Uraia pacha na Tanzania

kwa tanzania urai pacha ni lazima tufikirie mara mia moja ili kutoa uamuzi mara moja tusipende kuiga kila kitu kwa nchi
 

Acha wendawazimu kijana hujui kuwa Dunia inaongozwa na Waisrael kwa mwamvuli wa USA na Russia? Unaijua siasa ya uraia pacha? kama unataka kwenda huko we nenda kawe raia hukatazwi watanzania wa kawaida hata passport hawana wewe unawashawishi uraia pacha utawasaidia nini!
 
BILA shaka wengi tunakumbuka kwa uchungu kabisa jinsi tulivyoshuhudia viwanda vilivyotengenezwa kwa mikopo ambayo ni sehemu ya deni la Taifa, vilivyouzwa kwa bei ya 'kutupa' kwa wanaoitwa 'wawekezaji'.

Wengi wa 'wawekezaji' hawa walichofanya ni kugeuza viwanda vile kuwa maghala na kuuza majumba na mtandao wa rasilimali ambazo zilikuwa chini ya viwanda; na kwa kuwa hawakuwa na nia hasa ya kuzalisha wengi waliuza mitambo au waliitelekeza kwa walinzi ambao hawakuwa na mwajiri wa moja kwa moja, kufanya walinzi wale waendelee kujilipa 'mishahara' kwa kuuza mitambo ile ya gharama katika vipande vidogo vidogo kama vyuma chakavu.

Matokeo ya ubinafshaji katika maisha ya wanachi yalishuhudiwa kwa katika eneo la ukosefu wa ajira, ajira isiyo na uhakika na kutokuwa na hakika ya maisha ya kila siku na kupanda kwa gharama zisizoepukika za maisha. Hiki ndicho kipindi ambacho nchi yetu ilishuhudia kina 'Ngapulila' wengi ambao kwenda nje kutafuta maisha ndio lilikuwa suluhisho pekee la matatizo yao ya kiuchumi waliyokuwa wakipambana nayo, ambayo kwa bahati mbaya na kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yao walijikuta hawakuwa na mtu wa kuwasemea. Ikumbukwe, msingi mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Azimio la Arusha ilikuwa ni kuwasemea wanyonge, 'kubatilishwa' kwa Azimio la Arusha kule Zanzibar na kuachia nguvu ya 'mitaji' kutamalaki, kulidhoofisha sana misingi ya utu na imani ya watu kwa serikali yao.

Walioondoka wakati ule wengi wao walikuwa 'waathirika' wa mabadiliko yale yaliyoruhusu ubinafsishaji katika sekta zote muhimu, na ndiyo hawa tunawazungumzia leo kama 'diaspora'. Kati ya masuala yanayozungumzwa sana ni kuruhusu uraia-pacha. Naamini na nimepata kusikia mara kwa mara viongozi wetu waandamizi wakitoa kauli za kukubaliana na suala hili la kuruhusu uraia-pacha wakitumia sababu zile zile walizotumia kwenye ubinafsishaji wa viwanda; sababu kuu inayotumika sasa katika kutaka kuhalalisha 'uraia-pacha' eti ni kuvutia mitaji, kuongeza ajira na kuongeza pato la serikali kupitia kodi. Imekuwa ni mazoea kwetu kuenenda kwa matukio. Kufanya maamuzi makubwa na yenye athari kubwa kwa spidi ya 'kufa mtu'.

Kwa sababu hii, mara kwa mara tumejikuta tukifanya makosa, na kwa kuwa tu wazito kutambua makosa yetu, mara kwa mara tumejikuta tukirudia makosa yale yale, kwa kuwa hatujifunzi. Safari hii pia, suala la uraia-pacha 'tumeshauriwa' na sasa utekelezaji wake ni moja ya mambo yanayoenda kwa kasi kubwa, kwa hulka yetu si jambo la kustaajabisha. La kustaajabisha hapa ni jinsi gani suala hili linavyopelekwa-pelekwa, ni suala linalostaajabisha kwa kila mtu anayetaka kujisumbua kujifikirisha.

