Upuuzi: Simba wanaenda kurudia kosa lilelile kwa makocha

Yule wa horoya alikuwa amefika nusu fainali kama mbili na last time ndiye alikuwa aje wakachagua pablo instead
Walimchagua Pablo kwa vile aliwaambia amefundisha soka Real Madrid! Nyau hazijielewi!
 
Nyau wampe timu Julio!
 
Simba wanakosea…. kusubiri Makocha Watume applications ni Kama hatujui tunacho kitaka.

Timu kubwa zinavunja mikataba ya makocha, Simba tunatakiwa tuangalie kocha gani tunamtaka halafu tunavunja mkataba wake na sio kusubiri applications.
 
ni sahihi...
na huyu TD ndiye mtu anasimamia falsafa ya soka ya klabu..
miaka nenda rudi timu inaeleweka ni aina gani ya football inacheza, ...mchezaji gani , kocha gani ataendana na style ya soka mnayoitaka. lakini ni mtu kwanza kuhusika ktk ushauri inapohitajika wa namna ya kuajiri mwalimu etc , kuliko hizi kamati.
 
Tungefanikiwa zaidi Kama tungepata Kocha Mwaafrika.
Lakini, tuna viongozi weupe, ni vigumu kutuamini.
 
Tatizo Simba hupenda makocha wa bei rahisi, japo ukimsikiliza Mo akiongea anatuaminisha sana pesa sio tatizo, ndio maana hukimbilia ulaya kuchukua makocha wasiojulikana wa bei rahisi na kuwaacha hawa wa Afrika wenye sifa za kutosha.

Viongozi wa Simba wanatuona tuna akili ndogo sana za kuwapapatikia wazungu.

Bahati mbaya hao wazungu wa bei rahisi wakishapata majina na mafanikio Simba SC hukimbilia timu nyingine kubwa zaidi, mfano yule kishingo aliyekimbilia Morocco. Simba sasa imegeuka timu ya kukuza viwango vya wachezaji na makocha.
 
Tatizo Simba inaongozwa na mwanadada msomi, kila kitu anajua yeye
 
Waafrika ni rahisi kuhongeka ndohof
Hiuo inachangiwa kwa asilimia kubwa na viongozi wa hizi timu. Wapo tayari kumlipa mzungu million 40 ila mwafrika mwezao wanampa million 5🤣🤣🤣🤣

Omeona title winning bonus ya kocha wa wydad? $200,000 kwa kushinda champions league unadhani huyo utamletea vijisnti vya kumuhonga? Tafuta quality coach mlioe vizuri masuala ya kuhongwa hutayasikia
 
Mkuu kishingo si wa kaliba ya chini
Alikuwa kwenye benchi la ufundi
Cameroon ilipo chukua afcon miaka ya karibuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…