Roho yangu inaniambia, Novemba 2020 tunamwapisha Cammilius kuwa raisi hapo uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Iwapo hili litakuwa naamini haya ndiyo mambo kumi na sita ya awali kabisa ambayo rais Membe atatakiwa kufanya ndani ya siku 100 za kukaa ofisini
1. Kuhuisha mchakato wa katiba mpya, Watanzania tunataka katiba mpya, iliyobora, yenye kuchukua mengi ya rasimu ya Jaji Warioba. Bila Katiba mpya nzuri tutaendelea kupiga mark time bila kusogea kama Taifa.
2. Kurekebisha sheria ya Habari na Makosa ya mitandao, hakuna taifa linaloweza kuendelea kwa kulimit uhuru wa watu wake kutafuta na kupashana habari, hata hiyo China wanayoitolea mfano, ni baada ya kiongozi shupavu Deng Xiaoping kuifungua China iliyokuwa imefungwa na sera za Mao ndo wachina wakaanza kuerevuka na kuona ulimwengu hasa wa west unaendaje na hivyo na wao kusonga mbele
3. Kuhakikisha ndani ya siku 100 kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, itakayohusisha vyama vyote, hili likiwa ni kuliponya Taifa lililogawanyika kutokana na sera za kibabe za utawala uliomtangulia
4. Kuomba msamaha kwa niaba ya serikali wale wote waliovunjiwa nyumba, waliobambikiziwa kesi, juu ya waliopotea na kuhakikisha anatangaza Fidia kwa wale wote waliokumbwa na kadhia hii, na kuahidi kuwa havitatokea tena
5. Kutangaza kuwa serikali haitaingilia wakulima kwenye kujitafutia soko bora la mazao yao, na kwamba serikali itakuwa tayari kutumia ofisi zake za kibalozi duniani kote kuwatafutia masoko Wakulima kama amvavyo Kassim Majaliwa alifanikiwa kuwatafutia wakulima wa Korosho masoko, lakini wazo lake hilo likakataliwa dakika ya mwisho na bosi wake mbele ya Kadamnasi
6. Kurekebisha sheria ya takwimu, kuondoa vikwazo vya kufanya tafiti na kuirudisha Tanzania kwenye mikataba ya kuendesha nchi kwa uwazi
7. Kutangaza mara moja kuuza ndege zote zilizonunuliwa katika utawala huu, na badala yake kupeleka pesa kwenye kutengeneza Liganga na mchuchuma ili kiwanda hicho kitoe chuma kitakachojenga SGR badala ya kutumia mamilioni ya Dola kuagiza chuma kutoka nje
8. Pamoja na kwamba kutakuwa na serikali ya umoja wa Kitaifa, atangaze kuheshimu demokrasia, uhuru wa mawazo, kukosoa na kukosolewa.
9. Atangaze vita kali dhidi ya ufisadi, aanzishe mchakato wa kuwafikisha wote mahakamani mafisadi, Siyo apige kelele za kupambana na ufisadi majukwaani, bali atende, tuone ufisadi ukipigwa vita kwelikweli bila kuonea mtu
10. Atangaze kulipa malimbikizo yote ya wafanyakazi, kuwapandisha madaraja kwa mujibu wa sheria za utumishi, sheria hii ya mafao ya 25% iondoke , watoto wenye mimba waruhusiwe kuendelea na masomo.
11. Kwa Msamaha wa Rais, aamuru wale wote walioondolewa kazini kwa vyeti feki lakini umri wa kukaribia kustaafu umewakuta karibia na kustaafu, basi kwa kuwa wamelitumikia Taifa kwa muda mrefu, tusibeze mchango wao, wapewe stahiki zao!
12. Siku ya kwanza kabisa ofisini autangazie umma kuwa anataka kuona bunge lenye meno makali, lililo live!
13. Atangaze uchunguzi wa Shambulio la Lissu, uchunguzi wa kupotea kwa Ben Saanane, Azory, Kanguye na yeyote yule ambaye hatumjui
14. Kufumuafumua serikali za mitaa, kuondoa ambao siyo wataalamu na kuweka wataalam na Kuzirejeshea Halmashauri nguvu za Kukusanya ushuru kwenye maeneo yao, hususan Ushuru wa mabango etc.
15. Kuunda Serikali yenye sura ya Kitaifa, Serikali yenye uwakilishi wenye sura ya Kitaifa ( Siyo proportionally unateua Waislamu wengi mpaka Wakiristo wanashtuka kulikoni, Au proportionally unateua Wakiristo wengi mpaka waislamu wanaona hapa kuna udini wa wazi, kitu ambacho hakiwakilishi demographic composition ya kitaifa, Au unateua watu wa Kanda ya Kusini wengi mpaka watu wa Ksnda nyingine wanahisi kuna Ukanda hapa). Harmony katika nchi ni muhimu, na lazima serikali iwe na sura ya KITAIFA
16. Kuhuisha Maridhiano huko Zanzibar!
Cammilius uwezo wa kuwa Rais unao, Sababu ya kuwa raisi unayo, na najua nia ya kuwa raisi unayo, HEBU FANYA KWELI BASI!!!
N.B
Katiba inaniruhusu kutoa maoni, na kuwa na mawazo ya kutaka kuona nchi yangu inakuwaje na inaongozwaje, Siyo Uhaini kutaka kumuona mtu fulani anakuwa rais!. HAKI YANGU YA KIKATIBA IHESHIMIWE!