Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Kibuli cha mr. Solex kinakuja kumtokea puani, amekuta maisha yanaendelea atambue lazima akitaka kubadirisha maisha ya watu, hawezi simamisha maisha completely ili aanze mwanzo, hapo kwenye mahesabu tunafanya kitu kinaitea intersection lazima kuwepo na kitu tunasema (free zone.

Sasa yeye asitake kuangalia kila kitu na kutembea kigazani sababu tu kavaa bodyguard.
 

Miss Kyenda, ni wanadamu wachache sana wanaokubali mabadiliko, haijalishi mabadiliko gani, ya aina yoyote ile..
Lakini pia ukiangalia katika mapinduzi ya jambo lolote lile duniani ni lazima pawepo na “sacrifice”. Ukiangalia historia ya mambo duniani, hakuna ukombozi uliowahi kutokea pasi na kuwa na wahanga.
JPM anaonekana ni mwiba mchungu, lakini ipo siku atafananishwa na lile jiwe kuu la pembeni walilolikataa waashi.
Nasema haya kwa maana kwamba Watanzania kama tunataka mabadiliko na kufikia maendeleo ya kweli, hatuna budi kukubali baadhi yetu kama sio wote kuwa sadaka kwa manufaa ya kizazi kijacho.
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea hapa duniani bila ya kuwepo wahanga, watu waliopambana na hata kufa kwa ajili ya ukombozi wa nchi zao( haijalishi iwe ni kwa njia ya vita ama amani)
Mimi naichukulia hali hii tunayopitia kama taifa kuwa ndio “sacrifice” yetu kwa ajili ya mustakabali mwema wa Taifa hili. Naikumbuka historia ya safari ya wana Israel jangwani kuelekea nchi ya ahadi, mapinduzi ya viwanda Ulaya na Marekani kuelekea maendeleo, China na Asia katika ujenzi wa nchi zao, n.k. Ni safari zilizokuwa na taabu na machungu mengi lakini mwisho wa siku walizifikia ahadi na ndoto zao. Na hata sasa vizazi vyao vinakula mema ya nchi zao lakini vinawakumbuka majemedari hao walioumia/kufa kwa ajili ya kizazi kilichopo.
Watanzania tukubali tu, hatuwezi (kama kweli tunataka maendeleo) kuyafikia pasipo kuwa na watu watakaojitoa na hata kufa kwa ajili ya wengine.
Mimi ni mtumishi wa serikali na hata hili la 25% linanigusa na kuniumiza lakini najifariji kwamba hii ndio sacrifice yenyewe ili watoto na wajukuu zangu waje waikute Tanzania ya maziwa na asali huko siku za usoni.
Lakini pia hata maandiko yanatuambia kuwa safari ya mbinguni sio nyepesi, ni yenye tabu na mapito magumu na kwamba watakaostahimili mpaka mwisho ndio watavikwa taji ya uzima.
 
Hapo ndipo ataharibu kila kitu ujue sophia simba yupo kimya umewahi kujiuliza? Kuna bomu huko linakuja
Usitishe watu, Sophia hana lolote tena kamalizwa kisiasa ni vile alikuwa anaandika barua mia kwa mwaka kuomba asamehewe arudishwe chamani.
 
Usitishe watu, Sophia hana lolote tena kamalizwa kisiasa ni vile alikuwa anaandika barua mia kwa mwaka kuomba asamehewe arudishwe chamani.
Unajidanyanya mzee kuandika barua kurudishwa chamani kunaweza kuwa ni mtego sophia hajaisha kisiasa kakaa kimya hapend usumbuf wa mapema kama wakina membe kwa hiyo nae kinana kamalizwa kisiasa au nape?
 
Mafisadi au wanufaikaji wa kazi za mafisadi utawajua tu mwandiko wao.
 
Dkt.Membe atarudisha utawala wa sheria na demokrasia.Atarudishwa uhuru wa habari.Ataacha mihimili ya dola ifanye kazi bila kuingiliana.Ataondoa siasa za upendeleo kwa watu wachache.Na pia ata boresha maslahi na mafao ya wafanya kazi wa umma.
 
Mkuu, unachokisema kwa kiasi kikubwa ni sahihi. Katika mabadiliko lazima patokee wahanga, machungu na bei ili kuyafanikisha. Wapo watakaoumia na wapo watakaonufaika. Ila kikubwa ni kuangalia gharama dhidi ya faida za mabadiliko tajwa.

Tuna misingi yetu kama nchi ambayo tumejiwekea na bila shaka tunapaswa kuiimarisha. Umoja, amani na mshikamano. Tujipime kama misingi hii inaimarika au kobomoka kuendana na mabadiliko.
 


Rangi ya picha imejibu maswali yote
 
Dkt.Membe atarudisha utawala wa sheria na demokrasia.Atarudishwa uhuru wa habari.Ataacha mihimili ya dola ifanye kazi bila kuingiliana.Ataondoa siasa za upendeleo kwa watu wachache.Na pia ata boresha maslahi na mafao ya wafanya kazi wa umma.
Mmh ok sawa [emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]
 
Binadamu wa ajabu na mpotoshaji uliyetukuka. 25% ya pensheni na zilizobaki zinakwenda kununua wabunge na madiwani wa upinzani ili waunge mkono juhudi? Hivi mtu ukifanya kazi nzuri hata isipoungwa mkono haitaonekana? Mwanafunzi anafanya vizuri darasani lakini wanafunzi wenzake wanamchukia, itamzuia kufaulu?
 
2020 JPM atavunja rekodi atashinda kwa 98%.
Tusubirie tukutane 2020, kwa sasa tusipoteze muda na nguvu zetu kulumbana , tuchape kazi kwa maendeleo yetu na taifa
 
Mafisadi au wanufaikaji wa kazi za mafisadi utawajua tu mwandiko wao.
Hii lugha ya kijuha ndo inanishinda kuelewa inamsaidiaje huyo mkuu wenu wa malaika!! Kila anayekosoa utendaji mbovu na wa kutafuta sifa binafsi wa bosi wenu mnambatiza alikuwa anafaidi ufisadi, mbona mnaounga mkono ndo wengi mlikuwa mnafaidi ufisadi? Chenge anampinga malaika? Ndugai anampinga malaika? Asas anampinga malaika?
 
Usipende kukariri, si wote tunaongozwa na subconscious..!
Muda ndio huleta majibu sahihi.
Tutajua kipi ndio sivyo na kipi ndivyo hivyo.

Nani alikuwa anaongozwa na subconcious mind au nani alikuwa ana insight kubwa ambayo inakuja kuwa reality in future.
Kuamini maisha bila njia za kifisadi na wizi haiwezekani nako ni kufikiri mambo kwa kutumia subconcious mind kama vile ulivyo aminishwa na mafisadi na wanaotaka jamii(nchi) yenu ibaki maskini huku wewe ukionjeshwa raha kidogo na mamilioni wakiangamia.
 
Aliyepo hatumtaki, mnayemtaja hatumwamini. Tuleteeni jina lingine tafadhali...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…