Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?


Kwa msimamo wa baadhi ya wana cdm,wameshamteua mtu wao wa kugombea urais 2015 ambaye ni Dr. Slaa, ndani ya chadema hakuna demokrasia ya ushindani bali ni uteuzi. Kumbuka uchaguzi wa mwenyekiti mwaka 2009, Mbowe aliteuliwa, hakuchaguliwa na wanachama !
 
Bunge lililopita nilimsikia Zitto Zuberi Kabwe akisema ana orodha ya watanzania hasa viongozi wenye account nchi za ng'ambo zilizotumika kuficha pesa za wananchi wake wa Kigoma Kaskazini na waTanzania kwa ujumla. Alitoa muda kwa serikali iwataje yenyewe la sivyo atawataja yeye (Zitto). Nilitoka kidogo sijafuatilia kama serikali imeshawataja, na kama haijawataja Zito ameshawataja sasa?

Katika hali ya kawaida (common sense) mtu aliyekuibia nyumbani kwako kama unamjua kwa sura na kwa jina unasubiri nini kuchukua hatua arudishe mali yako? Kuchelea kuwataja kunatoa tafsiri mbalimbali kwa umma, kunaashiria wingu la kutaka rushwa toka kwa wahusika wasitajwe. Hatuwezi kuwa na vijana kama hawa tuliowatuma wakatukamatie wezi wa nchi halafu wanafanya mzaha wa aina hii.

Kama mwananchi una taarifa ya waporaji wa nchi yako toa taarifa kwa wananchi wako ili wajue nini cha kumfanya mporaji, usijenge mazingira ya kupewe rushwa. Maana hela zinazoporwa ndio mshahara, madawati, maji, vitabu shuleni, nyumba za walimu, barabara, dawa hospitalini, n.k
 

Nahisi hii ni mada inayojitegemea na imeunganishwa hapa kimakosa. Hii ndo yenye kichwa cha Zitto na Rushwa Ni Kama Uji na Mgonjwa, au siyo?
 
Kumekuwepo na habari za muda mrefu na ambazo baadaye zimekuja kuthibitishwa na muhusika mwenyewe Mhe, Zitto pale alipowaambia wapiga kura wake kuwa mwaka 2015 hana mpango wa kugombea ubunge tena, bali harakati zake zinaangalia urais kupitia CDM.
Kama katiba inavyosema kuwa kila raia anayo haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi katika ngazi yoyote ili mradi awe ametimiza kanuni zote kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kwangu mimi sina ugomvi na hilo, bali wasiwasi wangu kwa ndugu yangu huyu ni pale mnapotaka kuwachanganya wale wafuasi wenu. Ikumbukwe kuwa Chadema kama chama kikuu cha upinzani hapa nchini kwa sasa kipo katika wakati wa mapambano wa kuhakikisha kinaendelea kuongeza namba ya wapiga kura wake ili kiweze kupita ki-urahisi na kuweza kutwaa madaraka hapo 2015!! Sasa inapofika wakati hata wale wachache ambao tayari wameweza kuvunwa kwa kipindi hiki halafu ndani ya chama hichohicho mkaanza kuwagawa makundi, Je, si kwamba ni kutoa nafasi ya kukifanya CCM kiendelee kujihakikishia utawala kwa kura zake zilezile??

Zitto Kabwe ni mwanasiasa kijana kama mimi japo namzidi umri, lakini pia ni mtu makini na mchambuzi/mfuatiliaji wa mambo kwa kina. Hata hivyo pamoja na kuwa na sifa hizo kwangu mimi bado namuona kama ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi akiwa chini ya mtu kama Dr. Slaa ukizingatia kuwa pamoja na kuwa mbunge ambaye amejizolea sifa nyingi kwa kuibua mijadala na kujenga hoja zenye mashiko, lakini muda wa yeye kukabidhiwa nchi kama hii bado haujafika.

Hitimisho. Kama alivyoandika Mzee wangu Mayage S. Mayage katika makala yake ndani ya Raia mwema Oct 3-Oct 9, 2012, kwamba “Katika mazingira hayo, ni muhimu kwa kila kiongozi wa Chadema mwenye njozi za kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa kuchukua tahadhari katika njozi zake hizo! Kila mtanzania, na hasa mwanachama wa chadema anajua ni mwanasiasa gani ndani ya chama hicho ambaye leo hii amekifikisha hapo kilipo. Na hao ndio wenye uamzi wa mwisho wa kusema wanamtaka nani 2015. kinyume na hapo ni kutaka kuleta fujo tu kwa agenda iliyojificha!!” Tafakali.

Miwatamu.
 


