SoC01 Uraibu wa Ngono

SoC01 Uraibu wa Ngono

Stories of Change - 2021 Competition

Jade_

Senior Member
Joined
Apr 19, 2015
Posts
122
Reaction score
214
Uraibu upo wa aina nyingi. Kuna uraibu wa pombe, sigara, madawa ya kulevya, na uraibu wa chakula. Leo nitajikita kwenye uraibu wa ngono.

Tofauti na uraibu wa pombe, sigara na madawa ya kulevya ambazo hazimpati yeyote, (sio kila mtu atangukia kwenye raibu hizi) uraibu wa chakula na ngono ni rahisi kumpata mtu yeyote, kwa sababu miili yetu kibayolojia imeumbwa kuhitaji vitu hivi. Uraibu huu ukiongezea na uraibu wa video za ngono za mtandaoni (nitaongelea siku nyingine) inawaharibu kabisa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa na kuhatarisha mustakabali wetu.

Dalili za uraibu huu ni kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengi kwa wakati mmoja. Iwe mwanaume au mwanamke, kama muda wote unawaza kufanya ngono na huwezi kujizuia basi jua kwamba una shida mahali. Kama unatumia muda mwingi sana kupita na kuzunguka kwenye maeneo ambayo unajua utakutana na watu wa kulala nao au unatumia pesa nyingi kupita uwezo wako ili upate ngono basi una shida.

Kama upo tayari kufanya chochote na lolote ili kukidhi kiu yako ya ngono, bila kujali kama unavunja sheria, unaumiza watu au unajiweka katika mazingira hatarishi una shida. Kama huoni binadamu wana utu ila ni wakulala nao tu basi kuna shida. Kama upo tayari kuvumilia kudhalilishwa na kujidhalilisha ili upate ngono, kuna shida.

Je, nini kinasababisha uraibu wa ngono? Kuna sababu nyingi lakini wataalamu wengi wanakubaliana kwamba haya ni matokeo ya kudhalilishwa kingono utotoni. Kuna wanaopapaswa sehemu za siri na wafanyakazi wa ndani. Kuna wanaoambiwa na wafanyakazi wa ndani wawapapase sehemu zao za siri. Wengine wanadai walifanya mapenzi na watu wazima walivyokuwa watoto (kwa wanaume hii ni sifa). Kuna wengine wanabakwa na ndugu jamaa, marafiki na watu wa dini. Kuna wanaoadhibiwa kwa kupigwa sehemu za siri.

Kuna wanao angalia picha na video za ngono tangia wakiwa wadogo. Chochote unachomfanyia mtoto akiwa mdogo ndicho kitakaa naye mpaka atakapoingia kaburini. Rejea uzi wangu kuhusu elimu kwa watoto wadogo . Unapomzoesha mtoto mambo ya ngono unamwekea akilini kwamba upendo na mahusiano ni ngono. Binadamu tunahitaji kuwa na mahusiano mazuri na binadamu wenzetu kusaidiana na kupeana moyo. Watu wengi ni wapweke na wanafikiri kwamba ngono ndio namna ya kuondokana na upweke.

Sababu nyingine ni jamii yetu. Tangia tukiwa wadogo tunaambiwa kwamba mwanaume kazi yake ni kutafuta ngono na mwanamke kazi yake ni kuwa chombo cha ngono. Kama wewe ni mwanaume na hufanyi mapenzi muda wote au haupo mawindoni muda wote basi unaonekana una walakini kwenye maumbile yako. Kama huna wanawake wengi kwa wakati mmoja au kama haupo tayari kufanya mapenzi na mwanamke yeyote atakayekutaka basi unakuwa kituko. Utaambiwa ndio bayolojia ya mwanaume ilivyo na muda wote anahitaji kutulizwa hamu.

Kitu ambacho siyo kweli na mara nyingi mwanaume huyu anahitaji mtu wa kumsikiliza na mtu atakayeweza kumwamini ili amtegemee. Mwanamke kama hujakaa kimvuto wa kingono unaowatamanisha wanaume basi wewe thamani yako inashuka kwenye jamii. Kama ukimtega mwanaume na hajategeka basi kama mwanamke umefeli. Kama hutamaniki huna mantiki ya kuishi. Hapa inaonyesha ya kwamba hata kama mtu alikuwa asiwe mraibu wa ngono atakuwa tu kwa sababu ndivyo jamii inavyomtaka awe.

Lakini cha kuchekesha ni kwamba jamii hiyohiyo inayokutaka uwe kiumbe cha ngono muda wote inataka pia usifanye ngono. Hizi ni jumbe mbili kinzani. Ngono inafanywa kama vile ni dhambi kubwa mno na hata hisia za kufanya ni udhaifu wako wakutenda dhambi. Hii ni sababu inayopelekea watu wa dini mara nyingi kuwa waraibu wa ngono. Wanafahamu kwamba wana shida na katika harakati za kutatua shida hiyo wanafikiri kwamba wakishika sana dini na wakijinyima kabisa kufanya ngono watakuwa amejitibu.

