Uraia pacha na Tanzania

Uraia pacha na Tanzania

Kama Balali tu hakuwa na uraia pacha alitukimbia hivihivi kweupe mchana, sasa hawa viongozi wetu mafisadi si watatumalizia rasilimali na kutukana kabisa wao sio watanzania? Kwa maadili ya Taifa hili yalivyo sasa hivi kwa kweli tuliangalie vizuri hili jambo la uraia pacha!
 
Suala la uraia pacha, limejitokeza tena kuwa hoja nzito katika mkutano wa tatu wa uratibu wa wadau Watanzania wanaoishi ughaibuni (diaspora), huku baadhi wakiitaka serikali kuharakisha mchakato wa kuanzisha utaratibu huo. Walisema Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanapata adha kubwa na wengine wanashindwa kuwekeza, kurudi au hata kusaidia familia zao kile walichochuma kwa sababu tofauti zikiwemo za usumbufu na kupanda kwa gharama.
IPPMedia

Hili swala la "Dual Citizenship" kama "Udanganyika", haliepukiki, tupende tusipende, ni lazima litakuja tu, tena tukilipokea kwa sasa, nchi itafaidika mno..Mifano iko mingi...
Kuna raia wetu waliopo pande nyingi za dunia, walioenda kihalali na kwa kubabaisha, ila wana haki za kuishi huko..Sasa kama wakiruhusiwa kupata uraia wa hapa (Ulaya na Marekani wanaruhusu dual citizenship-uraia-pacha), basi kuna mambo mengi tu mazuri nchi yetu yaweza kufaidika..

  • Kiuchumi-Kwa kuwekeza hela zao kwenye uchumi wetu, kwenye kilimo, usafirishaji, capital marketing na afya..na mengine mengi tu..
  • Michezoni-Kuna vijana wa hawa watazania walioko huko ughaibuni, wanashiriki kwenye michezo mbalimbali achilia mpira tu, wako kwenye riadha, sarakasi na filamu..sasa hawa wakipewa fursa, mbona ukwasi wa medali michezoni utapungua!
  • Elimu-Sababu ya kudorora kiuchumi huko ughaibuni, nafasi za kazi zimepungua hasa kwa ma graduates, hii itakuwa nafasi bora kwetu kugeuza kibao, kwa kufanya (brain-drain) kwa wenzetu kama wanavyo na walivyotufanyia miaka kadhaa..
  • Kijamii - Wengi tunajuwa nikiwemo pia, nina ndugu na jamaa zangu huko, wakati wa misiba, harusi, kudorora kwa afya kwa wenzangu huku bongo, ujenzi, biashara n.k. Hawa ndugu na jamaa au "Wabeba maboksi", kwa kweli huwa wanajituma sana sana kushiriki kutatua matatizo kama haya, labda wabongo wenzangu watakuwa na stori tofauti..Nina jamaa yangu yuklo zenji na pemba, wanadai jamaa zao Ulaya, huwa wanapeleka kuanzia mchele, sukari, mafuta ya kupikia na vyakula vya makopo! Amini usiamini...
  • Tukiongelea uraia-pacha, tunamaanisha hata wasio na jamaa au ndugu watanzania, wanaweza kuwa wazungu kabisa/wahindi/wachina/wajapan na hata wenzetu barani Afrika, waliokuja kama ma "expatriates", kikazi, kibiashara na wanatimiza au wametiza masharti ya kuomba uraia wetu..mie nawakaribisha wote bila hiyana kama wametimiza na ku "tick the boxes"..Hawa wote mchango wao utalifanya taifa letu liwe lakuonewa wivu duniani...
  • Na mengine mengi tu madogo kwa makubwa......

Kuna baadhi ya articles hapa chini wenye muda naomba wazipitie, kama tutaweza kuwawezesha hawa wenzetu huko kuwa pamoja nasi kiuraia..

BBC News - Africans' remittances outweigh Western aid BBC News - Africans' remittances outweigh Western aid

Africa: The overlooked role of the African Diaspora Africa: The overlooked role of the African Diaspora - Afrik-news.com : Africa news, Maghreb news - The african daily newspaper

The world economy: The magic of diasporas | The Economist The world economy: The magic of diasporas | The Economist

http://www.diaspora-centre.org/DOCS/Diaspora_Developme.pdf

African diaspora African diaspora - Wikipedia, the free encyclopedia

Social Remittances of the African Diasporas in Europe, Case studies: Netherlands and Portugal http://www.coe.int/t/dg4/nscentre/Resources/Publications/Social_Remittances_August2006_en.pdf

Finance & Development, September 2011 - Harnessing Diasporas Finance & Development, September 2011 - Harnessing Diasporas via
 
Serikali yetu imekalia kula tu, kuorodhesha watu huko ughaibuni watapewa bajet au wanataka jua idadi yao ili watoe rushwa watakayonufaika ili kuruhusu hoja ya uraia pacha kujadiliwa?
Jukumu la kujiandikisha watanzania walio ughaibuni la mtanzainia mwenyewe utaratibu unamtaka akifika nje aende ubalozi uliokaribu akajiandikishe.
 