Kwanini Unataka huyo MLAFI WA MADARAKA AJADILIWE KWA MAPANA ? ILI AJISIKIE KUWA HE"S ABOVE ALL OTHER'S ??? MWACHENI TUNAMPA MSISITIZO USIO NA MAANA na atajisikia na kutuharibia nchi yetu...
EMBU ANGALIA HOJA ZILIZOMO HUMU ZOTE NI ZA HUYO BWANA AMBAYE NI MBINAFSI, MCHOYO na MPWEKE...
 
Tuujadili uraisi kwa mapana au tumjadili Zitto kwa mapana.kama ni uraisi licha ya kutokidhi vigezo, hata chama chake hakijamteua bado. Ni vema angekua na ndoto za uwaziri mkuu.
 
Mh Zitto ni mwanasiasa makini na kujitangaza kuwania nafasi hiyo hivi sasa ni Ujasiri wa kuungwa mkono. Makundi hayakwepeki, lamaana ni kufahamiana, kujadiliana na kuheshimiana. Wote wanaowania Urais, ni bora wajitokeze sasa hivi, ili wananchi tuwe na muda mwingi kuwafuatilia mienendo yao.
 
sioni sababu ya kujadili, ni kuikuza na kumpa sifa.
Mwerevu anajua nini cha kutamka na wakati gani.
Aitafute kwanza hekima.
 
Tuujadili uraisi kwa mapana au tumjadili Zitto kwa mapana.kama ni uraisi licha ya kutokidhi vigezo, hata chama chake hakijamteua bado. Ni vema angekua na ndoto za uwaziri mkuu.
Ni wazi kabisa CHADEMA ikitwaa madaraka ZZK lazima aukwae uwaziri tena wizara nyeti. Badala yake yupo busy na kuutaka urais kama siyo kutumiwa na CCM ni nini?

Katika hali yoyote ile kwayeye kuupata urais itamchukua si chini ya miaka kumi kwasababu kila mpenda mabadiliko angependa kuuona utendaji wake kwanza ZZK kama waziri kabla hatujamwamini kwa ngazi ya urais.

He needs to grow up first! For Christ's sake he doesn't even have a wife
 
ZeMarcopolo

Today 12:55
​

JF Senior Expert MemberArray


​


[h=2]
Re: Dr. Slaa: Josephine alikuwa mtaalam pekee wa IT wa UNHCR kanda ya Africa, ni international figur[/h]
Dr. Slaa siku hizi anapenda zaidi MIPASHO kuliko issues. Hii ni dalili ya kukata tamaa ya Urais.
Nadhani Pasco alikuwa sahihi aliposema Slaa hatagombea Urais. mtu anayetaka Urais hawezi kudwel kwenye MIPASHO namna hii wakati wananchi wanachinjana Geita...

Mkuu Ze Marco, hii thread kule imefungwa, hivyo nimeona nikujibu humu kwa sababu hapa ndipo nilipoweka ule mtazama!. Sijasema Dr. Slaa hagombei, nimesema msimamo wake naujua!, na wakati akiutoa msimamo huo, alikuwa na wife wake!. Huo msimamo sijautangaza humu kwa sababu mazungumzo yetu hayakuwa rasmi (off the record).

Nadhani umenielewa!.

Pasco.​


 

Hapo kwenye red mkuu kidogo umeniacha, kwani tayari amemuowa?.

Nadhani ktk mambo yatakayomfanya asigombee moja ni hilo.
Kufika kukokotwa mahakamani kwa ajili ya mke wa mtu.
Jambo hilo limemharibia sana.


Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Nafanya tuu rejea ya haya niliopata kuyaandika!, nikujaribu kuunganisha na the dots kwa haya aliosema ZZK

Natumaini, wengi baada ya kuisoma hiyo barua ya ZZK, mnaweza kuwa na mchango tofauti na jinsi mlivyochangia mwanzo kwenye uzii huu!.
Pasco.
 
"If you cant convince them,Confuse them" by Adolf.A.Hitler
 
Pasco unamaanisha nin mkuu? "Sauti ya wengi ndio sauti ya mungu?
Mkuu Sixa, sio ""Sauti ya wengi ndio sauti ya mungu!" bali ""Sauti ya wengi ndio sauti ya Mungu!", na wengi hao huanzia wawili na kuendelea!.
Pasco
 
Nimekuwa nikifanya mapitio ya uzi huu, kuna mambo nimejifunza!.
Pasco.
 
Pasco kwa ufupi mada yako inaomesha hali halisi itavokua 2015. Yaani :
Chadema=wakristo
Cuf= waislamu
Ccm= wakristo + waislam

Ni wazi mshindi anajulika hivo wazo lako kwa chadema kumsimamisha Zitto ni stategy inayoweza kubadilisha fomula hio hapo juu. Hii ni kwa wale wenue kuona mbali na kufahamu siasa za ushindani na namna ya kujipatia ushindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…