Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?

Mkuu Mkandara, nikiwa mdogo, nilipenda sana kusikiliza michezo ya redio RTD enzi hizo, nikajisemea nitakuwa msanii!. Nikiwa sec pale Tambaza, nikaenda straight arts, kuna mwalimu mmoja wa pale family friend, akajo home kuripoti kwa wazee kijana anasoma fani za wajinga!, nikalazimishwa kusoma science ila nikasoma arts as option, nilipasua zote ila nika opt, arts na kutinga Ilboru, huko nilifanya mpaka drama performance!. Hivyo kiukweli mimi ni msanii kwa maneno na matendo na mara nyingi tuu hutoa comments kwa fasihi. Only wenye uelewa wa fasihi ndio wananielewa, na wasionielewa, tunakwenda nao hivyo hivyo!.

Hao jamaa ninaowafagilia, ni pace makers wetu kuelekea Magogoni 2015!. Ili ushinde kwa urahisi, lazima pace maker wako awe mzuri!.
 
Pasco,wakati bado tunasubiri video zaidi zenye kuonyesha wengine walichosema,hii iliyotolewa, inayomwonyesha Nassari makosa hadi sasa ni ya gazeti,Zitto kosa lake ni kuendeleza issue bungeni wakati ambao si sahihi.Pia kuonekana kama anashabikia,hilo limepelekea haya maneno ndani na nje ya chama chake...however hapo pa kushabikia makosa ni ya wote.
 

Duh! Kweli we nuksi
 
Mkuu Pasco, pamoja na kwamba mara nyingi unakuwa na habari zenye utata, wakati mwingine unakuwa objective sana.
Langu moja tu hapa la kuchangia. Kwakuwa unakiri kwamba ulizungumza na Dr. Slaa kuhusiana na mbio za uraisi 2015 na ilikuwa off records na wewe usingependa kutueleza kile alichokuambia, lakini kwa maelezo yako na ushauri wako ni kama vile umetuambia ulichokipata kwa Dr. Slaa.

Sasa basi ni vizuri ieleweke kwamba hakuna mtu anayemzuia zitto kugombea uraisi, kinachogomba hapa ni kwamba kila mara yeye tu ndiye anazungumzia kugombea uraisi, mbona wengine hawajitokezi hadaharani kutangaza nia ya "presidential hopeful?
Inawezekana wapo wengine ndani ya chadema ambao wana nia ya kuwania uraisi lakini wako kimya kwa ajili ya maslahi mapana ya chama chetu. Mbona hatumsikii Dr. Slaa ama Mbowe wakitangaza nia ya kuwania uraisi wazi wazi kama anavyofanya zitto?

Kwa namna yoyote ile huu si wakati muafaka wa kuzungumzia mambo ya uraisi, kwetu sisi chadema huu ni muda muafaka wa kujenga na kuimarisha chama. Ni muhimu sana zitto akautumia muda huu kuunga mkono operation Sangara pamoja na M4C ili utakapofika wakati wa kutafuta atakayebeba bendera ya chadema kwenye uchaguzi mkuu 2015, tuwe na base ya kutosha. Kama zitto ana nia ya dhati ya kutaka chadema ichukue uongozi wa nchi, na yeye ana nia ya dhati ya kuwa raisi wa nchi hii kupitia chadema, si vibaya aendeleze harakati zake kimya kimya, kwakuwa inawezekana kuna wengine wanaoutaka uraisi na wanafanya harakati kimya kimya bila kusababisha mizozo ndani ya chama.

Kwakuwa kila mara anapotangaza nia ya kuwania uraisi amekuwa akiibua sintofahamu ndani ya chama, ni vizuri atumie weledi wake, busara yake na uwezo wake kuhakikisha hakuna hizi unnecessary unrest ndani ya chama. Kila mmoja amekuwa akishuhudia vurumai zinazojitokeza kwa sababu ya zitto. Na ieleweke kwamba hakuna chuki katika hili isipokuwa sisi wengine tunachotaka na kuhimiza ni umoja na mshikamano miongoni mwetu ili tufanikishe malengo yetu ya kuchukua uongozi wa nchi 2015. Mimi naamini nafasi ya pekee ya chadema kuchukua uongozi wa nchi hii ni 2015 wala si vinginevyo, kwa kutumia katiba ya zamani ama mpya, huo ndio wakati wetu muafaka kushinda uchaguzi mkuu.
 
ungetwambia dr. slaa alikujibu vp? kama jibu unalo alafu utaki kusema ulichoandika hakina maana yeyote
 
ungetwambia dr. slaa alikujibu vp? kama jibu unalo alafu utaki kusema ulichoandika hakina maana yeyote
armanisankara, nakubaliana na wewe, nilichoandika hakina maana yoyote, na nachukua fursa hii kumshauri mode aifunge hii thread!.
 
