Kwenye medani ya soka Tanzania, kuna taasisi kubwa 2 na Imara - Yanga SC na Simba SC..
Hata uwatengeneze akina Azam na misuli yao ya kiuchumi, bado IMANI ya wapenda soka nchini ni Yanga na Simba - kama mchezaji hujafikia kiwango cha kucheza mle basi CV yako kama mwanasoka is questionable; ni hivyo hivyo kwa wanataaluma - kama hujaweza kusoma course yoyote UDSM pamoja na ujingaujinga wao wa siku hizi basi you haven't lived your scholarly life to the fullest..
Sasa najiuliza, hizi timu Membe na timu Lowassa ndani ya CCM ni TAASISI kamili sasa? Ni DINI kamili? Maana piga ua garagaza ukiwa mwanaccm lazima uangukie kwenye Timu hizi mbili ili udumu katika Siasa. Hata mwenyeketi mwenyewe tunamwona hatua kwa hatua sasa anajitambulisha na TIMU mojawapo, huku akituma vijana wake kuishambulia na kuididimiza TIMU nyingine... Mwenyekiti alianza kum-court Lowassa na sasa anakula na kuwastarehesha wanataasisi muhimu wa Timu Lowassa - the Mwang'ondas and the Rostams..
These two guys must be pretty SMART therefore - Lowassa na Membe, badala ya kupambana nao kwa ngumi na mitutu heri wangewatambua tu hata kuziita kumbi za Mikutano Lumumba na Kizota kwa majina yao - labda hata yule mwenye nia ya kuliviringisha Jiwe(Mzigo wa dhambi ya mauti) kutoka kwenye mlango wa Ikulu angetulia - ukiwa na PhD lazima uwe na uwezo wa kudeal na issues scientifically, siyo kutumia maguvu tu, swine!
Hongereni Timu Lowassa na Timu Membe...hadi Jiwe kujaribu kutengeneza Identity yake ndani ya CCM lakini akashindwa na akwarudia hakika nyinyi ni magwiji wa siasa za nchi hii - hasa Mzee mzima Edo, hizo nywele nyeupe hukupewa bure Mzee Baba
Hope in future nitaona Taasisi ya Siasa na Uchumi ya Edward Lowassa CCM ama Chuo Kikuu Dsm; Taasisi ya Siasa na Diplomasia ya Bernd Membe CCM ama Chuo Kikuu Dsm!