Wanafikiri kwamba uraibu wa ngono ni udhaifu wao na wanatakiwa kuushinda kwa namna yeyote ile, kitu ambacho si kweli. Ukijinyima sana kufanya kitu basi ndio utakuwa unakiwaza muda wote. Mtu ambaye yupo kwenye diet atawaza chakula muda wote. Hii inapelekea kusikia kesi za mapadre kulawiti watoto au viongozi wa dini kuishi maisha ya aina mbili. Mchana anahubiri, usiku ananunua machangudoa au anatembea na waumini.

Madhara ya uraibu wa ngono ni mkubwa mno. Achilia mambo ya magonjwa ya zinaa yasiyo na tiba kama UKIMWI na Kaswende (haya pia ni majanga). Mzazi ambaye ana uraibu wa kutembea na watoto atawaambukiza na wao wawe na uraibu wa kutembea na watoto wao. Na kuna uwezekano mkubwa huyo mzazi alifanyiwa hivyo na wazazi wake. Hata kama mzazi hatembei na mtoto lakini kuna uwezekano mkubwa mtoto huyo akarithi tabia hizo, yaani na yeye akawa mraibu wa ngono. Kiufupi vizazi vinaharibika.

Uraibu wa ngono unasababisha watu wabake, watembee na watoto wachanga, wanyama na tabia nyinginezo ambazo zinatisha. Watu hawa wanahatarisha maisha ya watu wanaowazunguka. Pia uraibu huu unakulevya kama madawa, muda wote unakuwa kama ndio umetoka kuamka. Huwazi kufanya chochote cha maana na unawaza ngono tu. Mahusiano ya familia na wanaokuzunguka yanazorota, unakuwa mtu wa siri sana. Kibaya pia ni matatizo ya kisaikolojia. Ngono haiwezi kutatua maumivu tuliyoyapata tukiwa wadogo na kuendelea kufanya ngono kupita kiasi kunazidisha matatizo.

Watu hawa hufanya binadamu wenzio kama vyombo vya starehe na wapo tayari kuwafanyisha vitendo vya kiudhalilishaji ili kutimiza haja zao, kama vile kulazimisha kuingia au kuingiliwa kinyume cha maumbile. Au matendo ambayo sio za kawaida. Kifo cha mende kwake ni ushamba.

Je, nini kifanyike? Kutibu uraibu wa ngono sio kitu kirahisi. Kuna mwanamke anafikiri kufanya mapenzi muda wote na mumewe kutamsaidia aridhike na asichepuke. Hii ni imani potofu. Huwezi kumsaidia mraibu wa madawa kwa kumpa madawa kila anapotaka. Au kwamba kujinyima kabisa ndio suluhisho hapana. Pia kutunza siri ya uraibu huu hasa kwenye familia hakumsaidii mraibu na wanaomzunguka. Kutunza siri kunaendeleza hii laana na kuangamiza vizazi hadi vizazi. Ni bora afungwe jela asidhuru mtu tena. Na akiwa huko apate tiba.

Mtu mwenye uraibu wa ngono anatakiwa apate ushauri wa kisaikolojia. Kwa hapa Tanzania ni ngumu kidogo kwa sababu hospitali iliyobobea kwenye mambo ya akili ni moja tu ambayo ni Mirembe. Kwa sababu hiyo basi inabidi watu wenye haya matatizo watengeneze makundi yakupeana moyo. Makundi ya kuongea na kusikilizana.

Hii ni tiba inayotoa unafuu mkubwa sana na kuwapa waraibu matumaini. Hata asasi zinazoshughulika na uraibu wa madawa na pombe zinaweza kupokea pia waraibu wa ngono (hatua za kutibu raibu zote zinafanana). Inabidi muhathirika atambue sababu ya uraibu wake. Atafanya hivi kwa kupata tiba ya muda mrefu ya ushauri nasaa. Serikali iwekeze sana kwenye miundombinu ya magonjwa ya akili hasa katika kuongeza wataalamu wa saikolojia ili waweze kutibu watu ambao kwa nje wanaonekana wapo sawa na si mpaka wawehuke ndio wapate msaada.

Wazazi na walezi jamani, tunzeni watoto wenu. Usimuache mtoto akalale kwa ndugu au jamaa, usiogope kuambiwa unadekeza mtoto, au unamficha mwanao. Tuwapende watoto na tuwasikilize ili waweze kuwatengeneza mawazo mazuri ya mahusiano na binadamu wenzio waepukane na upweke. Watu wengi ni wapweke na upweke hata siku moja hautatatuliwa kwa kufanya ngono. Mwisho kila mtu kwa imani yake na kwa Mungu wake asali sana, na amini kwamba Mungu anampenda na atamsamehe kwa makosa yake hata kama ni makubwa kiasi gani.

Kitabu cha Out of the Shadows: Understanding Sexual Addiction kilichoandikwa na Patrick Carnes Ph.D kinatoa maelezo ya undani na ya ziada kuhusu uraibu wa ngono.
 
