Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Binadamu wa ajabu na mpotoshaji uliyetukuka. 25% ya pensheni na zilizobaki zinakwenda kununua wabunge na madiwani wa upinzani ili waunge mkono juhudi? Hivi mtu ukifanya kazi nzuri hata isipoungwa mkono haitaonekana? Mwanafunzi anafanya vizuri darasani lakini wanafunzi wenzake wanamchukia, itamzuia kufaulu?

Sawa mimi mpotishaji ila wewe ndiye mkweli ambaye unafanya kazi ktk moja ya mashirika ya pensheni hivyo unaona jinsi serikali inavyochukua hela kwenda wanunua wabunge na madiwani.
Ila kubali ukatae, bila sacrifice of any magnitude whether peaceful or hostile, hutokaa uone maendeleo.
Tuliza ubongo chini, fuatilia mambo duniani halafu fikiri pia uone kama hao wote unaowajua wameendelea kama walilala na kuamka matajiri. Ukiyang’amua hayo naamini utarudi hapa ili tujadiliane kwa kufikiri
 
Mkuu Mshana Jr kwa jinsi nchi ilivyo sasa ni heri tukarudi tu Misri hata kama Membe anaonekana anamguu mdogo kuliko viatu vyetu, yaani kama tu vile Mkwere alipofanya ile potelea mbali liwalo na liwe na kuamua kumzawadia KITI bwana Jiwe kuliko Mamvi basi na sisi wengine tunasema potelea mbali liwalo na liwe Membe atatutoa porini.

Ila tuwe makini tunaenda kwenye uchaguzi mgumu labda kuliko hata ule wa 2015, watu wengi sana watapoteza maisha maana kumbuka haiba ya weji na DAB ilivyo, ni watu ambao wanaamini zaidi ktk kupoteza na kufuta kabisa.

Mungu atutangulie.
Itategemea na mtazamo wa wabangua korosho je watakubali kutumika au wataheshimu mikataba ya viapo vyao
 
Naamini hili no wazo zuri si kwa Membe tu Bali kwa yeyote atakaefanikiwa kuchaguliwa kuwa rais wa jmt!..
 
Roho yangu inaniambia, Novemba 2020 tunamwapisha Cammilius kuwa raisi hapo uwanja wa Taifa Dar es salaam.

Iwapo hili litakuwa naamini haya ndiyo mambo kumi na sita ya awali kabisa ambayo rais Membe atatakiwa kufanya ndani ya siku 100 za kukaa ofisini

1. Kuhuisha mchakato wa katiba mpya, Watanzania tunataka katiba mpya, iliyobora, yenye kuchukua mengi ya rasimu ya Jaji Warioba. Bila Katiba mpya nzuri tutaendelea kupiga mark time bila kusogea kama Taifa.

2. Kurekebisha sheria ya Habari na Makosa ya mitandao, hakuna taifa linaloweza kuendelea kwa kulimit uhuru wa watu wake kutafuta na kupashana habari, hata hiyo China wanayoitolea mfano, ni baada ya kiongozi shupavu Deng Xiaoping kuifungua China iliyokuwa imefungwa na sera za Mao ndo wachina wakaanza kuerevuka na kuona ulimwengu hasa wa west unaendaje na hivyo na wao kusonga mbele

3. Kuhakikisha ndani ya siku 100 kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, itakayohusisha vyama vyote, hili likiwa ni kuliponya Taifa lililogawanyika kutokana na sera za kibabe za utawala uliomtangulia

4. Kuomba msamaha kwa niaba ya serikali wale wote waliovunjiwa nyumba, waliobambikiziwa kesi, juu ya waliopotea na kuhakikisha anatangaza Fidia kwa wale wote waliokumbwa na kadhia hii, na kuahidi kuwa havitatokea tena

5. Kutangaza kuwa serikali haitaingilia wakulima kwenye kujitafutia soko bora la mazao yao, na kwamba serikali itakuwa tayari kutumia ofisi zake za kibalozi duniani kote kuwatafutia masoko Wakulima kama amvavyo Kassim Majaliwa alifanikiwa kuwatafutia wakulima wa Korosho masoko, lakini wazo lake hilo likakataliwa dakika ya mwisho na bosi wake mbele ya Kadamnasi