Kwa kuwa nchi yetu imejaa 'wawekezaji' kutoka kila taifa, bila shaka wengi wangetamani kuitumia fursa hii; swali ni kwa kiasi gani uraia huu pacha utaendelea kuwafaidisha wengine (Wazungu, Wachina na wahamiaji wengine) na si Watanzania ni swali linalohitaji mjadala, lakini dalili za mvua ni mawingu. Kuna kila dalili, suala hili linashabihiana kama ilivyo kwa wawekezaji wakati tunawafungulia milango, Watanzania waliaminishwa 'uwekezaji' ni kwa faida ya Watanzania, kwa kuwa umasikini wetu umetokana na kutokuwa na mitaji.

Kilichotokea kila mtu anafahamu, Watanzania waligeuka manamba kwenye nchi yao, na kwa kuwa tumecheza na hatima yetu katika maeneo nyeti tumebaki watazamaji pale raia wa nje wanapokuja kuchukua fursa za kazi, biashara na uwekezaji. Kama ilivyo katika uwekezaji, uraia wa nchi pacha hauna hakika kama utamnufaisha Mtanzania aliyepo Tanzania au yule aliye ughaibuni. Hata kama wenzetu wamefaidika nao, mazingira ya Tanzania ni tofauti na wenzetu, na hata sababu za Watanzania kuondoka na kuishia ughaibuni hazishabihiani kihivyo na wengine.

Hivyo basi utafiti ni muhimu kufanyanyika kabla ya maamuzi. Bila utafiti haiyumkini uamuzi huu ukawa na athari za muda mrefu; hata kama utawafaidisha Watanzania wasiozidi milioni tatu wanaoishi nje, ukawa janga kwa Watanzania zaidi ya milioni 42 wanaoishi Tanzania, na kwa hakika fursa chache zilizopo na zilizotengwa kwa ajili ya Watanzania zikapotea hasa kwa kuwa kuna kila dalili kuwa 'wawekezaji' walio nyumbani ndio watakaochangamkia zaidi 'fursa' hii. Haishangazi basi, suala hili la uraia pacha linachagizwa na serikali za nje kama Canada na Oman (ndizo zilizotajwa) na kuingizwa kwenye ajenda kama mahitaji muhimu ya Watanzania wanaoishi nje. Swali la kujiuliza hapa kwa nini Canada na Oman ndizo vipaumbele na si Afrika Kusini, au Ulaya?

Sipendi kuhisi, lakini isije ikawa huu ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu kuwarudisha wale waliokimbia Azimio la Arusha na Mapinduzi ya Zanzibar kwa mlango wa nyuma, hasa kwa kuwa mpango huu unawezeshwa na serikali hizo (rejea Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje Uk. 43-44) Mheshimiwa Spika, ...katika mwaka huuwa fedha, Wizara yangu imechukua jitihada zamakusudi za kupanua wigo kwa kuwafikia Diaspora waishio Canada na Oman. Mikutano na Watanzania hao iliandaliwa sanjari na ziara za Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika nchi hizo mwezi Oktoba 2012.

Nchi hizi mbili, kwanza zina Watanzania wengi walio jizatiti kiuchumi, kijamii na hata kisiasa. Lakini pili, Serikali za nchi hizo zinaunga mkono jitahada zetu na zipo tayari si tu kuwawezesha ila kushirikiana na Diaspora hao kuchangia maendeleo ya nchi yetu. Kama ilivyo gesi na madini, suala la sera lilikuwa ni muhimu sana katika mjadala na kwa kiasi kikubwa watu walijiuliza; "hii kasi yote ni ya nini?" Kama ilivyo muhimu kuwa na sera ya madini kabla kuuzwa kwa vitalu, vivyo hivyo kuna umuhimu wa kuwa na sera ya "Watanzania wanaoishi nje" kabla hatujaruhusu kinachoitwa "uraia-pacha". Ni muhimu sana kuwa na sera ambayo Watanzania wanaoishi nje na wadau wa nyumbani wakashiriki kuitengeneza.