Upvote 39
Kitovu cha yote ni upungufu wa afya akili kwa wazazi juu ya watoto wao.
 
Nani alikwambia hao wanaume wa kiarabu wanajicontrol katika mambo ya sex.
Sema tu kinachowalimit ni mazingira yao ni magumu kukutana na mwanamke kirahisi lakini bado wanatamani wapate nyama mpya kila siku.
Ndio maana wakiwa mtandaoni wanasumbua sana dada zetu kuwapigia video call na kuwatongoza.
Lakini mazingira ya kwetu yamerahisishwa kila kona tunapishans na wanawake wamejiachia na nguo za nusu uchi kama ni mwanaume uliyekamilika lazima utaingia kwenye vishawishi.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Tena hao watu wanakuwa na addiction kubwa na mara nyingi wanakua masexual deviant (wanapendelea mambo ambayo siyo ya kawaida kabisa).
 
yes mkuu wale ndio huwa wanavurugwa kabisa.
Na ni ving'ang'anizi sana kwa dada zetu hatari
 
MWILI NI BOKSI LA ROHO , NA WEWE NI ROHO. Mwili wako Utaoza , Ila Wewe Ambaye Ni Roho Utaishi Milele - Kwenye Kuishi milele utaishi kwenye pande moja wapo mbinguni au motoni. Biblia inasema zikimbieni tamaa za mwili. - Mwili hueka upinzani Mkubwa kwa Roho kwa sababu unajua utakaa kwa muda mfupi. Biblia inasema roho i radhi bali mwili ni dhaifu.
Kamwe katika dunia hii hakuna raha kwenye kitu chochote
Uzini, Porn, Punyeto huwa zina roho chafu ya kishetani, ukishafanya kitendo hiki pepo hao huuanza kufanya kazi yao na dalili ni kukosa amani, kukosa hamu ya kuishi, kujihisi hauna thamani . Kuna video nyingi Youtube zinaonesha pepo hao wakitolewa kwa maombi.
Jinsi ya Kuacha ni kumfanya Yesu kuwa role model wako. Kumbuka hakuna kitu chochote kinaweza kukupa furaha katika hii dunia - Furaha ya kweli ipo kwenye kusali na kujazwa Roho Mtakatifu rohoni mwako. Pombe , Uzinifu zina furaha ya muda na maumivu makali ya muda mrefu. STAY PURE. - MWILI NI BOKSI LA ROHO, NA WEWE NI ROHO
 
Kabisa. Haya mambo mwisho wake ni mbaya mno.
 
Uraibu upo wa aina nyingi. Kuna uraibu wa pombe, sigara, madawa ya kulevya, na uraibu wa chakula. Leo nitajikita kwenye uraibu wa ngono.

Tofauti na uraibu wa pombe, sigara na madawa ya kulevya ambazo hazimpati yeyote, (sio kila mtu atangukia kwenye raibu hizi) uraibu wa chakula na ngono ni rahisi kumpata mtu yeyote, kwa sababu miili yetu kibayolojia imeumbwa kuhitaji vitu hivi. Uraibu huu ukiongezea na uraibu wa video za ngono za mtandaoni (nitaongelea siku nyingine) inawaharibu kabisa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa na kuhatarisha mustakabali wetu.

Dalili za uraibu huu ni kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengi kwa wakati mmoja. Iwe mwanaume au mwanamke, kama muda wote unawaza kufanya ngono na huwezi kujizuia basi jua kwamba una shida mahali. Kama unatumia muda mwingi sana kupita na kuzunguka kwenye maeneo ambayo unajua utakutana na watu wa kulala nao au unatumia pesa nyingi kupita uwezo wako ili upate ngono basi una shida. Kama upo tayari kufanya chochote na lolote ili kukidhi kiu yako ya ngono, bila kujali kama unavunja sheria, unaumiza watu au unajiweka katika mazingira hatarishi una shida. Kama huoni binadamu wana utu ila ni wakulala nao tu basi kuna shida. Kama upo tayari kuvumilia kudhalilishwa na kujidhalilisha ili upate ngono, kuna shida.

Je nini kinasababisha uraibu wa ngono? Kuna sababu nyingi lakini wataalamu wengi wanakubaliana kwamba haya ni matokeo ya kudhalilishwa kingono utotoni. Kuna wanaopapaswa sehemu za siri na wafanyakazi wa ndani. Kuna wanaoambiwa na wafanyakazi wa ndani wawapapase sehemu zao za siri. Wengine wanadai walifanya mapenzi na watu wazima walivyokuwa watoto (kwa wanaume hii ni sifa). Kuna wengine wanabakwa na ndugu jamaa, marafiki na watu wa dini. Kuna wanaoadhibiwa kwa kupigwa sehemu za siri. Kunawanao angalia picha na video za ngono tangia wakiwa wadogo. Chochote unachomfanyia mtoto akiwa mdogo ndicho kitakaa naye mpaka atakapoingia kaburini. Rejea uzi wangu kuhusu elimu kwa watoto wadogo . Unapomzoesha mtoto mambo ya ngono unamwekea akilini kwamba upendo na mahusiano ni ngono. Binadamu tunahitaji kuwa na mahusiano mazuri na binadamu wenzetu kusaidiana na kupeana moyo. Watu wengi ni wapweke na wanafikiri kwamba ngono ndio namna ya kuondokana na upweke.

