Kwa sasa kuna mvutano ndani ya CCM kuhusu uhalali wa watu wengine kugombea nafasi ya uraisi wakati aliyekalia kiti bado anaruhusiwa kugombea tena kwa mujibu wa katiba. Lakini huu ni mtazamo usio sahihi kwa sababu zifuatazo
1. Iwapo muda wa uchaguzi utafika, halafu mazingira ya kisiasa yakafika ikaonekana chama kitapoteza uchaguzi kwa kumsimamisha tena Magufuli, itakuwa ni suicidal kulazimisha agombee ( Labda kama kina Plan B ya ushindi nje ya sanduku la kura). Katika muktadha huu, ni muhimu chama kikawa na mtu au watu wenye uwezo wa kusimama na kuuzika na kukubalika. Kwa hiyo ni muhimu sana kwa watu kama Kammilius Bernad Membe kuendelea kupiga Jaramba ili Chama kitakapoamua basi aweze kubeba bendera kwa weledi zaidi na kukipa chama ushindi
2. Duniani hakuna anayejua ya kesho, Mungu pekee ndiye anayejua ya kesho, Uzima na afya zetu ziko mikononi mwa Mungu, kutokana na ukweli huu lazima kila Taasisi na siyo CCM tu bali hata vyama vya upinzani, lazima viwe na plan B ikitokea emergency!. Naambiwa hata kwenye mambo ya kiserikali, protokali zinataka chain of command ilindwe, ili ikitokea dharura basi mtu ambaye yupo katika chain of command anatake over smoothly!. Je CCM plan B ni nini?, Nani ameandaliwa na chama kushika nafasi iwapo mgombea anayetegemewa hatokuwa katika nafasi ya kugombea?.Au mnataka kuzima moto na kulipualipua kumleta mtu ambaye hajajiandaa kushika usukani kwa tiketi ya chama?. Swali hilihili linapaswa kuulizwa kwa vyama vya upinzani pia
Kwa hiyo kwa mujibu wa sababu hizo kubwa mbili. Ni muhimu sana kwa Kammilius Membe kuendelea kupiga Jaramba mdogomdogo.Wahafidhina wa CCM wanaonufaika leo watamchukia, lakini kuendelea kujinoa na kuwa tayari ni muhimu si kwa chama chake tu, bali kwa Taifa zima!. Taifa halihitaji mtu aliyekurupuliwa from nowhere na kupewa urais, Taifa linahitaji Mtu aliyejiandaa vyema, mwenye malengo kuja kuwa raisi
Nadhani Kammilius Membe atakuwa rais mzuri kwa sababu
1. Ana exposure, yuko sophisticated, hana mambo ya kilugaluga
2. Ana Akili nyingi sana, reflection ya I.Q yake ni Diplomasia iliyoenda shule. Ana first class huyu chuo kikuu maana yake ni kwamba hahitaji kutumia misuli mingi kung'amua kilicho bora na sahihi kwa nchi ukilinganisha na wale wenye shule za kuunga unga hadi kuwa madoctor au Maprofesa
3. Ni Jasusi aliyebobea, anaijua nchi nje ndani, amefanya kazi "kitengo" ofisi ya rais tangu akiwa kijana mbichi, anaijua Ikulu, anajua power za Ikulu. anajua afanye nini ili kuweka mambo sawa
4. Ana ajenda kabambe ya uchumi, anajua kuwa elimu yetu inahitaji restructuring, kuwekeza kwenye vyuo vya ufundi etc
5. Siyo Mdini, hawezi kufanya teuzi za ubaguzi wa waziwazi wa kidini, Siyo mkanda, siyo mkabila
CCM mwacheni Membe apige Jalamba!