6. Kurekebisha sheria ya takwimu, kuondoa vikwazo vya kufanya tafiti na kuirudisha Tanzania kwenye mikataba ya kuendesha nchi kwa uwazi

7. Kutangaza mara moja kuuza ndege zote zilizonunuliwa katika utawala huu, na badala yake kupeleka pesa kwenye kutengeneza Liganga na mchuchuma ili kiwanda hicho kitoe chuma kitakachojenga SGR badala ya kutumia mamilioni ya Dola kuagiza chuma kutoka nje

8. Pamoja na kwamba kutakuwa na serikali ya umoja wa Kitaifa, atangaze kuheshimu demokrasia, uhuru wa mawazo, kukosoa na kukosolewa.

9. Atangaze vita kali dhidi ya ufisadi, aanzishe mchakato wa kuwafikisha wote mahakamani mafisadi, Siyo apige kelele za kupambana na ufisadi majukwaani, bali atende, tuone ufisadi ukipigwa vita kwelikweli bila kuonea mtu

10. Atangaze kulipa malimbikizo yote ya wafanyakazi, kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa sheria za utumishi, sheria hii ya mafao ya 25% iondoke , watoto wenye mimba waruhusiwe kuendelea na masomo.

11. Kwa Msamaha wa Rais, aamuru wale wote walioondolewa kazini kwa vyeti feki lakini umri wa kukaribia kustaafu umewakuta karibia na kustaafu, basi kwa kuwa wamelitumikia Taifa kwa muda mrefu, tusibeze mchango wao, wapewe stahiki zao!

12. Siku ya kwanza kabisa ofisini autangazie umma kuwa anataka kuona bunge lenye meno makali, lililo live!

13. Atangaze uchunguzi wa Shambulio la Lissu, uchunguzi wa kupotea kwa Ben Saanane, Azory, Kanguye na yeyote yule ambaye hatumjui

14. Kufumuafumua serikali za mitaa, kuondoa ambao siyo wataalamu na kuweka wataalam na Kuzirejeshea Halmashauri nguvu za Kukusanya ushuru kwenye maeneo yao, hususan Ushuru wa mabango etc.

15. Kuunda Serikali yenye sura ya Kitaifa, Serikali yenye uwakilishi wenye sura ya Kitaifa ( Siyo proportionally unateua Waislamu wengi mpaka Wakiristo wanashtuka kulikoni, Au proportionally unateua Wakiristo wengi mpaka waislamu wanaona hapa kuna udini wa wazi, kitu ambacho hakiwakilishi demographic composition ya kitaifa, Au unateua watu wa Kanda ya Kusini wengi mpaka watu wa Ksnda nyingine wanahisi kuna Ukanda hapa). Harmony katika nchi ni muhimu, na lazima serikali iwe na sura ya KITAIFA

16. Kuhuisha Maridhiano huko Zanzibar!

Cammilius uwezo wa kuwa Rais unao, Sababu ya kuwa raisi unayo, na najua nia ya kuwa raisi unayo, HEBU FANYA KWELI BASI!!!

N.B
Katiba inaniruhusu kutoa maoni, na kuwa na mawazo ya kutaka kuona nchi yangu inakuwaje na inaongozwaje, Siyo Uhaini kutaka kumuona mtu fulani anakuwa rais!. HAKI YANGU YA KIKATIBA IHESHIMIWE!
UKO SAHIHI KABISA ILA SIYO KWA MEMBE TU KWA YOYOTE ATAKACHUKUA NCHI 2020!!!!
NAJUA JIWE ANASOMA HUU UZI KAMA VIPI ABADILI GIA ANGANI!!!!!
 
Now days we're going crazy....Hali ni mbaya mpaka tumebaki kujifariji na ndoto
 
Naona wanajitekenya na kucheka wenyewe, ndio raha ya ujinga.
 