Sababu nyingine ni jamii yetu. Tangia tukiwa wadogo tunaambiwa kwamba mwanaume kazi yake ni kutafuta ngono na mwanamke kazi yake ni kuwa chombo cha ngono. Kama wewe ni mwanaume na hufanyi mapenzi muda wote au haupo mawindoni muda wote basi unaonekana una walakini kwenye maumbile yako. Kama huna wanawake wengi kwa wakati mmoja au kama haupo tayari kufanya mapenzi na mwanamke yeyote atakayekutaka basi unakuwa kituko. Utaambiwa ndio bayolojia ya mwanaume ilivyo na muda wote anahitaji kutulizwa hamu. Kitu ambacho siyo kweli na mara nyingi mwanaume huyu anahitaji mtu wa kumsikiliza na mtu atakayeweza kumwamini ili amtegemee. Mwanamke kama hujakaa kimvuto wa kingono unaowatamanisha wanaume basi wewe thamani yako inashuka kwenye jamii. Kama ukimtega mwanaume na hajategeka basi kama mwanamke umefeli. Kama hutamaniki huna mantiki ya kuishi. Hapa inaonyesha ya kwamba hata kama mtu alikuwa asiwe mraibu wa ngono atakuwa tu kwa sababu ndivyo jamii inavyomtaka awe.

Lakini cha kuchekesha ni kwamba jamii hiyohiyo inayokutaka uwe kiumbe cha ngono muda wote inataka pia usifanye ngono. Hizi ni jumbe mbili kinzani. Ngono inafanywa kama vile ni dhambi kubwa mno na hata hisia za kufanya ni udhaifu wako wakutenda dhambi. Hii ni sababu inayopelekea watu wa dini mara nyingi kuwa waraibu wa ngono. Wanafahamu kwamba wana shida na katika harakati za kutatua shida hiyo wanafikiri kwamba wakishika sana dini na wakijinyima kabisa kufanya ngono watakuwa amejitibu. Wanafikiri kwamba uraibu wa ngono ni udhaifu wao na wanatakiwa kuushinda kwa namna yeyote ile, kitu ambacho si kweli. Ukijinyima sana kufanya kitu basi ndio utakuwa unakiwaza muda wote. Mtu ambaye yupo kwenye diet atawaza chakula muda wote. Hii inapelekea kusikia kesi za mapadre kulawiti watoto au viongozi wa dini kuishi maisha ya aina mbili. Mchana anahubiri, usiku ananunua machangudoa au anatembea na waumini.

Madhara ya uraibu wa ngono ni mkubwa mno. Achilia mambo ya magonjwa ya zinaa yasiyo na tiba kama UKIMWI na Kaswende (haya pia ni majanga). Mzazi ambaye ana uraibu wa kutembea na watoto atawaambukiza na wao wawe na uraibu wa kutembea na watoto wao. Na kuna uwezekano mkubwa huyo mzazi alifanyiwa hivyo na wazazi wake. Hata kama mzazi hatembei na mtoto lakini kuna uwezekano mkubwa mtoto huyo akarithi tabia hizo, yaani na yeye akawa mraibu wa ngono. Kiufupi vizazi vinaharibika.

Uraibu wa ngono unasababisha watu wabake, watembee na watoto wachanga, wanyama na tabia nyinginezo ambazo zinatisha. Watu hawa wanahatarisha maisha ya watu wanaowazunguka. Pia uraibu huu unakulevya kama madawa, muda wote unakuwa kama ndio umetoka kuamka. Huwazi kufanya chochote cha maana na unawaza ngono tu. Mahusiano ya familia na wanaokuzunguka yanazorota, unakuwa mtu wa siri sana. Kibaya pia ni matatizo ya kisaikolojia. Ngono haiwezi kutatua maumivu tuliyoyapata tukiwa wadogo na kuendelea kufanya ngono kupita kiasi kunazidisha matatizo.

Watu hawa hufanya binadamu wenzio kama vyombo vya starehe na wapo tayari kuwafanyisha vitendo vya kiudhalilishaji ili kutimiza haja zao, kama vile kulazimisha kuingia au kuingiliwa kinyume cha maumbile. Au matendo ambayo sio za kawaida. Kifo cha mende kwake ni ushamba.

