Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Nchi hii tangu uhuru imefilisiwa na makundi mawili... kundi la wafanyabiashara ambao miongoni mwao sio Watanzania na kundi la Wanasiasa wazito ambao karibu wote ni Watanzania wenzetu!! Majizi haya kutoka kundi la wanasiasa walifanya ufedhuli huu wakati wanafahamu fika Watanzania tuliwapa kazi ya kulinda maslahi yetu!

Nitajie jizi moja tu kutoka kwenye kundi la hawa wanasiasa wezi na mafisadi ambae amefanywa chochote na huyo Magufuli wenu mnayetaka kutudanganya kwamba anapambana na mafisadi... ONLY ONE!
Ni kweli hajawagusa wanasiasa wenzie wanao husishwa na ufisadi au ubadhirifu wa mali za umma. Lakini naona juhudi za kuzuia wasitokee wanasiasa wengine wengi watakao fanya ufisadi uliokufuru bila woga kama awamu zilizopita.

Angalau yeye ana anzia hapa ingawa siso tunapenda angelianzia na wa awamu zile kuwawajibisha kisheria.
 
Utaratibu huo ulikuwepo hata kwa awamu zilizopita sema umesahau, mfano mbatia aliteuluwa kuwa mbunge na JK
Hawa ni watu wa ajabu sana.Yani wao wanaamini kila kinachotokea leo ni kipya
 
Ulikuwa miongoni mwa wajenga hoja humu JF lakini siku za karibuni uwezo wako umeshuka sana labda kwa vile uwezo wa ccm kujenga hoja pia umeshuka hivyo timu nzima kiwango kimeporomoka hakuna wa kumwinua mwenzake. Unaposema hakuna wa kumsumbua JPM kwa sasa wakati tetesi tu za kujitokeza kwa Membe zimemuibua Katibu mkuu wa CCM utabaki unachekesha walionuna. Kwa taarifa yako JPM anasimbuka tena anasumbuka si kidogo, na hapa BM hajatoa tamko rasmi na udikteta wa siasa za majukwaani bado unaendelea subiri zifumuke utajificha chooni.
Hapo mwisho umesema labda Mungu atende yake kuhusu JPM, nadhani ulimaanisha Mungu amchukue mja wake. Kwa taarifa yako na hili liko wazi tangu tupate Uhuru huyu ni Rais wa kwanza wa JMT kuombewa na wananchi wake ni "bora afe tuchague mwingine". Kiongozi mwingine aliyewahi kuombewa hivyo ni Rais wa Zanzibar kipindi hicho mzee KOMANDO Salmini Amour. Kama hali imefika hapo kwa huyo uliza hali ilikuwaje Zanzibar wakati wa Komando hadi ukafikia wananchi kuchukia uhai wa kiongozi wao?
Hao wananchi wanaosema bora afe si ndio haohao bavicha?Hizi siasa za kuombea mabaya zimeanza toka 2015.Kumbuka kifo cha Celine kolimba wapinzani walifurah sana, akaja nape kupata ajali wapinzani waliomba kwanini hajafa. So unachokiona kwa bavicha kuombea jpm afe sio kigeni hata kidogo labda kama siasa umeanza leo
 
Kwani Jk wakat anamteua mbatia uvccm waliisha?
Nyie vichwani sijui mnatatizo gani mwenzio kashindwa kujibu wewe ndo upo chaka balaa
IMG_20181202_132350.jpeg
 
Kwa hiyo hapo nape anamwambia membe asiharibu kuzima taa maana ukumbini wako wote wanaweza kupigana kumbo wakitoka nje
 
Dah shida ya Serengeti huwa na misimamo yao waliyokarrshwa tayar. Unaulizwa huko uvccm waliisha watu hata akateuliwa mbatia wa nccr?
Wewe sijui unaelewa au umechanganyikiwa hao wakina waitara wameteuliwa na magufuli? Je wamebaki kuwa wabunge wa chadema au wa ccm? Walikuwa raia wa kawaida au wamejivua nyadhifa zao

Serengeti wanakuja huko wanakuwa viongozi wako wakina katambi,gekul na waitara magufuli anawanyoosha sana mnawaita nyumbu wakija huko mabosi wenu.
 
Nakumbuka mshana alishawahi kutangaza kuhama jukwaa la siasa,nashangaa kuona leo yupo jukwaani,ni lini alibatilisha uamuzi wake?
 
