Uraibu wa kamari za Kichina, mabonanza na pombe kali unazidi kumaliza watumishi wa umma. CCM ipo kimya

Uraibu wa kamari za Kichina, mabonanza na pombe kali unazidi kumaliza watumishi wa umma. CCM ipo kimya

Walimu, madaktari na watumishi wa kila kada wanajimaliza kwa pombe kali na kucheza kamali za kichina maarufu kama bonanza.

Mishahara ikitoka ni kucheza makamali tu na kunywa pombe kali.

Wanasahau familia zao na kutoa matumizi.

CCM ipo kimya. Watumishi wanahitaji msaada wa kisaikolojia.
Umeacha kuongelea mambo ya maana unaongele mabonanza na pombe kali. Kibaya zaidi unaihusisha CCM yenye viongozi waliokosa DIRA eti ndo watatue changamoto hizo
 
Sasa unataka serikali au ccm iwafundishe watu kutunza familia zao??.
 
Mtu akishakuwa addicted wa kucheza hizo kamari hawezi kujinasua mwenyewe ! Ile milio na rangi rangi zinazotokea kwenye mashine za kamari mtu anapozungusha zimeteñgenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu wa kumfanya mchezaji awe teja wa hizo mashine !!
Ha haa. Kile kisahani cha kutolea hela ndio kinachonifurahisha.
Ikidondoka mia mbili. Inadondoka kwenye ngazi kama tatu hivi. Kwa hiyo mtu akila mia mbili, anakuwa kama amekula mia sita.
We uliyekaa karibu ukisikia hile mlio unajua jamaa amepuna kinoma!
 
Ila waafrika tunapenda kujiendekeza mambo ya kipumbavu yaani mtu mzima una jiita msomi una subiri CCM ije ikuelekeze ni namna gani ya kutunza familia?

Yaani hii ccm iliyo shindwa kutatua kero kama umeme na maji kwa miaka 60 ya uhuru ndo ije kuhangaika na saikorojia ya mtu aliye endekeza upumbavu.

Alafu kingine pombe na kamari mnavisingizia tu, kitu kinacho maliza hela za watz kwa sasa sio kwa wazee wala vijana ni uzinzi.

Hivi kijana anapokea mshahara wa 500,000 alafu wakati huo ana familia ya mke na watoto watatu lakini wakati huo huo ana michepuko mitatu unategemea nn zaidi ya kuitesa familia?
Pumbavu mkubwa.
 
Hili nalo ni janga kubwa sana katika jamii,
Mleta mada anza na familia yako kuwapa elimu kuhusu janga hili,

Kila mtu anayeona kua hili jambo ni hatari basi atoe elimu kwa jamaa zake wa karibu,

Tuanzie hapo kwanza.
We ni mpumbafu
 
Kuna Afisa kilimo aliajiriwa katika kijiji fulani,si unajua hawa jamaa hawanaga kazi sana na ofisi zao huwa zipo nyumbani anapoishi

Kutokana na kutokuwa na kazi ya kufanya,yeye akaona acheze makamali akihisi yanaweza kumuongezea kipato,alianza na mabonanza akawa anashinda nayo,alivyoona anapigwa sana akahamia kwenye kamali za mpira huko nako akawa ni wa kupigwa tu,unamkuta ana makaratasi kibao kama mwehu
Ajabu sana hii yaani afisa kilimo akose kazi ya kufanya daaah.
 
Ha haa. Kile kisahani cha kutolea hela ndio kinachonifurahisha.
Ikidondoka mia mbili. Inadondoka kwenye ngazi kama tatu hivi. Kwa hiyo mtu akila mia mbili, anakuwa kama amekula mia sita.
We uliyekaa karibu ukisikia hile mlio unajua jamaa amepuna kinoma!
Kuna mwamba alikula 16200. Aisee hizo kelele zake utadhani nguruwe anakula sugarcane, au mbwembwe za chawa akiwa anataka kununuliwa bia au anaomba mkopo
 
Pumbavu mkubwa.
Acha matusi mjinga ww maana ni dalili za ugonjwa wa akili yaani majitu mazima mnataka mdekezwe kama watoto ?ya kwamba serikali imekosa mambo ya kufanya mpaka ianze kuajili wanasaikolojia kwa ajili yenu?

Ishini maisha yanayo endana na mishahara yenu acheni ujinga mnazitesa familia zenu.

Ukikosa akili jua utaishi maisha magumu haijalishi unapokea mshahara mkubwa kiasi gani, maana kamari na pombe ziko dunia nzima.
 
Hiv hayo madude jwann wachina wenyewe ndio wanayasimamia.halalfu hayakubal hela isipokuwa sh 200 .huwa yanatambuaje kuw hii ni shiling 200.na yapo sana mfano hapo iringa stend ya zaman karibu na Mr hotel hivo vifrem vya kuzunguka kwa ndan kuna hilo mashiine naonaga mtu anachenji alfu 10 anapewa ma coin anaanza kuyaweka weka mle wala haesabu wala nin.
 
Ndugu zangu kila mmoja apambane kivyake kujiokoa!
Acheni kusubiri ccm ikuletee wokovu jamani!
Mkifanya hivyo kuna siku mtategemea shetani awaambie msitende dhambi ili msiende motoni!
 
Back
Top Bottom