Uraia Pacha Tanzania: Siasa ya Bernard Membe na hatma yake

Uraia Pacha Tanzania: Siasa ya Bernard Membe na hatma yake

Chifu, unaanza kusahau ulichokiandika?!?

Pale awali ulisema "wabongo wana ma qualifications......"

Ndiyo hapo sasa, wenye hizo qualifications wazielezee ili waipe uzito hoja.

Wewe unafikiri qualification nini? Mana ushaipaza sana kabla hata ya kuisikia.

Mtu anaweza kutakiwa kuongea na kuandika Kiswahili tu, aende Homeland Security kuangalia masuala ya terrorism, akawa a natural born speaker ambaye Kiswahili ni lugha yake, tayari qualification hiyo, tatizo mkoba tu, anaambiwa "kaa pembeni".

Anakwenda Mkenya Kiswahili chake cha manati, lakini kwa sababu ana mkoba anaambiwa pita.

Unaona kukataa dual kunavyoleta upuuzi?
 
German
Dual citizenship


Allowed under following circumstances:

  • If he/she is an EU or Swiss citizen during naturalization.
  • If he/she is a refugee and holds a 1951 travel document during naturalization.
  • where a child born to German parents acquires another citizenship at birth (e.g. based on place of birth, or descent from one parent)
  • where a naturalized German citizen, or a child born to non-German parents (non-EU or Swiss) in Germany, request and obtain a permission to keep his foreign nationality.
  • where a German citizen acquires a foreign nationality with the permission of the German government (e.g. existing relative ties or property in Germany or in the other country or if the occupation abroad requires domestic citizenship for execution)

Chech
Petr was a Czech citizen who has married an Australian woman, Blanche. After a few years, he successfully applied for Australian citizenship. He is permitted to keep his Czech citizenship as he has gained it in connection with a marriage, becoming a dual national.

SPAIN
dual nationality

In becoming a Spanish citizen, you may or may not obtain dual nationality or be required to renounce your current citizenship. Citizens of Latin American countries, Andorra, Portugal, the Philippines, or Equatorial Guinea are not required to renounce their citizenship, and their dual nationality is bilaterally recognized.
In other cases things can go a bit differently. For example, UK citizens, when becoming a Spanish citizen, are required to renounce their previous citizenship, yet this is not allowed by the UK. This means that you would then have two nationalities (but not dual nationality) as Spain would not recognize the UK nationality.

Pheeeww!!

Ok. Let me assume you have added one more country. 10 more are needed.
 
Kimsingi karibu nchi zote za europe zinaruhusu Dual citizenships

Source tafadhali?

kama mnavyoweza kujiwekea kwamba mkenya haruhusiwi kupata uraia wa tanzania bila kuukana uraia wake wa kenya na kuikabidhi passport.

Kuukana uraia wa Kenya na kukabidhi passport ya Kenya ili upate uraia wa Tanzania ndiyo dual citizenship unayoitaka wewe?!?
 
Source tafadhali?



Kuukana uraia wa Kenya na kukabidhi passport ya Kenya ili upate uraia wa Tanzania ndiyo dual citizenship unayoitaka wewe?!?
Unaelewa maana ya mfano wewe?
Source ya hiyo jaribu kuperuzi peruzi kabla ya ku-post, vinginevyo utaunekana pro mjuha ndugu.
 
Mbona hizo hazihitaji kuwa na uraia wa nchi mbili?
Duh! Kwa hiyo unataka kutuletea rais mwenye uraia wa Malawi sasa enh?!?
Tusipindishe issue kwa sababu tu tunataka kupindisha. Kwa sheria ya sasa ya uraia huwezi kuwa na uraia wa nchi mbili unapofikisha miaka 18. Ndio maana kuna haja ya kuibadirisha sheria kwa sababu hakuna sababu yoyote ya maana ya kumvua mtu uraia wake wa asili (Tanzania) kwa sababu tu ameomba uraia wa nchi nyingine. Ikumbukwe kama mtu hajaomba kuvuliwa uraia wake wa Tanzania basi wengine hawana mamlaka ya kumvua uraia wake.




