mansoorsaid
JF-Expert Member
- May 31, 2014
- 1,498
- 286
kwa tanzania urai pacha ni lazima tufikirie mara mia moja ili kutoa uamuzi mara moja tusipende kuiga kila kitu kwa nchi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wasiwasi wengi walionao si kweli kabisa, Nchi ya wayahudi Israel imejengwa na inanguvu kubwa duniani kwasababu ya wayahudi zaidi ya 7m waliosambaa duniani.
Nchi ya Singapore imeimarishwa uchumi na diaspora, Nchi ya Ethiopia imefaidika sana na diaspora kiuchumi, Nchi ya Ghana, nk nk. Si kweli kwamba watanzania waliolazimika kufanya kazi nje ya Tanzania sio wazelando, na si kweli kwamba hawasaidii Tanzania msaada wao ni mkubwa kuliko bajeti ya wizara mbili za serikali.
Miaka kumi au ishirini baadaye kutakuw na zaidi ya watanzania 10m duniani wenye biashara, ajira nzuri, elimu, utaalamu nk. Vile viloe kutakuwa na watanzania zaidi ya 4M waliostaafu nje wenye malipo mazuri ya uzeeni wangependa kuja na kuishi nyumbani na kutumia hizi fedha ambazo zitatengeneza ajira zaidi ya 5M.
Ukiangalia leo na sasa na matukio ya kiuchumi mabovu, utawala mbovu, sheria gandamizi na za upendeleo, wizi wa kukimbia nchi na kukimbiza fedha utahisi hakuna faida. Wezi unaowaogopa wewe hawahitaji uraia pacha , wana fedha za kununua uraia popote duniani. Nchi ya marekani ukiwa na zaidi ya $500,000 unapewa ukazi, mwizi wa bot au mhujumu anaweza kuishi popote bila kuhitaji uraia pacha kwani hahitaji ajira ana fedha.
Wazalendo masikini ndio wanahangaika. Hakuna tajiri mwenye haja ya kuishi nchi masikini kama zetu wala kuwekeza kwa kudumu.
Wengi wazawa wa kweli wanapenda nchi zao.
Acha wendawazimu kijana hujui kuwa Dunia inaongozwa na Waisrael kwa mwamvuli wa USA na Russia? Unaijua siasa ya uraia pacha? kama unataka kwenda huko we nenda kawe raia hukatazwi watanzania wa kawaida hata passport hawana wewe unawashawishi uraia pacha utawasaidia nini!
Mkuu wenzeio tumeshachukua uraia wa Kenya. Hivyo naingia bongo bila bughudha wala viza. Nikiwa ndani ya Tanzania natumia passport yangu ya bongo kwa shughuli zangu za bongo na utambulisho kama mtanzania. Nikitoka nje narudi zangu Kenya kwa mkwaju wa kikenya,Kwasababu Tanzania inasuasua na sheria ya uraia pacha wakati nchi wanachama Kenya, Uganda na Rwanda zikiwa tayari zinatambua Uraia pacha na wananchi wake walio nje ya nchi zao kufurahia, na Kwasababu Tanzania ni mshiriki wa east african community huku ikitambua east african citizenship na passport, Watanzania ambao wanapata ugumu na Tanzania kwasababu wamepata uraia wa nchi zingine ni vyema wakafikiria kuchukua Uraia wa Kenya, Uganda au Rwanda na wataendelea kuishi na kujiendeleza kwenye nchi yeyote ya jumuiya ya afrika mashariki bila bugudha na kukwepa adha ya siasa za nyumbani ambapo Mtanzania huyu ataishi Tanzania kama raia ama wa Kenya, Rwanda, au Uganda huku akiwa amelinda uraia wa nchi nyingine unampa kula na ajira.
Tanzania mpaka mwanzoni mwa miaka ya 90 passport zilikuwa zinatolewa kama almasi kwa ugumu sawa na kung'oa jino bila ganzi.
Waliopo nje ya nchi wanaohitaji uraia pacha ni watoto wa masikini waTanzania walioenda nje kutafuta riziki, uwezo wao mpaka sasa ni kusaidia ndugu zao direct help chakula, malazi na vijiada vidogo. Mzunguko wao unakuwa kwani kila mwaka wanaongezeka. Misaada yao inaongezeka pato la taifa kwa kutuma fedha kwa ndugu zao, hupunguza trade deficit kubwa tuliyonayo.
Number ya wahamiaji kutokwa TZ kwenda nje kutafuta ajira inaongeza kwa kasi. Leo tuna vyuo vikuu zaidi ya 40 vinazalisha wastani wa wahitimu zaidi ya 10000 kila msimu. Hakuna ajira, wataondoka kwenda sehemu nyingi za dunia kutafuta ajira. Wataznania wazawa ni wazalendo kupindukia asilimia 95 hukumbuka nyumbani, kwa kujenga nyumba, kusaidia ndungu na kuanzisha vimiradi vidogo vidogo.
Kizazi cha wataznania wa nje kitakuwa na elimu nzuri, ajira safi na utaalamu mkubwa tutakihitaji sana kuliko sasa.