Mchakato wa kuitengeneza sera hii haiyumkini utatoa nafasi kwa serikali kuwafahamu hao "diaspora" ni kina nani, wanafanya nini, wako wapi, na maeneo gani ya kimkakati tunahitaji kushirikiana nao katika kuiendeleza nchi yetu. Matokeo ya kitaalamu na kitafiti yanaweza kutoa mwelekeo mzuri katika kuangalia njia bora zaidi ambayo serikali inaweza kuitumia kuwaleta karibu Watanzania (pengine bila hata ya kulazimika kuwa na uraia-pacha). Ifahamike kuwa ni nchi chache sana ambazo zinatoa uraia-pacha usio na masharti tena kwa sababu za kimkakati. Nchi nyingi zinatumia njia mbalimbali na tofauti kuwafanya wananchi kuwa sehemu ya nchi wanazotoka na kuwafanya wawajibike katika kushiri katika juhudi za maendeleo.

Mexico wana mpango unaitwa 'Tres Por Uno (3x1)' ambao unamuwezesha kila diaspora anayetuma pesa moja nyumbani kuwekeza, serikali inamuongea 3; mpango huu ni bora na nafuu zaidi kuvutia uwekezaji kuliko ule wa kusamehe kodi 'wawekezaji'; njia nyingine ya kuvutia diaspora ni pamoja na kutambuliwa na kuchukuliwa kama raia ikiwemo kupewa hadhi maalumu ya ukazi ambao hauna masharti kwa mwananchi yeyote anayeamua kurudi kufanya kazi au kuwekeza (Ethiopia wana utarativu wa yellow card) Pamoja na hayo, serikali inaweza kutathmini changamoto wanazokumbana nazo Watanzania nje na kuangalia ni jinsi gani na kwa kiasi gani serikali inaweza kubeba baadhi ya changamoto ambazo zipo nje ya uwezo wa diaspora wenyewe, kurahisisha maisha yao na kushiriki kwa karibu katika ujenzi wa Taifa, changamoto hizi ni kama gharama ya usafirishaji pesa nyumbani (ambazo ni kubwa ukilinganisha na nchi nyingine za jumuiya ya Afrika Mashariki), haki za Watanzania wanaoishi nje, na hata kubadilishana kodi na nchi nyingine (kama nchi zinavyobadilishana wafungwa).

Ingawa tumebinafsisha vingi, bado hatujachelewa, kuna vingine hatupaswi kuvibinafsisha, uraia ni suala mojawapo.
 

Tanzania mpaka mwanzoni mwa miaka ya 90 passport zilikuwa zinatolewa kama almasi kwa ugumu sawa na kung'oa jino bila ganzi.

Waliopo nje ya nchi wanaohitaji uraia pacha ni watoto wa masikini waTanzania walioenda nje kutafuta riziki, uwezo wao mpaka sasa ni kusaidia ndugu zao direct help chakula, malazi na vijiada vidogo. Mzunguko wao unakuwa kwani kila mwaka wanaongezeka. Misaada yao inaongezeka pato la taifa kwa kutuma fedha kwa ndugu zao, hupunguza trade deficit kubwa tuliyonayo.

Number ya wahamiaji kutokwa TZ kwenda nje kutafuta ajira inaongeza kwa kasi. Leo tuna vyuo vikuu zaidi ya 40 vinazalisha wastani wa wahitimu zaidi ya 10000 kila msimu. Hakuna ajira, wataondoka kwenda sehemu nyingi za dunia kutafuta ajira. Wataznania wazawa ni wazalendo kupindukia asilimia 95 hukumbuka nyumbani, kwa kujenga nyumba, kusaidia ndungu na kuanzisha vimiradi vidogo vidogo.

Kizazi cha wataznania wa nje kitakuwa na elimu nzuri, ajira safi na utaalamu mkubwa tutakihitaji sana kuliko sasa.