Haki ya msingi kwa mujibu wa nani?
Kama ni haki yako kwanini uipoteze kwa kuikana na kuchukua uraia wa nchi nyingine?
Ni haki ya msingi kwa mujibu wa asili ya mtu kama asili yako ni Tanzania inabidi ibaki hivyo na hakuna mwingine anayeweza kuibadirisha sio Inzi sio jamii forums na wala katiba.Ndio maana kuna haja ya katiba kulinda haki hii ya asili.Hili wasitokee watu huko wakajiamulia kwa sababu wewe umeondoka Tanzania basi si Mtanzania.

Sasa hao wahanga wa vita wanataka uraia wa nchi mbili wa nini? Ina maana watataka kurudi kwao siku moja? Kwa hiyo nia yao ni kujibanza Tanzania kwa muda ili baadaye pakitulia kwao warudi, huku wakiwa wametutia hasara ya kuwatunza kama wakimbizi? Unafikiri Tanzania ni msamaria mwema?

Sikumaanisha hivyo katika hoja yangu. Lakini pia hao sio kipaumbele cha hoja ya msingi.

Kama ndivyo, Tanzania kuna utaratibu wa kisheria wa kuhifadhi watu wa namna hiyo. Na kama wakitaka uraia wa Tanzania, pia kuna taratibu zake. Mbona kuna wasomali wengi tu kule Tanga walishapewa uraia wa Tanzania na kupewa ardhi ya bure kabisa!!!
Ni kweli kabisa na kama tuliweza kufanya hayo basi pia tunaweza kubadilisha sheria na kuanza kuwaruhusu Watanzania waweze kuwa na uraia wa nchi mbili bila kupoteza chochote kile.

Swali kwako, ni nini hasara au matatizo ya kuruhusu uraia wa nchi mbili?
 
Sweeden
On July 1, 2001, a new Citizenship Act came into effect in Sweden. The new law makes it possible to have dual citizenship. The law also gives children further opportunity to become Swedish citizens independent of their parents

source:
http://www.swedenabroad.com/en-GB/Embassies/New-York/Services-for-Swedes/Swedish-Citizenship/Dual-Citizenship/
 
Norway
Dual nationality

Whether a child whose father or mother is a foreign national also acquires his or her nationality at birth depends on the legislation of the country in question. Queries in this connection must be addressed to the relevant authorities of the country or its diplomatic mission (Embassy, High Commissioner, Consulate General) in Norway or abroad.

Norwegian law accepts dual nationality where it is the consequence of a child's acquisition at birth of its parent's nationality. See also "Dual nationality"

source: UDI: Norwegian citizenship by birth


Denmark
Dual nationality

It is a fundamental principle of the Danish legislation that dual nationality must be restricted as much as possible.

Dual nationality is, of course, accepted in various situations, such as if persons are born with dual nationality. As an example it can be mentioned that persons born in the USA or Canada by Danish parents also acquire US or Canadian nationality at birth on the basis of the so-called territorial principle

source:https://www.nyidanmark.dk/en-us/coming_to_dk/danish_nationality/dual_nationality.htm

Dual Citizenship Russia

source: http://www.dual-citizenship.com/dual-citizenship-russia/

Austria
Dual Citizenship

In general, the Austrian Nationality Act does not allow dual citizenship except for persons who obtain two citizenships at the time they were born (e.g. a person born to Austrians living in the US acquires both Austrian and US citizenships at the time of birth).
source:http://www.austria.org/austrians/citizens/citizenship

Switzerland
Swiss legislation allows naturalized persons to have dual citizenship
source:
http://aso.ch/en/consultation/living-abroad/citizenship/dual-citizenship

Belgium
Dual citizenship for Belgians
source:
http://www.diplomatie.be/canberra/default.asp?id=81&mnu=81

Netherlands
Dual nationality

If you want to become a Dutch national, you may have to renounce your other nationality. In other cases, you are allowed to keep one or more other nationalities.
source: http://www.government.nl/issues/nationality/becoming-a-dutch-national

Finland
After June 1st, 2003 dual /multiple nationality is accepted by the Finnish legislation.
source:
http://www.finland.org/public/default.aspx?nodeid=35852&contentlan=2&culture=en-US
 
Chifu, unataka kusema mfumuko huo utakuja kama upepo na kuifanya Tanzania nayo ikumbwe na kimbunga cha dual citizenship?
I was showing recent trend of dual nationality across the world.

