Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Hakika ni tumaini jipya kwa watanzania anapaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo hii ni kutokana na ukweli kwamba ni mtu mwenye mtazamo wa kimataifa na mwenye uwezo wa kurudisha heshima ya nchi yetu kidiplomasia.
Siku akipotea mmsaidie kumtafuta..
 
Baada ya Jana na Leo kufululiza thread za hiki kichwa adimu, aghalabu nyoyo za wadanganyika zimepata faraja, pengine faraja na neema tulizoziishi enzi za baba Ritz zinatarejea.
1. Mmefanana hulka
2. Umakini
3. Upole na kusikiliza maoni ya watu
4. Ubobezi wa kidiplomasia
5. Halafu wote mlianzia mambo ya nje
6. Marafaki wa mataifa
7. Very smart katika maamuzi
Twende na Membe 2020
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] naunga mkono hoja
 
Ni kweli kama Membe akiwa Rais siwafichi naingia ' Msituni ' rasmi na najua nitapata Ushirikiano wa nani au nchi gani ila nina uhakika kama akidumu sana basi itakuwa ni Wiki mbili tu au Mwezi ila ' nitamsumbua ' na ' nitamtesa ' mno kisha najua nitammudu na nikisha ikamata Tanzania yote bila hata Kinyongo naitisha Uchaguzi wa Haki na Halali na Mshindi yoyote atakayepatikana nitamkabidhi nchi yenu mara moja ili aongoze Kiustaarabu na Kidemokrasia kisha ' Mwanamume ' narudi zangu Nyumbani Kwangu ninakokupenda JamiiForums naendelea kuangalia ' Mpuuzi ' mwingine atakayeleta ' Fyoko Fyoko ' nimuendee tena Msituni.


Basi kwa taarifa yako sisi tunapigania uchaguzi huru na wa haki. Tunamuunga mkono yoyote atakayepambana na huyu anayechezea demokrasia yetu. Tumechoka hata akituonyesha picha za SGR 1000 hatumtaki. Demokrasia yetu ni muhimu kuliko hizo reli na ndege zake. Hizo reli na ndege hata wazungu wangeleta maana zilikuwepo lakini tuliwaondoa. Aje huku mitandaoni apate majibu kwa jinsi watu wanavyomshangilia mwizi ndio ajue hatuna mpango naye na yoyote mwenye tabia zake.
 
Membe hana impact yoyote ile ndani ya CCM au nje ya CCM, Magufuli ataendelea kuwa Rais mpaka 2025.

Na akimaliza muda wake au akitoka huyu tutaangalia nchi tumpe ama Profesa Makame Mbarawa au Dkt. Hussein Mwinyi kwani GENTAMYCINE navutiwa nao sana Kiuongozi na nawaona ni ' Potential Candidates ' kwa mwaka 2025 na wakitaka wanifurahishe kabisa kama mmoja wao akichua nchi basi Uwaziri Mkuu ampe / apewe Waziri ninayemkubali katika Awamu hii ya JPM aitwae Suleiman Jaffo. Naamini CCM hawataniangusha katika ' machaguo ' yangu haya na yatakuwa kama ninavyoyaombea yawe lakini wakijisahau au kujiroga tu wampe Membe ndipo mtajua kuwa kumbe hata Tanzania ' Waasi ' wapo ila wametulia tu wakiusoma mchezo na ' nitakinukisha ' Tanzania nzima hadi Membe akimbie nchi.
 
Tuambiane jamani, hizi nyuzi nyingi za Membe kwa wiki hii kutokea ghafla ghafla ni coincidence au kuna kitu kinaendelea 'behind the scenes'. Mwenye taarifa credible,please.
 
Unafiki wetu hautatuacha salama. Leo Membe tegemeo la mtz. Akishakaa kwenye kiti tunabadilika mbona Amelkuwa ndivyo sivyo. Kama usitegemee binadamu kukufanikisha kwa kila kitu. Kuna walio sema Nyerere alikuwa bora, wengine Mwinyi, wengine Mkapa , wengine Kikwete na hata leo wapo wasemao Magu ni bora. Wategemeoa Membe pia wanaweza cheka siku moja au kulia kama wengine leo waliao. Cha msingi ni kupambana na maisha yako, mengine mwachie Mungu.
 
Habari wana jamvi.. Leo nimekutana na nguli wa diplomasia katika Mishe mishe za hapa na pale, nikapata walau lisaa La kupiga nae story.

Kasema amewamiss sana Watanzania. Amewakumbuka sana hivi karibuni na pia anawatakia jumapili njema.

Nawasilisha.
Asante kwa salamu.

Mwambie vile viatu alivyoviacha braza kuna jamaa mwenye miguu mikubwa amevivaa. Keshokutwa anatarajia kuvivua akaoge. Aje tu akajaribu kama ataviweza. Ila asitegemee sana maana jamaa amevitanua sana vitampwaya.
 
Back
Top Bottom