Kama Balali tu hakuwa na uraia pacha alitukimbia hivihivi kweupe mchana, sasa hawa viongozi wetu mafisadi si watatumalizia rasilimali na kutukana kabisa wao sio watanzania? Kwa maadili ya Taifa hili yalivyo sasa hivi kwa kweli tuliangalie vizuri hili jambo la uraia pacha!

Kama Babali aliwakimbia wakati hatuna uraia pacha, bado unadhani kutokuwa nao ndio itafanya mafisadi wasiwakimbie? Yule fisadi wa chenji ya rada yuko wapi, si alikimbia? Kwa hiyo tatizo sio uraia pacha.
 
Sawa mkuu nakubaliana na wewe. Ila hili suala linapata upinzani kwasababu watu wengi watuambiwi clear benefits ni zipi. Hebu niorodhoshee faida tano kwa taifa za hii kitu.
 
Hivi kwa nini Tanzania hatuna uraia PACHA? Nini kinashindikana Na nini tatizo? Mwenye kujua naomba unijuze.

Kwa wanaoishi nje ya nchi, naona si sahihi kuwanyima haki ya nchi waliozaliwa.
 
Uraia pacha ni mzuri ila kwa usalama serikali yetu bado hawajaukubali labda miaka ya mbele huko.japo mwisho wa yote lazima pia unatumia passport moja tu huwezi ukatumia 2 hata kwa nchi zilizoruhusu.kuna mchezaji mmoja yeye sijui angechagua uraia wa nchi gani kwa sababu baba ni mjerumani na mama ni muingereza na yeye kazaliwa Canada.sasa kama huyu amiliki pass 3?. Mwisho alikuwa alikuwa anaishi uingereza tu ila anakuwa na nusu uraia wa nchi hizo nyengine,kwa mahusiano ya kihistoria ya hizo nchi anapewa ruhusa special tu.Na miaka ya karibuni ongezeko la watu hao wazazi nchi mbili tofauti wanaenda kuzaa nchi ya tatu.Mwi ni mtoto ataangalia maslahi yake kwa huko mbele.
 
Kuna madhara yoyote yanaweza kujitokeza kutokana na kuruhusu uhuru wa mtu kuwa raia wa nchi mbili?
 
Kuna madhara yoyote yanaweza kujitokeza kutokana na kuruhusu uhuru wa mtu kuwa raia wa nchi mbili?
Hakuna. Weka sheria na taratibu kwa mtu mwenye uraia pacha, basi. Mfano mwenye uraia pacha hawezi kuwa Rais. Nchi itafaidika zaidi kwa uraia pacha kuliko inavyokataza.
 
Hakuna. Weka sheria na taratibu kwa mtu mwenye uraia pacha, basi. Mfano mwenye uraia pacha hawezi kuwa Rais. Nchi itafaidika zaidi kwa uraia pacha kuliko inavyokataza.
Sasa urahia pacha ukishaweka hizo sheria tayari haina maana becoz majority wanao benefit na uraia pacha ni wenye nchi na sio wananchi.
 
Hakuna shida ya uraia pacha inabidi serikali iweke kanuni/sheria ambapo both parties benefit.
 
Sasa urahia pacha ukishaweka hizo sheria tayari haina maana becoz majority wanao benefit na uraia pacha ni wenye nchi na sio wananchi.
Hizo data kuwa wanaofaidika ni wenye nchi na sio wananchi umetoa wapi ?
 
Hizo data kuwa wanaofaidika ni wenye nchi na sio wananchi umetoa wapi ?
Afghanistan ni case study....majority ya watu ambao walikuwa members of perliment including prezda kazai waluikuwa na dual nationality...wakata wakala mihela na baada ya hapo wakasepa zao huku wanainchi wa kawaida waishia kufa njaa tuu.

Jiulize uraia pacha unamsaidiaje bodaboda mama ntilie mmachinga au fundi ujenzi na mbeba zege? Hao ndio wananchi
 
Pole kwa kukosa maarifa.
 
Pole kwa kukosa maarifa.
Aya bwana ila mie nina first hand experince maana nilifanya kazi huko so i know wat am talking about...

Kukosa maarifa ni huku kwankutamani passport za nchi nyingine. Tupambane turekebishe kwetu sio kutamani vya wenzetu tuu
 
Tanzania inaruhusu uraia pacha kwa kuzaliwa na kwa kurithi -- kwa watu wenye umri pungufu ya miaka 18. Kwa "kujilipua" ndio bado kuruhusiwa.
 
Hakuna madhara ya uraia pacha Kama sheria zikiwekwa ambazo zitadhibiti watu wenye uraia pacha wasiingie katika vitengo muhimu vya nchi Kama urais,waziri mkuu,waziri wa ulinzi,waziri mambo ya ndani,jeshi,usalama was taifa nk.
 
Back
Top Bottom