Uraia pacha ni uzalendo wa kulinda haki yako ya kuzaliwa. Ni muhimu na nihitaji la masikini. More doors and more opportunities.
Kapalamsenge hivi hujui kuna watu wamehamisha hela nyingi tu kutoka Tanzania hata kabla ya hiki kipindi tunapodai uraia wa nchi mbili na watu hao ni watanzania na bado wapo Tanzania na nina uhakika unawajua au unewahi kusikia. Sasa hebu nambie nini kitabadilika then kama uraia pacha utakuwepo? Au ndo wivu tu na roho ya kwa nini?Acha kutudanganya kijana hao walioondoka Tanzania kama wanataka kuja kuwekeza waje tu mbona wazungu na waasia wanakuja na sio raia? Usipendw kupigia debe vitu ambavyo wananchi maskini waviwasaidii. URAIA pacha utakunifaisha wewe na wenzio ambao mnataka kuhujumu nchi mkimbie huku mkiwa mmeshahamishia pesa huko mnakoenda.
Kapalamsenge hivi hujui kuna watu wamehamisha hela nyingi tu kutoka Tanzania hata kabla ya hiki kipindi tunapodai uraia wa nchi mbili na watu hao ni watanzania na bado wapo Tanzania na nina uhakika unawajua au unewahi kusikia. Sasa hebu nambie nini kitabadilika then kama uraia pacha utakuwepo? Au ndo wivu tu na roho ya kwa nini?
Huwa mnaandamana ili iweje?Mkuu Chilisosi kwanza kabisa kwa hali ya hewa inavyooneka huko nyumbani dual citizenship is inevitable its a matter of time.
Ulikua unachangia vizuri tu ila umekuja kuaribu pale uliposema kua eti ''unachangia sh ngapi zaidi ya maandamano'' sidhani kama kuna mtu anaandamana kwa kufuata mkumbo bali raia wanaandamana kwa kuchoshwa na dhuluma na uonevu wanaofanyiwa na serikali hii ya kijani so you have to note that.
Huwa mnaandamana ili iweje?
Mbona siku hizi kimya??
katika suala hili tuzibe maskio kuwasikiliza opurtunists kama huyo leticia. eti kamuacha nyerere lakini jina hataki kuacha. hivi kweli tunahitaji raia wa amerika wenye uraia wa tanzania? watu wanaosema wamekua wamarekani kwa ajili ya kupata fedha si wanaweza kutuuza kwa fedha wakiwa viongozi wa nchi yetu! hao walowezi ughaibuni wanachotaka kwetu hasa ni nini. kwani kuna mtu kawakataza kuwekeza na kusaidia jamaa zao?Suala la uraia pacha, limejitokeza tena kuwa hoja nzito katika mkutano wa tatu wa uratibu wa wadau Watanzania wanaoishi ughaibuni (diaspora), huku baadhi wakiitaka serikali kuharakisha mchakato wa kuanzisha utaratibu huo. Walisema Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanapata adha kubwa na wengine wanashindwa kuwekeza, kurudi au hata kusaidia familia zao kile walichochuma kwa sababu tofauti zikiwemo za usumbufu na kupanda kwa gharama.
Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere, (Chadema), alisema suala la uraia pacha ni muhimu na kwa sasa halikwepeki. Aliitaka serikali kuharakisha utaratibu wa huo ili kuwapunguzia adha Watanzania wanaoishi nje ya nchi na ambao hawataki kuukana uraia wao.
Kuwa na uraia pacha ni muhimu, wapo Watanzania waliokwenda Marekani kwa sababu tu ya ukimbizi wa kiuchumi na wakapata watoto huko, lakini watoto wao wanakuwa ni Wamarekani, kama kungekuwa na uraia pacha, hao wangeweza kuwa raia wa Tanzania na Marekani kwa wakati mmoja, alisema.Pia alisema Mtanzania aliyezaliwa Marekani akiwa na uraia pacha hataweza kuhatarisha vitegauchumi vyake iwapo atapenda kuwekeza nchini au hata huko Marekani. Watu wetu wa diaspora wanafanya mambo mengi na makubwa katika kuchangia uchumi wa taifa letu, lakini kwa kuwa misaada yao haijaorodheshwa na hakuna takwimu, michango yao haijulikani, alisema na kuongeza: Naiomba serikali kulitafutia ufumbuzi suala la uraia pacha mapema.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule, alisema suala la uraia pacha ni la Muungano na la kikatiba na kuwa lipo kwenye mchakato na litapatiwa ufumbuzi kwa kuwashirikisha Watanzania wote (Bara na Visiwani). Alisema kutokana na vuguvugu la mchakato wa kuwa na Katiba Mpya suala hilo linaweza kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi. Aidha, Haule alisema wizara yake imezielekeza balozi zake zote kuorodhesha Watanzania wanaoishi nje, shughuli wanazozifanya na utaalamu walionao ili kuwapa nafasi nzuri ya kuwekeza nchini kama wanataka.
IPPMedia
Viongozi wetu hawajiamini, hata hili uraia pacha wanahisi its a threat to status quo.Na wivu huu wa viongozi na wabunge wa CCM tutafikia muafaka?