Chifu, hao wanachama 20 wa EU wanaosapoti dual citizenship ni wepi?

Nafahamu mataifa 7 tu yaliyo kwenye EU yenye uwepo wa dual citizenship: Italia, Ureno, UK, Slovakia, Hungaria,Ufaransa na Ireland. Lakini nyingi za nchi za EU hazina hiyo dual citizenship katika mazingira rahisi na yanayoruhusu watu kutoka nchi zote duniani. Mfano, Hispania ina makubaliano ya dual citizenship na nchi ilizozitawala kule Marekani ya Kusini. Slovenia inaruhusu dual citizenship kwa waslovenia walio expatriates katika nchi mbalimbali tu, waliokimbia nchi involuntarily.

Kwani dual citizenship lazima iruhusu watu kutoka mataifa yote duniani? Kwa hiyo, kwa Spain unaweza kusema haina dual citizenship? Au ni sawa na kusema only multilateral, but not bilateral, is a treaty? Dual nationality, may be full, partial or restricted. Kati ya hizo 20, some have full dual nationality, some have partial dual nationality and other have restricted dual nationality.

Sasa ningependa nifahamu hizo nchi 11 nyingine (tukienda na Hispania na Slovenia pia).

Hizi hazina restriction yoyote.

1. Belgium
2. Cyprus
3. France
4. Greece
5. Hungary
6. Ireland
7. Latvia
8. Poland
9. Portugal
10. Romania
11. Slovenia
12. United Kingdom

Hizi zinakubali raia kutoka mataifa yote ispokuwa Marekani.

  1. Norway
  2. Sweden

Hizi zina either partial or restricted duo nationality

Czech

Person has been living in the Czech Republic for five years and the law of their home country does not allow them to be released from their citizenship. Person obtains dual citizenship (citizenship ex-lege).

Malta: Partial

- Child born abroad, who obtains the citizenship of the birth country, is allowed to maintain dual citizenship until age 19.
- Certain native-born Maltese emigrants are permitted to possess dual citizenship.

Spain

Spain has dual citizenship treaties with the following countries: Bolivia, Chile, Ecuador,Costa Rica, Guatemala, Nicaragua, Paraguay, Peru, the Dominican Republic, Argentina, andHonduras. Spaniards residing in the above countries do not lose their rights as Spaniards if they adopt the nationality of the country of residence.

Denmark

- Danish citizen who marries a foreign national and acquires spouse's citizenship is not required to renounce Danish citizenship (so dual nationality)
- Child born abroad to Danish parents who acquires the nationality of the country of birth may keep dual citizenship until the age of 22. Before reaching the age of majority (22), the person must apply to retain citizenship.

Austria

Child of Austrian citizens who was born in a foreign country and acquired citizenship according to the other country's laws can apply for Austrian citizenship.

Also, in exceptional cases, Austrian authorities may permit an Austrian citizen who obtains a new citizenship to retain their Austrian citizenship.

Germany

- After January 1, 2000, dual citizenship is allowed until age 23.


Pia kimsingi sheria ya utaifa ya Poland haitambui dual citizenship. Kwani hata kama mpolish ana uraia wa nchi nyingine, akiwa ndani ya Poland, uraia wa nchi hiyo hautambuliki. Atatambulika kama mpolish. Ingawa watoto wanaozaliwa na wapolish popote pale walipo wanatambulika kama wapolish.

