Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Siku hizi Lowassa kawa mzanzibar mpaka awemgombea mwenza wa Seif?.
 
Kwa sasa makamanda hawaoni hawasikii. Wao ni Membe tu tangu waamkapo hadi walalapo. Hata Mbowe wamesahau kuwa anasota lupango, au yule mgonjwa wa kule ubelgiji ndio wamemsahau kabisaa.
 
Hizi ndo hesabu za mvurugano.wapinzani wameamua kukokotoa hesabu hizi kimakusudi kuwatibua ccm.bashiru kwa ugeni wa kazi na kukosa uzoefu wa siasa halisi katibuliwa.anakuja kuonekana kituko.siasa hazisomewi.

Wapinzani wanaamini membe ana ushawishi wa watu flani ndani ya ccm.wanataka wamtumie avuruge ndani...amtie jakamoyo mheshimiwa.wanaamini inaweza mnyima raha mkuu.

Wanajumlisha na january ndani ya nyumba ili naye ahusike kutibua maji wnayokunywa wana ccm.january yupo makini.hatoi matamko.anajipanga.kwa mwaka 2020 hawa wote hawana matumaini mahesabu yao ni mwaka 2025.ambako pia wasahau.kwa nini?

Magufuli atakuwa anamweka mtu wake.hawezi waachia hao watu hata iweje.najua yupo smart katika hili.lakini pia wakati wa uchaguzi ccm hupingana na wapinzani wote ili wabaki wao waendelee kutawala.

Hesabu za mvurugano zinakosa majibu yanayotakiwa sababu mtu kama membe ni mdogo sana asiye na ushawishi wowote ndani ya chama.atafutwe mwingine
 
Pole sana chadema haipangiwi nani wa kugombea urais, ccm ndiyowanagombania u rais kama mpira wa kona. Membe Sasa hivi anamjambisha kiongozi wa watu wasiyo julikana.
 
Kama kucheza na akili za watu, ngoja presida amuite Membe ikulu kumsalimia na mazungumzo kidogo kama kada tu halafu ndio utajua siasa ni mchezo wa psychologically torture hahaha
 
Hizi ndo hesabu za mvurugano.wapinzani wameamua kukokotoa hesabu hizi kimakusudi kuwatibua ccm.bashiru kwa ugeni wa kazi na kukosa uzoefu wa siasa halisi katibuliwa.anakuja kuonekana kituko.siasa hazisomewi.

Wapinzani wanaamini membe ana ushawishi wa watu flani ndani ya ccm.wanataka wamtumie avuruge ndani...amtie jakamoyo mheshimiwa.wanaamini inaweza mnyima raha mkuu.

Wanajumlisha na january ndani ya nyumba ili naye ahusike kutibua maji wnayokunywa wana ccm.january yupo makini.hatoi matamko.anajipanga.kwa mwaka 2020 hawa wote hawana matumaini mahesabu yao ni mwaka 2025.ambako pia wasahau.kwa nini?

Magufuli atakuwa anamweka mtu wake.hawezi waachia hao watu hata iweje.najua yupo smart katika hili.lakini pia wakati wa uchaguzi ccm hupingana na wapinzani wote ili wabaki wao waendelee kutawala.

Hesabu za mvurugano zinakosa majibu yanayotakiwa sababu mtu kama membe ni mdogo sana asiye na ushawishi wowote ndani ya chama.atafutwe mwingine
Eti nini Membe hanaushawishi mpange na jiwe afu wape haki sawa utanambia
 
Msitake kuwagombanisha watu na Raisi wao.
Utaratibu ulioubalika ni kwamba Raisi anagombea katika vipindi viwili, hivyo awamu ijayo raisi atagombea tena.
kwani amekatazwa[emoji196]
agombee tu ila membe atakuwa nae pembeni
 
Habari za Jumapili waungwana

Uchaguzi mkuu wa Urais, wabunge na madiwani unatarajiwa kufanyika 2020 hapa nchini. Ni kiasi cha kama miaka miwili tu ijayo

Kwa mtazamo wangu huu ndio muda muafaka kwa wale wote wanaotaka kugombea hasa nafasi ya Urais wawe ndani ya Chama tawala au Upinzani wajitokeze mapema na kutangaza nia zao za kuomba ridhaa ya vyama vyao kugombea nafasi hiyo

Kwa kufanya hivyo watakua wanatutendea haki Watanzania kwa sababu tutakua na muda wa kutosha kuwapima uwezo wao wa kila nyanja

Miaka miwili ya kumsoma mtu mwenye nia ya kua Rais wa nchi yetu inatosha kabisa kufahamu utimamu wa afya yake ya akili, uwezo wake wa kiuongozi, uwelewa wake wa masuala muhimu ya ndani na nje ya nchi, kuchimba historia yake, uadilifu wake kuanzia ngazi ya familia na uzalendo alionao kwa nchi.

