Ulichoandika ndicho niliwaza ninaapa mbele yake devil, nilipoona tu ni Feitoto anaenda kupiga nikajua penati itapigwa juu angani ikatue kwao mkunazini au itapigwa nje na ndo ilivyokuwa. Yani kamuonesha kabisa Ayoub kuwa anapiga kushoto kipa akaenda huko huko hata kama mpira usingegonga nguzo angeudaka!
Azam waliocheza leo sio wale wa Mwanza, yaani mpira ulipoanza Azam walionesha wazi kuizidi Simba uwezo ila muda ulivyoenda wakajiangusha wakajilegeza wakawa mdebwedo, wanacheza kama wamelazimishwa, hadi ikaboa, Manyama, Sopu, Amoah na Mwaikenda watu wa kazi wakawekwa nje nikajua tayari matokeo yamepangwa!!
Azam mmeboa sana Leo yaani mnaiachia mbumbumbu FC nafasi yenu na mjue hawatatoboa hata makundi tu timu mbovu mbovu tu Mamelodi walitupoka uto ushindi wakapigwa nje ndani.
Kweli nimeamini soka la bongo linachezwa nje ya uwanja, yaani Putin hakukabwa aliachwa tu apige shuti afunge, kweli TFF makolo watupu, leo ligi imeharibika hakuna tena sijui mzizima derby my foot!! simba hii mbovu haina msuli wa kuibamiza Azam 3 - 0 ambayo gari limewaka!
Sidhani kama wanangu wataendelea kushabikia Azam lamba lamba tena baada ya kichapo cha mchongo cha Leo.
But anyway potelea mbali maisha mafupi raha jipe mwenyewe, bado point 4 tu Yanga bingwa inatosha!!