Kwa yale ninayoyasoma humu JF, wewe Pasco ni pro-Zitto. Fair enough, naamini hiyo ni haki yako.
Nakuomba uwasiliane na Zitto atueleze sababu za kuungwa mkono na viongozi wa CCM ambao kwa hali na mali
hawatakubali kuachia madaraka katika jina la Demokrasia ya Kweli unayoiamini.
Zitto kupewa Uenyekiti wa Kamati ya Bunge!

Zitto kupew posho ya safari za nje kwa kuingia kwenye msafara wa JK!
Zitto kuwa kipenzi cha Jack Zotta!

Zitto kutofunguliwa kesi na Jeshi la Polisi kama wenzake!
Na sasa Zitto kuwa kipenzi cha gazeti la Uhuru!

Tunajua kuna utata wa Uraia kwa watu kadhaa wa Kigoma,
na hili Zitto alilisemea vizuri wakati wa majadiliano ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Je, utata wa Uraia unamkumba pia yeye mwenyewe binafsi?
 
Pasco umeongea vitu vya maana sana umewaonyesha cdm ushindi uko wapi na vp wauchukue tatizo la cdm akitajwa Zitto tu basi wengi wanakasrika na hawataki kusikiliza chochote, lakini nawaambia CDM bila Zitto 2015 uraisi msitegemee Dk Slaa ameshakataliwa 2010 na tutamkataa tena 2015.
 
Last edited by a moderator:
Teh teh! unaongea vitu vya kipumbaavu mwenywe unaviona ndio hoja halafu unataka watu wajadili upumbavu huo! soma vizuri hoja za Pasco halafu zijibu kama unaupeo wakuchambua hoja, chuki zisikutoe akili
 
Nilikuwa Dodoma na niliongea na ZZK, ili haya sikumuuliza!. Nikimuona tena, nitamuuliza.
 
Pasco ni CCM damu...na pia ni muumini mzuri wa dini ya Edward Lowassa...anafahamu pia CDM ni chama makini.
Kama kweli Pasco si mwanachama, mshabiki au mkereketwa wa chama chochote cha siasa, kwanini azungumzie mambo ya siasa kwa kumfagilia Kabwe, Zitto Zuberi na Lowasa, Ngoyai Edward?

Pasco acha unafiki...be straight!!!
 
Kengemumaji una udini wa fikra, mtazamo dhaifu usio tija.
 

Herald Hunter, haya bwana, mimi ni CCM damu!, na namfagilia ZZK ili kuwaingiza chaka, mgombea wangu EL apete kwa urahisi!.
 
Ushindi mkubwa wa wabunge wa CDM ulichangiwa na ccm kuweka wasiokubalika na wana CCM wakawapigia wa cdm, hilo kama kuna mtu halijui basi asijiite anajua lolote la inji hii, huyu jamaa naona anatumia fasihi yake kulielewesha lkn watu wanaanza kumshambulia personally. Zito kuna wana CDM hawamtaki, still kuna wana CCM wanampenda, Slaa anapendwa na baadhi wa CDM na wengine hawampendi, sasa basi, chukua( Slaa = CDM+ CCM na Zito= CDM + CCM) + cuf na wasio na vyama nani ataweza kuwa nazo nyingi achukue nchi? Usisahau, ccm wao wanahitaji TU candidate mzuri wanachukua nchi sbb wana base kubwa ya wanachama hai na wapenzi hai
 
 
chadema kuongelea suala la nani awe rais ni mapema sana kwani kwa sasa wako ktk kuimarisha chama na Zitto anatakiwa naye kufanya kazi hiyo then chama kikiwa imara na kutambulika ndipo alete hoja yake kugombea urais but for now is too earlier kwa zitto kuwa rais na hata asihangaike kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo
 
Ingekuwa kumchagua mwenyekiti wa Chadema naunga mkono kabisa kwamba vikao vya ndani vingetumika, lakini atakayechaguliwa ni rais wa Wa Tz, hata mm nisiye na Chama nataka nimjue kati ya wagombea wote nani anastahili kutuvusha ktk huu msitu. Hebu kumbuka maneno ya Julius nyerere pale Mbeya wkt wa Mei Mosi 2005. TUNAMTAKA RAIS WA NCHI NA SIO M/KITI WA CHAMA. Fanyeni siri mtashangaa kumekucha mpige kelele tumeibiwa. Dr Slaa angetangazwa mapema 2010 leo hii CDM mngekuwa magogoni.Take my word sir i salute you!
 
Zito hatakaa awe Rais wa nchi hii hatoshi kabisa na msifikirie ule mpango wa kujaribu jaribu Urais utatokea tena saiv tunataka mtu smart na msafi pia mzalendo..Zitto hana hayo yote na pia haaminiki....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…