Hapo umepotosha. Mwanzoni sheria za Poland zilikuwa hazi-provide for duo nationality kwa foreigners, lakini Wapolishi hawakukatazwa kuwa na nationality ya nchini nyingine. So, it was one sided duo nationality.

Hata hivyo you may need to update your information. Mwaka huu Rais wa Poland ametia saini ya kuwa na dual citizenship to the threat of Ukraine: Foreign Ministry monitoring situation with introduction of dual citizenship in Poland
 
Wakuu,

Ingawa nimeingia late kidogo nimesoma hoja iliyoletwa na mkuu galiya.

Ametoa mifano ya nchi za wenzetu Kenya Uganda na Ghana ambao wameruhusu kitu kama hivyo, lakini ni baada ya kufanya utafiti wa kutosha kuangalia faida na hasara zakuruhusu raia wabebe pasi mbili za kusafiria.

Kenya wao wameweka utaratibu kwamba kama umepata pasi ya kigeni au upo mbioni kuipata, itabidi uombe ili wagonge muhuri au Vignette sticker kwenye pasi hiyo ya kigeni kuonyesha kwamba wewe unatambulika kuwa unayo pasi ya kigeni mbali na hiyo ya utaifa wako wa kuzaliwa.

Uganda wao walipitisha sheria hiyo mwaka 2009 na utaratibu wao unawataka raia wa Uganda wenye nia ya kuchukua pasi ya kigeni, kuwajulisha idara ya uhamiaji ya Uganda pamoja na kuwaonyesha nakala ya maombi yako.

Kwa mfano raia wa Uganda alie nchini Uingereza akifanya maombi ya pasi ya Uingereza a.k.a. kitabu chekundu, basi anatakiwa atume nakala ya fomu ya maombi kwenda Uganda ili wathibitishe kwamba maombi hayo yapo.

Lakini kuna waganda ambao hawaruhusiwi kuchukua uraia wa nchi zingine watu ambao ni raisi na baraza lake la mawaziri, na viongozi wengine waandamizi wa serikali pamoja na wakuu wa vyombo vya usalama, hii nafikiri inafahamika maana yake.

Ghana nao wameruhusu lakini si kwa wale ambao hawakuwa na uraia wa Ghana baada ya mwaka 1996 na pia hawaruhusu mtu mwenye pasi mbili kuzitumia kwa safari moja kwa minajili ya kufanya ufisadi.

Lakini sidhani kwamba hiyo ni lazima kwa raia wa nchi fulani kudai kutaka kuchukua pasi ya kigeni kwa minajili tu ya kutaka kuwa nayo kwani hilo ni suala la hiari na labda kulazimishwa na hali kama ya 1995 ambapo baadhi ya wazanzibari walilazimika kukimbilia Uingereza. Nchi kama Tanzania nayo ina haki ya kufikiria kwa kina suala hilo bila kukurupuka.

Kiukweli raia wengi wa Tanzania na wale wa nchi zingine wamehifadhi kinyume cha sheria pasi zao za nchi wanakotoka na kutumia pasi za kigeni na sababu zinajulikana zikiwamo kukwepa kulipa ada ya visa kama za kwenda USA au nchi zingine za Ulaya ambapo ukiwa na pasi za kigeni hakuna matatizo.

Ila kama lazima hiyo inamaanisha kwamba ili binadamu waishi ni lazima wale chakula sioni kwamba kuna ubaya bali subira inahitajika.

Uraia wa nchi mbili utawasaidia watanzania kusogea karibu zaidi na nyumbani, kupata nafasi ya kuwekeza na kufanya biashara kati ya ile nchi ya kigeni na nyumbani, na pia kuweza kutafuta wabia zaidi wa kigeni ili kufanya biashara mbalimbali zitakazoinua uchumi wa maeneo mengi ya nchi yetu.

Na hili si suala la pasi ya kigeni tu kutoka ughaibuni bali ni suala linalohusu pia raia wa nchi za Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda na Burundi ambao wanaingia na kutoka kila siku kwenyenchi hizo na wao wanahitaji uraia wa nchi mbili.
 