Je nini kifanyike? Kutibu uraibu wa ngono sio kitu kirahisi. Kuna mwanamke anafikiri kufanya mapenzi muda wote na mumewe kutamsaidia aridhike na asichepuke. Hii ni imani potofu. Huwezi kumsaidia mraibu wa madawa kwa kumpa madawa kila anapotaka. Au kwamba kujinyima kabisa ndio suluhisho hapana. Pia kutunza siri ya uraibu huu hasa kwenye familia hakumsaidii mraibu na wanaomzunguka. Kutunza siri kunaendeleza hii laana na kuangamiza vizazi hadi vizazi. Ni bora afungwe jela asidhuru mtu tena. Na akiwa huko apate tiba.

Mtu mwenye uraibu wa ngono anatakiwa apate ushauri wa kisaikolojia. Kwa hapa Tanzania ni ngumu kidogo kwa sababu hospitali iliyobobea kwenye mambo ya akili ni moja tu ambayo ni Mirembe. Kwa sababu hiyo basi inabidi watu wenye haya matatizo watengeneze makundi yakupeana moyo. Makundi ya kuongea na kusikilizana. Hii ni tiba inayotoa unafuu mkubwa sana na kuwapa waraibu matumaini. Hata asasi zinazoshughulika na uraibu wa madawa na pombe zinaweza kupokea pia waraibu wa ngono (hatua za kutibu raibu zote zinafanana). Inabidi muhathirika atambue sababu ya uraibu wake. Atafanya hivi kwa kupata tiba ya muda mrefu ya ushauri nasaa. Serikali iwekeze sana kwenye miundombinu ya magonjwa ya akili hasa katika kuongeza wataalamu wa saikolojia ili waweze kutibu watu ambao kwa nje wanaonekana wapo sawa na si mpaka wawehuke ndio wapate msaada.

Mada nzuri na umeiwasilisha na kuchangia vyema.Nina ndugu yangu wa karibu tu nadhani ana hili tatizo.
Mwaka jana ameponea chupuchupu miaka 30 jela baada ya kukata rufaa maana alishafungwa. Sababu ameshitakiwa kubaka mtoto wa miaka 6.Ushahidi haukuwepo wa kutosha ndio kilichomuokoa ila hata sisi ndugu zake tunajua n kweli alifanya au alikaribia kufanya.

Na hii tuna recall matukio yake ya nyuma n mengi na mabaya sio watoto,wanyama ,wazee ,wake za watu,chabo yaani ni uchafu haswaa nadhan kila unaoujua na cha ajabu ana mke na watoto.

Kwasasa toka atoke jela sijaskia chochote ila najua n muda tu atarudi.Naumia na sijui vipi tutamsaidia.Hebu nipe mawazo.
 
Mungu wangu. Poleni sana. Ahsante mkuu kwa mchango wako.
Huyo ndugu yenu ni kweli kabisa ana uraibu wa ngono tena ule wa level ya juu kabisaa. Mfanye namna yeyote ya kumdhibiti kwa sababu atazidi kuharibu watu na mtashangaa wanaokua karibu yake wanakuja kuwa na matatizo kama yake.
Ilitakiwa afungwe jela au hata afungiwe ndani alafu atafutiwe msaada wa kisaikolojia. Ifahamike hii tabia yake ilianza lini, chanzo chake na namna ya kuirekebisha kama itawezekana.
Hatakiwi kabisa kukaa karibu na watoto hata kama ni wakwake.
Mie pia nilitamani hata angefungwa miaka hata miwili..sielew ana bahat gani hakukaa hata miezi sita.

Mama yake anamkingia kifua sana anasema watu wanamsingizia mwanae kwahio hata kuwashauri watu swala la mwanasaikolojia watakataa..maana wanaukataa ukweli.

Sema alivyotoka jela majirani na watu wanaomfahamu waliumia sana.Wamepanga sasa hivi akikutwa anafanya tukio watamuua tu. Inasikitisha sana ila ndo ipo hivyo.

Anaishi na watoto wake wote mpaka wa mwanamke wa mwanzo mie naogopa pia kwa wanae.Mkewe mwenyewe ana mnyanyasa ni bint mdogo nahisi hata manyanyaso ya kingono yatakuwepo pia.
 
Uraibu upo wa aina nyingi. Kuna uraibu wa pombe, sigara, madawa ya kulevya, na uraibu wa chakula. Leo nitajikita kwenye uraibu wa ngono.

Tofauti na uraibu wa pombe, sigara na madawa ya kulevya ambazo hazimpati yeyote, (sio kila mtu atangukia kwenye raibu hizi) uraibu wa chakula na ngono ni rahisi kumpata mtu yeyote, kwa sababu miili yetu kibayolojia imeumbwa kuhitaji vitu hivi. Uraibu huu ukiongezea na uraibu wa video za ngono za mtandaoni (nitaongelea siku nyingine) inawaharibu kabisa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa na kuhatarisha mustakabali wetu.

