Urafiki wa Azam na Simba unaua soka letu

Hijakutana na Azam wakicheza na Yanga wewe
 
Unazungumzia urafiki wa Simba na Azam vipi Ile timu yenye urafiki na Wauwaji wa kusini, wajera jera, waja leo waondoka leo,kuna timu imenunuliwa toka mbeya kuja Singida, Ile iliyotolewa Singida kwenda mwanza na timu ya pale katikati ya nchi kuna mshambuliaji wao wazamani alihojiwa kabla mahojiano hayajafutwa alisema walikuwa wanaenda uwajanja ila wanajua kabisa matokeo yatakuwaje.
 
Nataka ukatae kama Azam sio tawi la Simba
 
Nataka ukatae kama Azam sio tawi la
 
acha kelele wewe, mpira mchezo wa wazi
 
Kwa mawazo kama haya utegemee eti kwamba tutaendelea, haiwezekani kamwe.
 
Ukimaliza utueleze na kuhusu urafiki wa Singida na Yanga

Ukimaliza pia utueleze kuhusu ufhamini wa GSM kwenye timu za Ligi kuu
 
Simba iko nafas ya 3, ila kama nyie mnaumia simba kua nafas ya 3...sjui hii tunaiitaje ..
 
Haya mwiko nyuma
 
Hata kama ni ushabiki ila tuwe wakweli

Azam leo mechi alikuwa anaihitaji ila hakuwa na uwezo

Hata refa alikuwa upande wao inaonekana alikula mlungula

Mtani leo kacheza kawaida tu ila matokeo yamekuwa upande wake


Sometimes hizi mechi zinaendeshwa na ushirikina zaidi
 
Ulichoandika ndicho niliwaza ninaapa mbele yake devil, nilipoona tu ni Feitoto anaenda kupiga nikajua penati itapigwa juu angani ikatue kwao mkunazini au itapigwa nje na ndo ilivyokuwa. Yani kamuonesha kabisa Ayoub kuwa anapiga kushoto kipa akaenda huko huko hata kama mpira usingegonga nguzo angeudaka!

Azam waliocheza leo sio wale wa Mwanza, yaani mpira ulipoanza Azam walionesha wazi kuizidi Simba uwezo ila muda ulivyoenda wakajiangusha wakajilegeza wakawa mdebwedo, wanacheza kama wamelazimishwa, hadi ikaboa, Manyama, Sopu, Amoah na Mwaikenda watu wa kazi wakawekwa nje nikajua tayari matokeo yamepangwa!!

Azam mmeboa sana Leo yaani mnaiachia mbumbumbu FC nafasi yenu na mjue hawatatoboa hata makundi tu timu mbovu mbovu tu Mamelodi walitupoka uto ushindi wakapigwa nje ndani.

Kweli nimeamini soka la bongo linachezwa nje ya uwanja, yaani Putin hakukabwa aliachwa tu apige shuti afunge, kweli TFF makolo watupu, leo ligi imeharibika hakuna tena sijui mzizima derby my foot!! simba hii mbovu haina msuli wa kuibamiza Azam 3 - 0 ambayo gari limewaka!

Sidhani kama wanangu wataendelea kushabikia Azam lamba lamba tena baada ya kichapo cha mchongo cha Leo.

But anyway potelea mbali maisha mafupi raha jipe mwenyewe, bado point 4 tu Yanga bingwa inatosha!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…