Hakuna ubaya.

Sasa kama hakuna ubaya kwa nini hutaki watu wapate huo uraia pacha?

Ila hadi sasa hakuna nchi ya kujivunia katika Afrika yetu.

Hakuna nchi ya kujivunia? Unamaanisha nini hasa?

Hakuna success stories toka Afrika za namna gani faida kwa mtu mmoja mmoja zimeleta faida kwa nchi nzima.

Huu sasa ni upofu wa makusudi tu. Hivi wewe huoni kwamba mimi nikifaidika na mimi huyu huyu nikimsaidia ndugu yangu aondokane na ufukara huoni kwamba nchi itakuwa imepungukiwa walau na fukara mmoja? Halafu kwani ni lazima kila ninachofaidika nacho mimi kama mtu binafsi basi na nchi nzima nayo lazima ifaidike nacho? Hatuko kwenye zama za ujamaa tena ndugu Nzi. You seem to be stuck in a time warp! But this is the 21st century brother-man. You need to get with the changing times or else.

Ndiyo. Wapo wanaijeria waliodusua sana Ulaya na Marekani. Je, wameifanyia nini nchi yao?

Nenda Naijeria ukaulize.

Labda nyie enthusiasts mje na mifano ya namna hizo faida za mtu mmoja mmoja zilivyoleta tija kwa taifa zima.

Hivi ni lazima faida za mtu mmoja mmoja zilete tija kwa taifa zima? Kwa mujibu wa nani? Halafu huoni kwamba mtu mmoja mmoja akifaidika na kuondokana na umaskini wa kutupwa kuwa hiyo nayo ni tija? Wewe hulioni kabisa hilo eeh?

Msije na makitu yenu ya kumasta individualism vs collectivism hapa.

Umeshindwa kabisa kutetea kwa hoja kwa nini hutaki huo uraia pacha zaidi ya kudai eti watu wamoja wamoja tu ndiyo watafaidika (jambo ambalo umesema halina ubaya na ambalo linakufunga wewe mwenyewe) na sasa umekuwa dismissive tu.

Maana nyakati zingine hayo mambo utengwa, ndiyo maana utasikia pato la taifa limekuwa huku raia mifuko ikizidi kutoboka. Na ndiyo maana pia kuna macro na micro economy.

What the hell are you talking about here?

Hata kama taifa linaundwa na mtu mmoja mmoja, katika uchumi kila pande inaweza tenganishwa na kujadiliwa kipekee.

Wewe tayari ushakubali kuwa hakuna ubaya kwa mtu mmoja mmoja kufaidika :becky:. Na sijui kwa nini wewe unaangalia upande wa uchumi tu kana kwamba uchumi ndiyo kila kitu.
 
Uraia wa nchi mbili utawasaidia watanzania kusogea karibu zaidi na nyumbani, kupata nafasi ya kuwekeza na kufanya biashara kati ya ile nchi ya kigeni na nyumbani, na pia kuweza kutafuta wabia zaidi wa kigeni ili kufanya biashara mbalimbali zitakazoinua uchumi wa maeneo mengi ya nchi yetu.


Ni jambo jema kueleweshana manufaa ambayo yanapatikana kwa kuwa na uraia wa mataifa mawili. Kwanza kama walivyoeleza wengine hakuna manufaa ambayo nchi yoyote inaweza kuyapata bila kupitia mtu mmojammoja. Vilevile si vitu vyote vinavyofanyika lazima viwe na manufaa kwa wananchi wote (wa kawaida). Kwa mfano pasi za kusafiria zinamsaidia nini (moja kwa moja) mwananchi wa kawaida? Lakini kama taifa kwa kumnufaisha mmoja anayesafiri kunakuwa na manufaa ambayo mwananchi wa kawaida hatimaye yanamfikia. Vivyo hivyo na uraia wa nchi mbili.