Uraia pacha ni uzalendo wa kulinda haki yako ya kuzaliwa. Ni muhimu na nihitaji la masikini. More doors and more opportunities.
 
Mkuu wenzeio tumeshachukua uraia wa Kenya. Hivyo naingia bongo bila bughudha wala viza. Nikiwa ndani ya Tanzania natumia passport yangu ya bongo kwa shughuli zangu za bongo na utambulisho kama mtanzania. Nikitoka nje narudi zangu Kenya kwa mkwaju wa kikenya,
Nikienda EU ama US natumia mkwaju wangu wa kimarekani. Passpoerts 3 zinanitosha na nashangaa wanaopiga kelele za uraia pacha, wa nini na wakati tayari ninao?
Uki overstay bongo, uwe na pesa zako tu manake jamaa wa uhamiaji pale airport ukiwakatia $100 wanakurekebishia kila kitu
 

Acha kutudanganya kijana hao walioondoka Tanzania kama wanataka kuja kuwekeza waje tu mbona wazungu na waasia wanakuja na sio raia? Usipendw kupigia debe vitu ambavyo wananchi maskini waviwasaidii. URAIA pacha utakunifaisha wewe na wenzio ambao mnataka kuhujumu nchi mkimbie huku mkiwa mmeshahamishia pesa huko mnakoenda.
 
kwa mtu ambaye hajaishi nje ya tanzania hawezi kujua hata siku moja kwa nini mtu anataka uraia wa nchi mbili.. n by nje simaanishi kenya wala uganda, toka nje ya africa kabisa.... tanzania wanadhani wajanja kubania uraia wa nchi mbili ila wanaumiza raia wao tu, wote walio nje wakirudi wajirundike wapigwe doro bongo sijui serikali italisha kila mtu, kama uhamiaji nafasi za kazi watu wamejitokeza uwanja wa mpira kuwania nafasi 70 peke yake. mtu aliye nje na ana ajira na hela ya kuishi na kuwasaidia nyumbani unamuona chizi unambania uraia, huu ujinga wa tanzania hua unanifanya nifikirie mara mbili kuacha uraia yani bac tu sema moyo unasema wavumilie wajinga
 
Kapalamsenge hivi hujui kuna watu wamehamisha hela nyingi tu kutoka Tanzania hata kabla ya hiki kipindi tunapodai uraia wa nchi mbili na watu hao ni watanzania na bado wapo Tanzania na nina uhakika unawajua au unewahi kusikia. Sasa hebu nambie nini kitabadilika then kama uraia pacha utakuwepo? Au ndo wivu tu na roho ya kwa nini?
 
Kuwa fisadi haijalishi lakini ukiweka huo uraia pacha utafanya wizi uwe mkubwa zaidi, nishasema kama ni suala la kuwekeza walete wawekeze haiitaji uwe na uraia pacha ndo uje uwekeze Tanzania.

 
Ndugu zanguni,

Kumekuwa na kelele nyiiingi za kipuuzi na za maana juu ya suala la uraia pacha , lakinbi hakuna aliekuja na solution nini kifanyike

Mimi binafsi napendekeza serikali iweke masharti ambayo yatamfanya mtu anaetaka uraia pacha achangie uchumi wa nchi yetu kwa kulipa kiwango kikubwa cha fedha sawa tu na serikali nyinginer kama za Uingereza zinavyofanya

Kwa mfano, kuomba uraia uingereza lazima ulipe £906 na kama una familia kubwa basi ndio imekula kwako, sawa na shs mil 2.5 kwa kichwa, hii itapunguza kelele za wale wanaosema diaspora hawachangii kwa taifa, mimi nitachangia zaidi ya 20 milions , wewe umechangia nini zaidi ya maandamano?