Itatupa pia nafasi ya kumpima uwezo na utayari wake wa kuunganisha nchi hii ambayo inamchanganyiko wa matabaka mbalimbali ya kijamii. Pia itatupa fursa ya kumjua mtia nia anauelewa gani kuhusu dunia ilivyo, uchumi unaendeshwaje na kama anatambua kinaga ubaga changamoto zainazoikabili dunia yetu na mikakati yake ya kuivusha salama nchi yetu katikati ya changamoto hizo

Huu ndio utaratibu uliopo katika nchi hasa zilizoendelea. Ni utaratibu ambao unahakikisha kua Rais ajae anakua ni mtu mwenye uwezo hasa wa kua kiongozi wa nchi na sio kituko

Tatizo tulilonalo kwenye nchi yetu ni kwamba tunataka surprises za dakika za mwisho. Tena tatizo hili lipo kwa vyama vyote vya siasa. Wanatuletea tu wagombea huku wanatuona Watanzania ni mazwazwa, tutamchagua tu hata watuwekee jiwe ilimradi chama kimempitisha! Utamaduni wa kuteua wagombea kama bahati nasibu ipo siku utatugharimu kama Taifa!!! Tutakuja kumpata Rais wa ajabu haijawahi kutokea, atakaekua ni aibu na fedheha kwa Taifa

Binafsi sijamsikia Bernard Membe akitangaza nia ya kugombea Urais lakini yalipoletwa madai kama anayo nia hiyo yametokea maoni tofauti ambapo watu wengine wanamuunga mkono na wengine wakimpinga na hata kumkashifu na mwenyewe hajakubali wala kukataa madai hayo

Kwa mtazamo wangu kama kweli Bwana Membe anayo nia ya kugombea nadhani kafanya jambo zuri sana. Huu mjadala unaoendelea kumuhusu naona kama ni mjadala wenye afya sana ambao unaweza kutuonyesha uwezo na mapungufu ya Membe ili wananchi wamjue na waamue

Badala ya kusema hana haki ya kugombea(kwa utamaduni wa CCM?) mjadala ungejikita katika kuchambua uwezo wake na mapungufu yake na kama hafai basi mapungufu yake yasemwe waziwazi na kama anafaa basi isiwe nongwa kwa yeye kutia nia ya kugombea

Ningependa na watu wote wenye nia hiyo kutokea vyama vyote wangefanya hivyo na wao ili watupe fursa na muda wa kutosha wapiga kura wa kuweza kuwachambua na kuwajua na isije kua tena mambo ya kushangazana dakika za mwisho
 
Well said lkn sioni kama hilo linaweza kutokea ktk bara la Africa na nchi zake zilizomo kwni nchi nyingi za kiafrica demokrasia ipo upande mmoja tu wa chama tawala kwa wakati huo nasi kwa vyama vyote kwn kwetu upinzani ndan na nje ya chama ni uadui mkubwa ambao kiongoz yoyote aliyeko madarakani hapendi kuusikia kwan kwa mawazo ya viongoz wengi nikwamba upinzani ndan ya chama chake au nje ya chama chake unahatarisha usalama wa utawala wao hvyo njia pekee ya kujilinda na mtu yoyote mwenye nia ya kutaka kujinadi mapma sera zake ni kumpa kashikashi za kila aina ili kumdhoofisha so kwayanayotokea hpa kwetu sio mageni na kamwe uliyoyaeleza hayawezi kutokea zaid na zaid tuendelee kusbir wnye mamlaka watuamulie wachaguane kbsa ksha sisi tutmize jukumu letu kikatba kupga kura ilihali mshindi anajulkana.......#tukutane2020
 
Unaelewa maana ya kutia NIA?
 
"Wana jamvi tuliochoshwa na huu utawala wa mtawala wa nchi ile hebu tuimbe haka kanyimbo hadi asikie aelewe kuwa hatuutaki uongozi wake na matendo yake"

Nimepita kijiwe cha wana CCM kindakindaki nimesikia wakiimba na kuelezana. Kweli wamemchoka!
 
Back
Top Bottom