Uraia wa nchi mbili una manufaa mengi. Kwanza ni kudumisha uhusiano kati ya anayeshikilia uraia wa nchi mbili na nchi yake ya asili. Nikitoa mfano ambao si wa moja kwa moja (kwa watu wa diaspora), hivi kwanini Wakenya wanaona fahari kuwa na mahusiano na asili ya raisi wa Marekani hivi sasa? Hayo si manufaa ya kiuchumi au ambayo yanaweza kupimwa moja kwa moja. Unaonaje kama Kenya wangekuwa na sheria inayoruhusu uraia wa nchi mbili wakati Obama anazaliwa? Hilo kwangu ni jambo muhimu la mahusiano ya kudumu na nchi ya asili.

Pili, yakidumishwa mahusiano na Watanzania walio na uraia wa nchi nyingine ni sawa na kujiwekea hazina nje ya nchi. Hazina hii inaweza kuwa uwezo wa kiuchumi na kifedha, utaalam, umaarufu na kadhalika. Ni rahisi sana sasa kuitangaza Kenya kwa kupitia Obama kuliko kuweka matangazo lukuki CNN kuitangaza Tanzania nchini Marekani. Usishangae Kenya wakipata watalii wengi kwa kujulikana kuliko Tanzania. Kama walivyoeleza waliotangulia kuna mchango wa mali unaoletwa Tanzania na walio nje ya nchi. Wengi kwenye mjadala huu wamekubali kuwa mchango huu una manufaa angalau kwa mtu mmojammoja. Hapa wanasahau kuwa huyo mtu mmoja mmoja akinunua chochote au akilipia huduma Tanzania si kwamba tu anakuza uchumi lakini analipa kodi na hivyo kuchangia bajeti ya serikali kwa manufaa ya taifa zima. Hivyo si kweli kwamba mchango wao unanufaisha mtu mmoja mmoja tu. Lakini kama tunakubaliana kuwa mchango wa mali unanufaisha taifa je, tungependa mchango huu uendelee ama imetosha kwa kizazi hiki? Kataa kubali, wanaopeleka fedha na mali nyingine ni wale ambao wanaifahamu Tanzania na ndugu walioko Tanzania. Lakini punde wanakuwa na vizazi ambavyo vimezaliwa ugenini, hawa hawaijui Tanzania na wala ndugu walioko huko. Je, unatarajia kuwa wakiwa watu wazima wataendelea utamaduni wa wazazi wao kutuma mali Tanzania? Uwezekano ni mdogo sana. Lakini hali hiyo inabadilika kama wakiwa raia wa Tanzania (pamoja na kuwa na uraia wa nchi walikozaliwa) maana kutakuwa na mahusiano ya uraia na hivyo kuonyesha kuwa wana thamani na majukumu fulani katika uraia wao. Hazina ya utaalam walio nao raia wa Tanzania wenye uraia wa nchi nyingine unaweza kuwa muhimu sana kwa taifa hasa tunapoingia kwenye tekinolojia ambazo hazijazoeleka nchini Tanzania. Kwa sasa wataalam wa nyanja za urani na mafuta na gesi ni wachache sana nchini mwetu. Lakini usishangae kuwa tuna idadi ya kuridhisha miongoni mwa waliochukua uraia wa nchi nyingine. Hazina hii inaweza kutumika kwa ubora zaidi kama nao wangeendelea kuwa raia wa Tanzania.

Uraia wa nchi mbili utasaidia sana katika kuwawezesha Watanzania hawa kusafiri kwa urahisi wakati mwingine si kati ya nchi mbili walizo na uraia nazo tu bali duniani. Masuala ya kuhitajika kuomba visa yanaweza kupungua kama uraia wako wa nchi nyingine unakuruhusu kwenda baadhi ya nchi bila visa. Wataalam wa kupinga hili wanaweza kudai nchi inanufaikaje? Manufaa ya nchi ni dhahiri yanatokana na manufaa ya mwananchi mmoja mmoja.