Dalili za uraibu huu ni kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengi kwa wakati mmoja. Iwe mwanaume au mwanamke, kama muda wote unawaza kufanya ngono na huwezi kujizuia basi jua kwamba una shida mahali. Kama unatumia muda mwingi sana kupita na kuzunguka kwenye maeneo ambayo unajua utakutana na watu wa kulala nao au unatumia pesa nyingi kupita uwezo wako ili upate ngono basi una shida. Kama upo tayari kufanya chochote na lolote ili kukidhi kiu yako ya ngono, bila kujali kama unavunja sheria, unaumiza watu au unajiweka katika mazingira hatarishi una shida. Kama huoni binadamu wana utu ila ni wakulala nao tu basi kuna shida. Kama upo tayari kuvumilia kudhalilishwa na kujidhalilisha ili upate ngono, kuna shida.

Je nini kinasababisha uraibu wa ngono? Kuna sababu nyingi lakini wataalamu wengi wanakubaliana kwamba haya ni matokeo ya kudhalilishwa kingono utotoni. Kuna wanaopapaswa sehemu za siri na wafanyakazi wa ndani. Kuna wanaoambiwa na wafanyakazi wa ndani wawapapase sehemu zao za siri. Wengine wanadai walifanya mapenzi na watu wazima walivyokuwa watoto (kwa wanaume hii ni sifa). Kuna wengine wanabakwa na ndugu jamaa, marafiki na watu wa dini. Kuna wanaoadhibiwa kwa kupigwa sehemu za siri. Kunawanao angalia picha na video za ngono tangia wakiwa wadogo. Chochote unachomfanyia mtoto akiwa mdogo ndicho kitakaa naye mpaka atakapoingia kaburini. Rejea uzi wangu kuhusu elimu kwa watoto wadogo . Unapomzoesha mtoto mambo ya ngono unamwekea akilini kwamba upendo na mahusiano ni ngono. Binadamu tunahitaji kuwa na mahusiano mazuri na binadamu wenzetu kusaidiana na kupeana moyo. Watu wengi ni wapweke na wanafikiri kwamba ngono ndio namna ya kuondokana na upweke.

Sababu nyingine ni jamii yetu. Tangia tukiwa wadogo tunaambiwa kwamba mwanaume kazi yake ni kutafuta ngono na mwanamke kazi yake ni kuwa chombo cha ngono. Kama wewe ni mwanaume na hufanyi mapenzi muda wote au haupo mawindoni muda wote basi unaonekana una walakini kwenye maumbile yako. Kama huna wanawake wengi kwa wakati mmoja au kama haupo tayari kufanya mapenzi na mwanamke yeyote atakayekutaka basi unakuwa kituko. Utaambiwa ndio bayolojia ya mwanaume ilivyo na muda wote anahitaji kutulizwa hamu. Kitu ambacho siyo kweli na mara nyingi mwanaume huyu anahitaji mtu wa kumsikiliza na mtu atakayeweza kumwamini ili amtegemee. Mwanamke kama hujakaa kimvuto wa kingono unaowatamanisha wanaume basi wewe thamani yako inashuka kwenye jamii. Kama ukimtega mwanaume na hajategeka basi kama mwanamke umefeli. Kama hutamaniki huna mantiki ya kuishi. Hapa inaonyesha ya kwamba hata kama mtu alikuwa asiwe mraibu wa ngono atakuwa tu kwa sababu ndivyo jamii inavyomtaka awe.

Lakini cha kuchekesha ni kwamba jamii hiyohiyo inayokutaka uwe kiumbe cha ngono muda wote inataka pia usifanye ngono. Hizi ni jumbe mbili kinzani. Ngono inafanywa kama vile ni dhambi kubwa mno na hata hisia za kufanya ni udhaifu wako wakutenda dhambi. Hii ni sababu inayopelekea watu wa dini mara nyingi kuwa waraibu wa ngono. Wanafahamu kwamba wana shida na katika harakati za kutatua shida hiyo wanafikiri kwamba wakishika sana dini na wakijinyima kabisa kufanya ngono watakuwa amejitibu. Wanafikiri kwamba uraibu wa ngono ni udhaifu wao na wanatakiwa kuushinda kwa namna yeyote ile, kitu ambacho si kweli. Ukijinyima sana kufanya kitu basi ndio utakuwa unakiwaza muda wote. Mtu ambaye yupo kwenye diet atawaza chakula muda wote. Hii inapelekea kusikia kesi za mapadre kulawiti watoto au viongozi wa dini kuishi maisha ya aina mbili. Mchana anahubiri, usiku ananunua machangudoa au anatembea na waumini.

Madhara ya uraibu wa ngono ni mkubwa mno. Achilia mambo ya magonjwa ya zinaa yasiyo na tiba kama UKIMWI na Kaswende (haya pia ni majanga). Mzazi ambaye ana uraibu wa kutembea na watoto atawaambukiza na wao wawe na uraibu wa kutembea na watoto wao. Na kuna uwezekano mkubwa huyo mzazi alifanyiwa hivyo na wazazi wake. Hata kama mzazi hatembei na mtoto lakini kuna uwezekano mkubwa mtoto huyo akarithi tabia hizo, yaani na yeye akawa mraibu wa ngono. Kiufupi vizazi vinaharibika.

