Naomba nikuulize, embu niambie sababu kubwa moja au ukiweza zaidi za kutufanya sisi turuhusu Uraia wa nchi 2, nikiimanisha Mtanzania wa kawaida(anayeishi TZ) atanufaika vipi kama huo Uraia wa nchi 2 ukiruhusiwa?
Unapofanya jambo usiangalie sana wewe directly unanufaika je, bali jaribu kufukunyua zaidi kuona taifa litanufaika je? Kimsingi wengi walio ndani wanalipiga taifa loss, maana hata mishahara wanayopata wanainyonya serikali wakati serikali haina mbinu ya kuongeza mzunguko wa fwedha.
Naomba nirudie mfano ule wa awali, ukiwa na sh milioni moja, ukaenda kijijini ukawagawia milioni na ukawakataza kutoka nje ya kijiji hicho, wataifanyia hiyo milioni biashara, wataizungusha hapa na pale ktk kijiji hicho, lakini ukirudi baada ya miaka utakuta hiyo pesa iko chini ya milioni, maana nyingine zitakuwa zimechanika na kupotea. ili hiyo pesa iongezeke lazima mtu wa-nje aingize pesa ktk kijiji hicho kwa namna yoyote, either kwa kununua kondoo kutoka kijiji hicho ama nk.
Ndivyo ilivyo kwa nyie mlio ndani, hata mkipiga kazi vipi, kama serikali haina uwezo wa kuingiza fwedha kutoka nje ya nchi na kuzitumbikiza ndani, hakuna cha kuendelea, badala yake mtakuwa mnaona viwanda vinakufa, mashirika yanakufa nk, kwa akili nyepesi mnakimbilia mafisadi. Lakini sababu kubwa ni kuwa serikali haiingizi fwedha kutoka nje ili kustimulate ulaji uliopo.
Mie nikiwa nje nikatuma euro 1000 ni fwedha clean, ambayo nimeiingiza ktk mzunguko, ni tofauti na wewe unayefanya kazi serikalini maana kodi unayolipa serikali imetoka serikalini humo humo, kimsingi hujaongeza kitu chochote. Ukibalance equation vizuri, unakuta umeinyonya serikali, maana umelipa kodi na una demand serikali ukitengenezee umeme,maji na hospitali nk, wakati mie naingiza fwedha for free with no demand.
Sasa basi, ili nchi iendelee, na mazao yenu yapate walaji kwa bei inayotakika, ili ku-weka maisha sawia, lazima serikali yenu iwe na uwezo wa kuleta fwedha kutoka nje ya nchi, na serikali haina mbinu ya kuleta hizo fwedha, inategemea watalii na madini, na watalii nao ndo hivo, madini nayo ndo hivo, maana wote hao hasa wa madini wanawaibieni na wanakuja na demand zao, kimsingi hapo ni loss tu.
Kilichobaki ni Disapora, wao wanaleta pesa bure, bila makubaliano na serikali na ndiyo njia pekee ya msingi ya serikali kuingiza fwedha clean zisizo na mawaa, hivyo basi ili serikali iweze kufua hizi fwedha lazima iwajengee wana disapora mazingira bora huko waliko ili wazichume zaidi, maana wanavyochuma huko ndivyo zinavyoongezeka kumiminika Tanzania. Wewe utanufaika je wakati huna ndugu nje ni hivi? mie nikimtumia ndugu yangu atayanunua mazao yako kwa bei nzuri, na kama wewe ni mwalimu basi huyu ndugu atakuja kusoma kwenye shule yako na kulipa fee ya utakayokenua.
Kwa msingi, huo ndo maana serikali bajeti yake haiwezi kujitegemea na badala inabidi iingie kuomba the so called donors, ili waingize fwedha ndani kwenye bajeti, na hawa donors kazi yao huwa wanategeshea chansi kama hizo ili wawape fwedha za karanga waje kuchimba hadi mchanga uhamishwe na kuwatilia sumu kwenye maji ya mito, ili wananchi wafe kwa wingi.
Kimsingi mnachoogopa ni baseless, mkumbuke hawa watanzania walio nje wana dada,kaka, wajomba,shangazi hivo kama ana jambo ambalo amenuia fanya ili kuliumiza taifa hakuna kinachomuzuia hadi hapo either ana dual ama hana.