Fbn
JF-Expert Member
- Jul 31, 2016
- 15,749
- 37,420
Taswira ya kweli ya wanaume wawili waliopigwa picha kutoka Damascus mwaka 1889:
Mkristo Samir alikuwa mlemavu wa kupooza na pia alikuwa mfupi. Na Mohammed, Mwislamu kipofu aliyekuwa akimbeba Samir mgongoni.
Samir aliyekuwa mlemavu wa kupooza alimtegemea Mohammed katika safari zake mitaani mjini Damascus. Naye Mohammed, kwa kuwa alikuwa kipofu, alimtegemea Samir kumwongoza njiani na kumwonya kuhusu mashimo na vikwazo.
Mmoja aliona na mwingine alitembea. Walikamilishana na kupambana kwa pamoja na ukatili wa maisha. Walikuwa mayatima, wapweke bila mama wala baba. Rehema ya Mungu ikawajumuisha pamoja.
Wakaamua kuishi pamoja chumba kimoja, na kufanya kazi sehemu moja. Samir alikuwa mwandishi na msimulizi wa hadithi, akifanya kazi katika moja ya vijiwe vya kahawa katika mji wa kale wa Damascus. Naye Mohammed alikuwa akiuza njegere mbichi mbele ya kahawa hiyo hiyo, akisikiliza hadithi za Samir.
Samir alipofariki, Mohammed alibaki akilia bila kukoma kwa wiki nzima. Kisha akapatikana amekufa pia—akiwa amekufa kwa huzuni ya kumpoteza nusu yake nyingine.