka. Kwa ivyo bado havifanyi kwa uwezo wake kwa sasa wanazalisha kutokana na demand tu ya million 6.

Kuhusu bei ya sukari kuwa chini Zambia kushinda Tanzania sababu zinaweza kuwa nyingi moja wapo cost of production, level of business investments, government incentives; etc.

Like I told usikariri uchumi, elewa factors kwanza.

The only logical explanation kwenye kupanda kwa saruji kuna baadhi ya viwanda wanadai walipandisha bei June, labda huyo distributor anaenunua huko ana low inventory turn over na anatumia FIFO only now the new price is being reflected. But surely it can’t take that long to shift cement nor the percentage in price hike is justifiable.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…