Uraibu wa ngono unasababisha watu wabake, watembee na watoto wachanga, wanyama na tabia nyinginezo ambazo zinatisha. Watu hawa wanahatarisha maisha ya watu wanaowazunguka. Pia uraibu huu unakulevya kama madawa, muda wote unakuwa kama ndio umetoka kuamka. Huwazi kufanya chochote cha maana na unawaza ngono tu. Mahusiano ya familia na wanaokuzunguka yanazorota, unakuwa mtu wa siri sana. Kibaya pia ni matatizo ya kisaikolojia. Ngono haiwezi kutatua maumivu tuliyoyapata tukiwa wadogo na kuendelea kufanya ngono kupita kiasi kunazidisha matatizo.

Watu hawa hufanya binadamu wenzio kama vyombo vya starehe na wapo tayari kuwafanyisha vitendo vya kiudhalilishaji ili kutimiza haja zao, kama vile kulazimisha kuingia au kuingiliwa kinyume cha maumbile. Au matendo ambayo sio za kawaida. Kifo cha mende kwake ni ushamba.

Je nini kifanyike? Kutibu uraibu wa ngono sio kitu kirahisi. Kuna mwanamke anafikiri kufanya mapenzi muda wote na mumewe kutamsaidia aridhike na asichepuke. Hii ni imani potofu. Huwezi kumsaidia mraibu wa madawa kwa kumpa madawa kila anapotaka. Au kwamba kujinyima kabisa ndio suluhisho hapana. Pia kutunza siri ya uraibu huu hasa kwenye familia hakumsaidii mraibu na wanaomzunguka. Kutunza siri kunaendeleza hii laana na kuangamiza vizazi hadi vizazi. Ni bora afungwe jela asidhuru mtu tena. Na akiwa huko apate tiba.

Mtu mwenye uraibu wa ngono anatakiwa apate ushauri wa kisaikolojia. Kwa hapa Tanzania ni ngumu kidogo kwa sababu hospitali iliyobobea kwenye mambo ya akili ni moja tu ambayo ni Mirembe. Kwa sababu hiyo basi inabidi watu wenye haya matatizo watengeneze makundi yakupeana moyo. Makundi ya kuongea na kusikilizana. Hii ni tiba inayotoa unafuu mkubwa sana na kuwapa waraibu matumaini. Hata asasi zinazoshughulika na uraibu wa madawa na pombe zinaweza kupokea pia waraibu wa ngono (hatua za kutibu raibu zote zinafanana). Inabidi muhathirika atambue sababu ya uraibu wake. Atafanya hivi kwa kupata tiba ya muda mrefu ya ushauri nasaa. Serikali iwekeze sana kwenye miundombinu ya magonjwa ya akili hasa katika kuongeza wataalamu wa saikolojia ili waweze kutibu watu ambao kwa nje wanaonekana wapo sawa na si mpaka wawehuke ndio wapate msaada.

Wazazi na walezi jamani, tunzeni watoto wenu. Usimuache mtoto akalale kwa ndugu au jamaa, usiogope kuambiwa unadekeza mtoto, au unamficha mwanao. Tuwapende watoto na tuwasikilize ili waweze kuwatengeneza mawazo mazuri ya mahusiano na binadamu wenzio waepukane na upweke. Watu wengi ni wapweke na upweke hata siku moja hautatatuliwa kwa kufanya ngono. Mwisho kila mtu kwa imani yake na kwa Mungu wake asali sana, na amini kwamba Mungu anampenda na atamsamehe kwa makosa yake hata kama ni makubwa kiasi gani.

Kitabu cha Out of the Shadows: Understanding Sexual Addiction kilichoandikwa na Patrick Carnes Ph.D kinatoa maelezo ya undani na ya ziada kuhusu uraibu wa ngono.
Kitabu hiki nakipataje
 
Mimi nadhani akili ukiipush kwenye sex ndio sababu kwanini tusipush akili kwenye kazi kujisomea na kuachana na magroup yanayohusu sex kuangalia porn na vinginekama hivyo
 
Mkuu unajua kitu kinachoitwa nyege?ndio maana mapadre wanabaka kwa sababu ya nyege,wenye nyumba wanabaka mahousegirl kwa sababu ya nyege,watu wanabaka wanafunzi na kuishia jela kwa sababu ya nyege.
Ukiwa na nyege huwezi kusoma ukaelewa lazima utakitupa chini hadi ukaziondoe nyege kwanza ndipo akili itakaa sawa
 
Mada nzuri na umeiwasilisha na kuchangia vyema.Nina ndugu yangu wa karibu tu nadhani ana hili tatizo.
Mwaka jana ameponea chupuchupu miaka 30 jela baada ya kukata rufaa maana alishafungwa. Sababu ameshitakiwa kubaka mtoto wa miaka 6.Ushahidi haukuwepo wa kutosha ndio kilichomuokoa ila hata sisi ndugu zake tunajua n kweli alifanya au alikaribia kufanya.

