Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Lowassa alitumia miaka 10 kujitangaza mitandaoni na kuwatumia viongozi wa dini eti wanamuomba kugombea urais na zaidi ya yote lowassa alikuwa kila mtu mwenye harambee lowassa anaomba awe mgeni rasmi na kutoa mafedha kedekede , akaanza kupanga safu yake ya uongozi kwenye jumuiya za ccm kuanzia vijana, UWT, jumuiya ya wazazi , wajumbe wa NEC , wajumbe Wa mkutano mkuu.
Kikwete akiwa rais akawa anamchora tu akijua wapi atakapomfyekelea mbali, kikwete yeye akaanza kupanga safu ndogo sana ya kamati ya maadili Kwa kuwaweka watu wake na kuhakikisha watu wenye damu ya lowassa hawapo,ilipofika muda kikwete akiwa na kamati isiyozidi watu 10 akamfyekelea mbali.
Shikamoo kikwete
 
220px-Tundu_A._M._Lissu.jpg

Kila niionapo hii picha huwa nafarijika sana huku nikiwaza siku yake ya kuapishwa pale uwanja wa Taifa akinamama akina baba wenye mapenzi ya kweli na nchi yetu watakavyozimia kwa furaha.
 
Kumekuwa na ubishani mkubwa kwamba Membe hawezi kumtoa Magufuli 2020 kwa sababu katika historia ya Tanzania hilo halikuwahi kutokea. Mimi nasema hapana,yote yanawezekana na sababu zipo lukuki!

Nikiangalia kwa upande wa CCM Mwanadiplomasia Bernard Membe ndiyo mtu pekee anayeweza kupindua meza kibabe pale CCM.

Acheni mawazo duni. Mbona babu zetu waliamini Nyerere na wenzake wangeweza kupindua meza kibabe ya mkoloni. Iliwezekana vipi?Ni mikakati kabambe inahitajika na siyo jambo la kitoto.

Sababu za Membe kufanikiwa hili ni nyingi kuliko kushindwa kwake.

1. Kutokubalika kwa Magufuli ndani na nje ya CCM

2. Kukosekana kwa utengamano wa kweli

3. Nia ya kuirudisha Tz kimataifa

4. Nia ya kurudisha mchakato wa Katiba ya Watanzania

5.nk

........... itaendelea(nitafafanua)
Inawezekana kama usingizi uliobeba ndoto hiyo hautakatika.
 
Hizi kelele ni za ndani ya nchi. Kumbuka rais wa nchi hachaguliwi na wanaccm tu. Usishangae hizi kelele zikasababisha serekali ikaamua kununua korosho za wakulima kilo sh. 5,000 ili kuzima hizi kelele za Membe.
kwa hiyo hakuna chama chochote cha siasa kilicho nyuma ya hii ajenda...

Ina maana watanzania wengi bila kujali vyama vyama vyao wanamtaka Membe....unataka kusema kwenye hili ccm na chadema pamoja na ACT wote wanamtaka Membe.

Mkuu nipe majibu ya kunielemisha sio kisiasa yaani kiujumla jumla.
 
Lowassa alitumia miaka 10 kujitangaza mitandaoni na kuwatumia viongozi wa dini eti wanamuomba kugombea urais na zaidi ya yote lowassa alikuwa kila mtu mwenye harambee lowassa anaomba awe mgeni rasmi na kutoa mafedha kedekede , akaanza kupanga safu yake ya uongozi kwenye jumuiya za ccm kuanzia vijana, UWT, jumuiya ya wazazi , wajumbe wa NEC , wajumbe Wa mkutano mkuu.
Kikwete akiwa rais akawa anamchora tu akijua wapi atakapomfyekelea mbali, kikwete yeye akaanza kupanga safu ndogo sana ya kamati ya maadili Kwa kuwaweka watu wake na kuhakikisha watu wenye damu ya lowassa hawapo,ilipofika muda kikwete akiwa na kamati isiyozidi watu 10 akamfyekelea mbali.
Shikamoo kikwete


Kwa taarifa yako na hili bandiko lako refu JK alimtaka Membe na kwa sababu ya hiyo nguvu ya Lowassa ndani ya ccm ndio iliyopelekea Magufuli kuitwaa hiyo nafasi. Usitake kumpa JK sifa asiyokuwa nayo. Na huyu Magu na vile hawezi siasa za ushawishi ndio atapigwa chini kirahisi. Huu ndio mwisho wa kikundi cha utekaji na kupiga risasi wengine.
 
Aaahh kwa haraka haraka utagundua Vijana wa Lumumba upande wa Jiwe ndo hawahawa walofungua nyuzi zakujifanya wanampenda Membe ,ili mradi tu kujaribu kupenyezesha mpango wa membe alonao.

Hapo ndo tunarudi kulee ,jiwe alipopiga marufuku wanachama kuanza kuanza kupiga kampeni zao mapema.