Hivyo basi, ili kupunguza kelele za mbulumundu na wanaojua nini tunaomba, napendekeza serikali itoze kila mtu anaetaka uraia pacha alipe milioni mbili unusu na awe ametimiza masharti yafuatayo

1. WAZAZI WAKE WAWE WATANZANIA
2. AWE KAZALIWA TANZANIA NA MMOJA WA WAZAZI WAKE LAZIMA AWE MTANZANIA
3. KAMA HANA CHETI CHA KUZALIWA BASI AKAONYESHE MAKABURI YA BABU ZAKE NA AZIJUE MIOLA ZAKE
4. KAMA KWELI NI MTANZANIA, UKIMUULIZA MASWALI KWA KISWAHILI JUU YA TANZANIA LAZIMA APATIE (kwa mfano tu, ATAJE MAJINA YA WATEMI WATATU MAARUFU NK)

4. LAFUDHI IWE YETU, (huwezi sikia mtanzania akakuambia .." mimi ni mubhongo..."

Zaidi ya hapo nadhani hakuna jipya...
 
Mkuu Chilisosi kwanza kabisa kwa hali ya hewa inavyooneka huko nyumbani dual citizenship is inevitable its a matter of time.

Ulikua unachangia vizuri tu ila umekuja kuaribu pale uliposema kua eti ''unachangia sh ngapi zaidi ya maandamano'' sidhani kama kuna mtu anaandamana kwa kufuata mkumbo bali raia wanaandamana kwa kuchoshwa na dhuluma na uonevu wanaofanyiwa na serikali hii ya kijani so you have to note that.
 
Last edited by a moderator:
Huwa mnaandamana ili iweje?

Mbona siku hizi kimya??
 
hiyo namba 2. imekaa vibaya. je
aliyezaliwa nje ya tanzania na wazazi/mzazi
watanzania inakuwaje?

halafu hayo maswali inabidi yawe yanaweza
kujibiwa na mtanzania yeyote liyepo tanzania.
 
Nafikiri hapa kuwe na sheria ambayo inatambua asili wa Watz walio nje ya nchi na kuwapa haki sawa na watz wengine.Ila kuwa na raia pacha tutapoteza Mali zote kwa wajanja wachache watakaotumia uraia pacha.
 
Mimi watoe wasipotoa sijali..naishi nchi ya watu kisheria..napiga kazi..nkitaka kurudi ntarudi kwa kufuata taratibu..sitegemei mbeleko yoyote toka tanzani..sitegemei siasa kuishi..watoe wasipotoa..watajua..huwezi kukaa unabishana na mijitu ya ccm ambapo..kila kitu kipo wazi
 
Reactions: BAK
No tuache siasa katika hili suala mkuu bali tujadili uharakishaji wa kupatikana muafaka wa dual citizenship sisi tumewahi kwenda hadi ubalozini tukaambiwa mambo yatakua mazuri ila tuwape muda. Swali ni kuwa mpaka lini ?
Huwa mnaandamana ili iweje?

Mbona siku hizi kimya??
 
MIMI SIELEWI DUNIA SASA NI KIJIJI
MOVEMENT OF ASSETS TO WHERE PROFIT IS REALIZE AT MAXIMUM
FURSA HIZI...JAMANI...KENYA HII
Diaspora Remittances contribute $3bln to Kenyan Economy
(Stock Markets, Business News, Earnings, Africa - CNBC Africa) Stanbic Investment Management Services released a report indicating that diaspora remittances have contributed more than $3 billion to the Kenyan economy in the last 5 years. For a closer look at these numbers ABN's Lerato Mbele is joined in our Nairobi studio, by Anthony Mwithiga, Chief Investment Officer at Stanbic Investments.
 
katika suala hili tuzibe maskio kuwasikiliza opurtunists kama huyo leticia. eti kamuacha nyerere lakini jina hataki kuacha. hivi kweli tunahitaji raia wa amerika wenye uraia wa tanzania? watu wanaosema wamekua wamarekani kwa ajili ya kupata fedha si wanaweza kutuuza kwa fedha wakiwa viongozi wa nchi yetu! hao walowezi ughaibuni wanachotaka kwetu hasa ni nini. kwani kuna mtu kawakataza kuwekeza na kusaidia jamaa zao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…