Uraia wa nchi mbili utasaidia kueneza sifa nzuri la taifa letu kuliko ilivyo sasa. Mtu akiwa raia wa nchi ya kigeni atashiriki katika masuala ya nchi yake mpya na kama bado kihalali anaruhusiwa kuwa raia wa Tanzania ni dhahiri kuwa ushiriki wake kwa namna moja au nyingine utaendana na utambulisho wa asili yake (maana itakuwa halali kufanya hivyo) badala ya sasa ambapo uraia wa Tanzania analazimika kuukana pindi anapopata ule wa nchi nyingine.

Kwa vile uraia wa nchi mbili sio jambo geni duniani, naamini faida zake zinajulikana na hata kama kuna hasara pia. Ingesaidia kama wanaopinga wazo hili nao wangeelezea hasara za urai wa nchi mbili. Mimi naona manufaa ni mengi na hivyo taifa litanufaika zaidi kama uraia wa nchi mbili utaruhusiwa.

Mimi nafahamu Watanzania wenye uraia wa nchi nyingine sasa ambao wamekuwa wakiifadhili shule ya Sekondari ya Usagara, Tanga (ambako walisoma). Wameanzisha maktaba na wana mpango wa kuanzisha kupatikana kwa chakula cha mchana kwa wanafunzi (jambo linalopigwa vita na mkuu wa shule - ana mgahawa hapo shule eti). Sina hakika kwamba wazee hawa watakapoondoka duniani, vizazi vyao (ambao ni raia wa nchi nyingine) wataendeleza desturi hii njema. Watoto wao wangepewa dual citizenship uwezekano wa kuendeleza hili ungekuwa mkubwa zaidi.
 
Mkuu ulieko Magubike ahsante kwa mawazo yako mazuri sana na yanazidi kujenga hoja ya kuhakikisha suala hili linashughulikiwa na serikali.

Tunapokuwa kwenye majadiliano ni lazima kuwe na hoja ambazo zinajaribu kutafuta angalu mawazo kama ya kwako ambayo yameelezwa kwa kifupi sana.

Lakini cha msingi ni kutambua faida zilizo nyingi kuliko hasara za raia wa Tanzania kushika pasi mbili tofauti.

Mimi nimeoa mzungu na nina watoto ambao kila mara nawaleta nyumbani ili wafahamu asili ya baba yao na pia najivunia kwamba mke wangu anafahamu namna ya kupiga hata ugali na hata kupiga goti akiwasalimu wakwe zake kwa sababu nilimfundisha haya mambo kabla sijamwoa na nikamwambia ni lazima tuelimishane tamaduni zetu.

Kwahio nafahamu unachokiongea ila inashangaza kuhusu huyo headmaster na mawazo yake mgando kuhusu kupinga maendeleo ya shule yake wakati yeye pengine anatumia njia zisizo bora kwenye kuhudumia lishe ya vijana.
 
It may be so,why the word must come from? And of course this is not a plan as we think,but it is something like a mission.

Uraia wa nchi mbili kwa dunia ilipofika sasa, hakuna tena option badala yake tungejikite zaidi kuangalia sheria nzuri ya kuingoza dual. Otherwise, either accommodate it or perish.
 
Unaelewa maana ya mfano wewe?

Mfano husioendana na kitu unachokiongelea nao ni mfano? Huo ni mfano mfu!!

Huwezi kutoa mfano kuhusu uraia wa nchi mbili kwa kusema "kwa mfano, kama mnavyoweza kujiwekea kwamba mkenya haruhusiwi kupata uraia wa tanzania bila kuukana uraia wake wa kenya na kuikabidhi passport".

Sasa kama mfano wenyewe ndiyo huo, inaonyesha hata unachokipigania hukuelewi na wala hukifahamu!!

Kama nchi za Ulaya ndiyo zimejiwekea sheria kama huo mfano wako, huo uraia wa nchi mbili unaingiaje kama sheria inamtaka mtu kuukana uraia mmoja ili aruhusiwe kuwa raia wa nchi nyingine?!?!?
 
Back
Top Bottom