Miss Kyenda, ni wanadamu wachache sana wanaokubali mabadiliko, haijalishi mabadiliko gani, ya aina yoyote ile..
Lakini pia ukiangalia katika mapinduzi ya jambo lolote lile duniani ni lazima pawepo na “sacrifice”. Ukiangalia historia ya mambo duniani, hakuna ukombozi uliowahi kutokea pasi na kuwa na wahanga.
JPM anaonekana ni mwiba mchungu, lakini ipo siku atafananishwa na lile jiwe kuu la pembeni walilolikataa waashi.
Nasema haya kwa maana kwamba Watanzania kama tunataka mabadiliko na kufikia maendeleo ya kweli, hatuna budi kukubali baadhi yetu kama sio wote kuwa sadaka kwa manufaa ya kizazi kijacho.
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea hapa duniani bila ya kuwepo wahanga, watu waliopambana na hata kufa kwa ajili ya ukombozi wa nchi zao( haijalishi iwe ni kwa njia ya vita ama amani)
Mimi naichukulia hali hii tunayopitia kama taifa kuwa ndio “sacrifice” yetu kwa ajili ya mustakabali mwema wa Taifa hili. Naikumbuka historia ya safari ya wana Israel jangwani kuelekea nchi ya ahadi, mapinduzi ya viwanda Ulaya na Marekani kuelekea maendeleo, China na Asia katika ujenzi wa nchi zao, n.k. Ni safari zilizokuwa na taabu na machungu mengi lakini mwisho wa siku walizifikia ahadi na ndoto zao. Na hata sasa vizazi vyao vinakula mema ya nchi zao lakini vinawakumbuka majemedari hao walioumia/kufa kwa ajili ya kizazi kilichopo.
Watanzania tukubali tu, hatuwezi (kama kweli tunataka maendeleo) kuyafikia pasipo kuwa na watu watakaojitoa na hata kufa kwa ajili ya wengine.
Mimi ni mtumishi wa serikali na hata hili la 25% linanigusa na kuniumiza lakini najifariji kwamba hii ndio sacrifice yenyewe ili watoto na wajukuu zangu waje waikute Tanzania ya maziwa na asali huko siku za usoni.
Lakini pia hata maandiko yanatuambia kuwa safari ya mbinguni sio nyepesi, ni yenye tabu na mapito magumu na kwamba watakaostahimili mpaka mwisho ndio watavikwa taji ya uzima.
Unafanya mabadiliko ndani ya familia, unaanza kufukuza mke, unaua watoto, unauza nyumba, hufai kuwa baba,

soma ulichoandika alafu fikirisha ubongo wako utaelewa namaanisha nini
 
Unafanya mabadiliko ndani ya familia, unaanza kufukuza mke, unaua watoto, unauza nyumba, hufai kuwa baba,

soma ulichoandika alafu fikirisha ubongo wako utaelewa namaanisha nini

Hekima mpe mwenye hekima ili azidi kuwa na hekima
 
Kila kete itatumiwa kwa asilimia mia moja
By far the top guy has been one step ahead of so many who underrated him.
In this game jasusi will lose....hivi hatukushangaa RA kuja baada ya muda mrefu? There was a reason....and RA still is the man who could organize those sort of moves.
Kitu ambacho mchaga ameshindwa....sidhani kama kule kwetu umakondeni kitafanyika
 
Mkuu Mshana Jr kwa jinsi nchi ilivyo sasa ni heri tukarudi tu Misri hata kama Membe anaonekana anamguu mdogo kuliko viatu vyetu, yaani kama tu vile Mkwere alipofanya ile potelea mbali liwalo na liwe na kuamua kumzawadia KITI bwana Jiwe kuliko Mamvi basi na sisi wengine tunasema potelea mbali liwalo na liwe Membe atatutoa porini.

Ila tuwe makini tunaenda kwenye uchaguzi mgumu labda kuliko hata ule wa 2015, watu wengi sana watapoteza maisha maana kumbuka haiba ya weji na DAB ilivyo, ni watu ambao wanaamini zaidi ktk kupoteza na kufuta kabisa.

Mungu atutangulie.
Nenda peke yako huko Misri...ila ujue hutaweza kubadilisha mwendo maana wale waliobisha Ile safari waliishia jangwani....hawakurudi Misri na wala hawakufika Caanan
 
Back
Top Bottom