Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Naomba niwaambieni kwa wale wambao mnafikiri ndani ya CCM hapawezi kua na mabadiliko yeyote ni kujidanganya kwa ssbabu ya mazoea ya nyuma, kwa vijana mliokua juzi yawezekana hamjui kitu ndio maana mnajipa matumaini kwa msilolijua. Hamuelewi na hamwezi kujua.

Siasa sio ubabe wala vitisho bali ni ufundi wa mtu kulingana na utashi wake. Ndani ya CCM kuna wanachama wenye kadi na katiba ya chama, wameisoma katiba na wanaelewa yaliyomo ndani yake na yanayoendelea hivi sasa. Ili kuepusha mgogoro ndani ya CCM ya sasa ni bora watu waachwe wateme nyongo zao kiliko kutumia mabavu na kukaa na mambo nyoni.

Kwa msiojua ni kwamba haya ya utawala huu wa sasa ni kwa sababu ya siasa za Bernard Membe ndani ya CCM, anajua ni wapi alijisahau na aliteleza na sasa anajiweka sawa asirudie makosa. Katiba ya chama inamruhusu kufanya hivyo, hayo mengine ya mwenyekiti wa sasa kurudi kugombea tena ni taratibu ilizo nje ya katiba na sio lazima.Waliofikiri asingeweza sasa wameina ni bora ngekua yeye kuliko tulikofikia.

Vijana wenzagu mkae mkitafakari kua Bernard Membe haya mawazo ya kutaka kua kiongozi wa taifa hili 2020 sio yake peke yake,atakua ameshauriwa na wazalendo wakongwe ambao tayari hawaridhishwi na upepo wa siasa za sasa. Mtu wa aina hii kutajwa sana sio kitu kidogo, kutakua na msukumo Mkubwa sana tena wa watu wanaojua ni wapi tupo hivi sasa.
Membe oyeeeee
 
Kuanza kufikiria raisi mwingine ili hali aliyopo madarakani anadaiwa kuwa kipenz cha watu si habari njema hata kidogo hasa ukizingatia kuna miaka 7 mbele.
Je hakuna mwingine vichwani mwetu afaae zaidi ya membe au yeye ndiye tumemtoa chambo aanze wengine wafatie
Mimi namuona Hussein Mwinyi ni kijana mtulivu na mwenye busara

Leta majina mengine kwa 2020 october
Membe oyeeee
 
BENARD MEMBE NDIYE ALIKUWA MGOMBEA SAHIHI 2015 .ISINGEKUWA CHUKI YA MKAPA LEO MEMBE ANGEKUWA RAIS WA TZ.AJIPANGE TU 2020
Suala siyo leo angekuwa ni rais, angekuwa ni raisi wa aina gani? Huyo mtu ambaye alishindwa kupata uzoefu wa kazi yake kwa miaka yote hiyo, ulitegemea awe rais wa maana?

Pesa yetu ya Gagafi iko wapi? Chenji ya rada iko wapi? to hell with that uselessness.
 
Atagombea kupitia chama gani? Maana kwa CCM wana utaratibu wa kumwachia Rais aliyepo madarakani, labda kama utaratibu utabadilishwa. Membe asijitafutie mabalaa.
Membe ana uwezo na udhubutu wa kubadilisha meza kabla ya 2020..
 
Kwani katiba ya ccm ilibadilishwa tena?maana kama mwenyekiti akichukuwa fomu ya kugombea urais basi hakuna nyang'au anayechukuwa fomu..kwahiyo ya membe msahau kabisa
Nzee Nkapa anaweza kumwambia aache kuchukua fomu
 
Hili litawezekanaje? Wakati Mzee Baba kashawahi ktk katiba ya chama kapiga pin. Wajumbe wa Halmashauri kuu na NEC kapunguza kwahiyo kwa jinsi muundo ulivyo kwa sasa anaweza kuwamudu waliopo, sioni sehemu Membe atakayopenyea.

Ingekuwa muundo bado upo uleule wa zamani hapo sawa. Labda sielewi nieleweshwe.
 
kwa kweli kama ingewezekana hata kesho membe angeingia tu ikulu. yaani kwa sasa Tunaongozwa kwa hulka za watu na sio katiba na sheria tena.
 
Na akimaliza muda wake au akitoka huyu tutaangalia nchi tumpe ama Profesa Makame Mbarawa au Dkt. Hussein Mwinyi kwani GENTAMYCINE navutiwa nao sana Kiuongozi na nawaona ni ' Potential Candidates ' kwa mwaka 2025 na wakitaka wanifurahishe kabisa kama mmoja wao akichua nchi basi Uwaziri Mkuu ampe / apewe Waziri ninayemkubali katika Awamu hii ya JPM aitwae Suleiman Jaffo. Naamini CCM hawataniangusha katika ' machaguo ' yangu haya na yatakuwa kama ninavyoyaombea yawe lakini wakijisahau au kujiroga tu wampe Membe ndipo mtajua kuwa kumbe hata Tanzania ' Waasi ' wapo ila wametulia tu wakiusoma mchezo na ' nitakinukisha ' Tanzania nzima hadi Membe akimbie nchi.
hao Wazanzibar feki wasahau urais. baada ya Magu tunaingiza Mtanganyika tena. na ikiwezekana hata membe. huyo mbalawa kabebwa tu huku bara mara baada ya kupigwa chini ubunge Pemba hatumtaki.
 
Anayeongelewa ni yule yule aliyekuwa waziri awamu ya nne au ni mwingine? Tusisahau Mungu bado anaipenda TZ. Alituepusha na Membe 2015 japo alikuwa na sapoti ya vigogo lakini Mungu akasema NO. Ingekuwa Mungu anapokea rushwa ni wazi Membe anaweza kuwa rais wa TZ. Mungu hata siku moja hapokei rushwa na bado anaipenda saaana TZ.
mkuu tatizo wa sasa aliingia bila rushwa lakini ndo anashangilia rushwa ya kununua wabunge dah
 
jamani hizi topics za Membe leo kulikoni?
Sijui nini kinaendelea aisee ila mimi kwa tathmini yangu naona kama hii ni move yake basi ndio anajimaliza kama ni move wameanzisha maadui zake kisiasa naona wanataka kum expose ili watu wamchambue, wanaomsifia wafanye hivyo na wanaompinga wamchafue

Kwa siasa za kiafrika hili litakua na negative impact kwa BCM. Kwa mataifa yaliyoendelea ni suala zuri sana mtu kuonyesha mapema nia yake ya kuitaka Ofisi Kuu iliwatu wamfanyie tathmini ya kina
 
Back
Top Bottom