Kwa ufupi..ukiwa na akili ya kawaida, utaona km ni Wafuasi wa membe...lkn kihalisia ni wafuasi wa JIWE ..namwisho Membe atajitoa mwenyewe..

Kimkakati, na Membe ni Mwanasiasa Nguli na mzito WALA HAWEZI KAA AANZISHE VIJIKAMPENI VYA KIPUUZI NAVYOVIONA HUMU .


Hata ivo Rais Ajaye ni Tundu Lissu .
Hiyo ndo nightmare kubwa ya jiwe na ccm, Lissu hazuiliki labda kwa risasi, na kwa taarifa tu ni kwamba hatarudi Tz kabla ya kutangazwa kuwa mgombea rasmi wa uraisi wa muungano wa upinzani Tz
 
Nitamuunga mkono membe ili alifurumushe tu jiwe afu baadae narudi zangu upinzani
 
Nikajua utakuja na wazo jipya kumbe bado una imani na ccm?
 
Ninyi watu msije mkauza nchi uarabuni kwa kujua au kutokujua
 
kwa hiyo hakuna chama chochote cha siasa kilicho nyuma ya hii ajenda...

Ina maana watanzania wengi bila kujali vyama vyama vyao wanamtaka Membe....unataka kusema kwenye hili ccm na chadema pamoja na ACT wote wanamtaka Membe.

Mkuu nipe majibu ya kunielemisha sio kisiasa yaani kiujumla jumla.

Mkuu watanzania huwa wanachagua kiongozi au huwa wanaletewa kiongozi na vyama vya siasa? Rais gani amewahi kupata zaidi ya nusu ya kura za wenye sifa ya kupiga kura? Rais wa nchi hii ni mwenye kura nyingi zilizopigwa. Na kwa taarifa yako hiyo kupiga kura ni kutimiza tu kiini macho cha demokrasia lakini rais hupitishwa na kitengo nyuma ya pazia regardless matokeo ya box la kura.

Watanzania wanachagua yoyote anayeletwa na chama. Hivyo hoja ya watanzania wote wamekubaliana hilo jambo halipo. Hakuna anayemtaka Membe sana sana hapa magu anarudishwa kwenye mstari kwa kuonyeshwa yeye sio kila kitu maana amelewa madaraka hivyo anafanya atakavyo. Mimi binafsi simkubali Membe, ila kama ataweza kutumika kumrudisha magu kwenye mstari nitamuunga mkono.
 
Hizi sasa ni bange, yaan mnataka kutugeuza watanzania kuwa machizi? Membe huyu huyu awe Rais wa Tz?
Ni afadhari aendelee Magufuli hadi azeekee Ikulu kuliko hiyo laana mnayoitaka.
Upumbavu km huu ulifanyika kuelekea 2005 tukadanganywa. Yaliyotokea baada ya kuingia mkenge wote tunajua. Bahati nzuri huyo Membe tunamjua udhaifu wake na tamaa zake tunazijua. Ccm haiwezi kumpitisha membe labda akagombee kwa manyumbu kwani huko akiamua Mbowe tu mchezo umeisha hakuna mjadala. Atakaepinga ataitwa msaliti.
 
Nimeeelewa jiwe anataka kufanya "cleaning the house thing" by setting membe up.
But kwa lengo lipi hasa nn target yake?
Walomtaja MEMBE ..ndio hao hao vijana wa JIWE.

Membe hawezi ruhusu vijana wake wawe ivi HATA SIKU MOJA UKU AKIJUA ALOKO MAGOMENI NI JIWE.

hawa nivijana wa Mitandaoni wa Jiwe, na usikute niwale waloitwa na Mtume Paul nahii ndo kazi walopewa ,ili mradi kumfanya Membe ajitafakari.

Mbona nirahisi kuelewa mchezo ulivo.
 
Shida kubwa ya wanasiasa ni kujipa matumaini ambayo ni unrealistic. Tunajua fika mfumo wa uchaguzi wa CCM. Tunajua fika nguvu ya nwenyekiti. Tunajua kuwa vikao vya NEC na CC-ambavyo mwisho wa siku ndio hifikisha wagombea wa kwenda NC-jinsi gani vimehodhiwa na mamlaka ya mwenyekiti. Tunajua fika kuwa ni mwenyekiti alivyo na uwezo wa kutumia vyombo vya dola kudhibiti mchakato mzima. Tunajua fika maraisi wote wastaaf ambao nguvu zao za ushawishi ni dhahiri wanasimama na Rais aliyepo madarakani.

Msijipe matumaini kuwa bwana huyu hajui political games. Alipopunguza wajumbe wa vikao vya maamuzi ule ulikuwa ni mkakati wa kupunguza watu wa kufanya maamuzi na kurahisisha party dominance.

Tuache kujidanganya, by all facts 2020 Ni JPM tena. Wengine wanaweza gombea sababu ni uhuru na haki yao kikatiba.
 
Back
Top Bottom