Wapinzani,jikiteni kwenye issue za maana kama 25% ya mafao ,Madawa hospitalini,Ajira na maisha duni ya raia wa vijijini,Issue za Membe kugombea Uraisi,sijui maandamano,mtapata kura na Waandamaji wa kimjinimjini kama wa humu JF, afu mwisho wa siku mseme tulishinda kura milioni sijui ngapi,ohh tulifanya polisi wakaandamana,acheni kuwaza maslahi yenu binafsi la sivyo mkiwa na bahati magogoni mtaishia kupiga picha tu.


Huo ndio uboya na siasa za matukio.
Vyama mbadala haviwezi kuongeza lolote kwa kukomaa na hilo kwani kura za watumishi huwa wanazo tangia hapo. Chunguza vizuri,watumishi wengi wa umma hawapigii chama tawala.
Kuna kundu kubwa la wakuda wa mjini/ masela na makachaa Ambao huwa hawapi kura- hilo ndio eneo potential la vyama mbadala kuinvest nguvu na mbinu zao kuwafanya wapige kura regadless wabampigia nani?.
 
2020 JPM atavunja rekodi atashinda kwa 98%.
Tusubirie tukutane 2020, kwa sasa tusipoteze muda na nguvu zetu kulumbana , tuchape kazi kwa maendeleo yetu na taifa


Ongelea mengine lakini Magufuli hawezi siasa za ushindani na hiyo 2020 kitakachofanyika sio uchaguzi bali ni kupoteza pesa za wananchi ili Magufuli na genge lake watangazwe washindi.
 
Hakuna watu WAPUMBAVU kama % fulani ya wabongo, yani mmekaa wanaume na map.umbu yenu kusapotiana vitu vya kusadikika?,Kama Lowassa alichemsha na kubaki kuwa raisi wa mitandaoni huyo Membe sio 2020 tu hata 2025 hawezi kuwa kiongozi wa nchi hii.Sana Sana mnamtafutia matatizo naye apigwe Parkinson Disease aanze kutetemeka tu.Tatizo ni pale mnapo undersetimate Serikali ya Tanzania, achana nayo kabisa msiichukulie kama Jamii Forums ambapo mtu anaota ndoto mchana anaamka anaileta humu na waotaji wenzake Kama yeye wanampa likes.
Wengi wana undermine serikali wanafikiri ni Rais kukalia kiti kile, sio rahisi hivyo kama wanajidanganya, lakini serikali hii inafanya kazi nzuri sana ni ngumu kuwabadili watu wanaopenda maisha rahisi na kuongea ongea sana badala ya kyfanya kazi.
 
Wakuu kwa jinsi nilivyosikia mkakati uliopangwa wa kumng'oa Jiwe madarakani.

Nimeamini 2020 Membe ndio Rais,hakuna namna.

Na hata wakimuua bado kuna mbadala wake wapo wawili .

Yani kumbe ni serious,Jiwe lazima ang'oke 2020
 
Kumbe bado wapo watanzania wenzangu wenye mawazo chanya kama haya! Nilidhani hatuzidi 1000 tunaofikiri kama we we.

Kibaya zaidi hata wale wanao jiita Great Thinkers wengi wameingia mtego wa mafisadi uchwara wa CCM na upinzani wanaotaka aondoshwe Magufuli awekwe mtu atakae waacha wafilisi nchi kama enzi za JK.
Nchi hii tangu uhuru imefilisiwa na makundi mawili... kundi la wafanyabiashara ambao miongoni mwao sio Watanzania na kundi la Wanasiasa wazito ambao karibu wote ni Watanzania wenzetu!! Majizi haya kutoka kundi la wanasiasa walifanya ufedhuli huu wakati wanafahamu fika Watanzania tuliwapa kazi ya kulinda maslahi yetu!

Nitajie jizi moja tu kutoka kwenye kundi la hawa wanasiasa wezi na mafisadi ambae amefanywa chochote na huyo Magufuli wenu mnayetaka kutudanganya kwamba anapambana na mafisadi... ONLY ONE!
 
Back
Top Bottom