Na hii tuna recall matukio yake ya nyuma n mengi na mabaya sio watoto,wanyama ,wazee ,wake za watu,chabo yaani ni uchafu haswaa nadhan kila unaoujua na cha ajabu ana mke na watoto.

Kwasasa toka atoke jela sijaskia chochote ila najua n muda tu atarudi.Naumia na sijui vipi tutamsaidia.Hebu nipe mawazo.
Nidhahiri kuwa katika ulimwengu wa roho kuna roho wachafu. Hakuna mtu anaye penda kuabika au kudhalilishwa kama ilivyo kwa ndugu yako

Ndugu yako huyo yeye kama yeye hana tatizo, tatizo ni kitu kilichopo ndani yake ambacho kinamzidi nguvu kwenye kufanya maamuzi. Hiyo ndiyo roho ambayo ametupiwa kutokana vyanzo mbalimbali

Hakuna namna ya kumsaidia mtu kama huyo bila kufanyiwa delivarence. Kwa kuombewa tu, atarudi kwenye hali yake nzuri ya kawaida

Kuwafunga jela, kuwaua sio solution. Ndio maana kesi za namna hyo haziiishi hata wangefungwa miaka 100. Ukimuua hiyo roho chafu inahamia kwa mtu mwingine ambae ni fresh kabisa na tatizo litakua palepale
 
MWILI NI BOKSI LA ROHO , NA WEWE NI ROHO. Mwili wako Utaoza , Ila Wewe Ambaye Ni Roho Utaishi Milele - Kwenye Kuishi milele utaishi kwenye pande moja wapo mbinguni au motoni. Biblia inasema zikimbieni tamaa za mwili. - Mwili hueka upinzani Mkubwa kwa Roho kwa sababu unajua utakaa kwa muda mfupi. Biblia inasema roho i radhi bali mwili ni dhaifu.
Kamwe katika dunia hii hakuna raha kwenye kitu chochote
Uzini, Porn, Punyeto huwa zina roho chafu ya kishetani, ukishafanya kitendo hiki pepo hao huuanza kufanya kazi yao na dalili ni kukosa amani, kukosa hamu ya kuishi, kujihisi hauna thamani . Kuna video nyingi Youtube zinaonesha pepo hao wakitolewa kwa maombi.
Jinsi ya Kuacha ni kumfanya Yesu kuwa role model wako. Kumbuka hakuna kitu chochote kinaweza kukupa furaha katika hii dunia - Furaha ya kweli ipo kwenye kusali na kujazwa Roho Mtakatifu rohoni mwako. Pombe , Uzinifu zina furaha ya muda na maumivu makali ya muda mrefu. STAY PURE. - MWILI NI BOKSI LA ROHO, NA WEWE NI ROHO
Mkuu kwanini roho iwekwe kwenye mwili huu dhaifu?
Maana yanayoonekana mwilini ni manifestation ya yanayoendelea huko ndani,

Kujikataa kuwa wewe sio mwili ni roho pekee ni kujaribu kujikimbia ,kitu ambacho huwezi,

As long as you live hapa duniani
Mwili na roho vyote ni wewe ,na ndio maana utaadhibiwa KWA matendo uliyotenda KWA mwili wako.

Unaweza kunisaidia kuclarify zaidi kama nakosea
 
Pole sana mkuu. Wanasaikolojia Tanzania wapo wachache. Labda upate matibabu hospitali ya Mirembe.

Kama kufika Mirembr ni shida, mtafute hata kiongozi wa dini yako (kama unayo). Lakini uwe makini kwa sababu hawa watu wanaweza kukuongezea ugonjwa. Tafuta mtu yeyote ambaye ni muelewa ambaye hatokuhukumu.

Na pia lazima utambue tatizo lako lilaanza lini.
Je maisha yako ya utotoni yalikuwaje?
Je Tinde,Tanga hapafai?
 
Mkuu hii mada yako ni murua sana na ina uhalisia kwa asilimia kubwa pia. Kisababishi kikuu cha hili nadhani ni kutumia muda mwingi tukiwa idle sana au mazingira yanayotuzunguka yanatuaminisha sex inakupa definition kubwa kuhusu uanaume/urijali wako.
Nachangia tu namna ya kuepuka au kuachana na hii hali pamoja na mengi yaliyokwisha kusemwa lingine ni kumcha Mungu na kuishi kwa vipaumbele vyenye manufaa zaidi maishani mwako badala ya sex.

Kitu ambaho watu wengi hatuwezi kukigundua mapema ni namna hii staili ya maisha inavyotafuna pesa kiasi kwamba ni rahisi kuamini kwenye mambo ya chuma ulete. Tukiishi kwa malengo ya kujiimarisha kiuchumi kila senti yetu itakuwa na maana na itakuwa ngumu kuitumia kwa starehe ya aina hii isiyozalisha asilani.
 
Back
Top Bottom