Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

hata penati aliyokosa samatta angekua membe angefunga goli zuri la kimataifa huyu jamaa kila sehemu anaweza.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kawafanya nini Membe ninyi watanzania wenzangu(ccm + chadema + others)
 
K
Eeh Mungu tuokoee sisi waafrica wa pumbavu na tusiwe kama huyu general mangi tusiona mbele hivi kweli huoni kazi ya magu kwelii au ulitaka kuendelea na kazi yak ya madawa ujambazi mix biashara za ujanja ujanja acheni kununuliwa tufanye kazi boss wako mwambie kashashindwa na soon tunamtumbuaa na yy
Kazi anayofanya zaidi ya kuzorotesha maisha na ustawi wa jamii. Wakulima wanalia, aliingia madarakani alikuta mbolea mfuko wa urea elfu 40, leo elfu 60. Aliingia madarakani alikuta gunia la mahindi elfu 75 leo gunia hilo elfu 15. Kikwete aliingia madarakani alikuta kima cha chini cha mshahara wa mwl alikuwabanapokea elfu 95, ametoka ameacha anapokea 545,000. Yeye ameongeza elfu 15 tu leo kima cha chini 560 ,Baba ako ameingia ikulu amekaa miaka mitatu hajapandisha mshahara kwa mtumishi yeyote wa nchi hii zaidi ya kulipa increment mara moja tu kati ya mara tatu zilizo hitajika. Kama huna data utamwona babaako amethubutu,lakini ukifuata magezeti utaona amefanya, hamna chochote anachofanya pale ikulu. Enzi za kikwete wananchi walikuwa wanajenga zahanati vifaa vya kiwandani wanapelekewa, leo fedha za miradi hazipelekwi kwenye halmashauri, wananchi wamejenga majengo ya shule,zahanati na miundombinu mingine zinabomoka na mvua.hakuna fedha za kunulia vifaa vya viwandani toka serikali kuu,halmashauri zinaambiwa zitumie mapato ya ndani, kwani wakati wa kikwete mapato ya ndani hayakuwepo ,mbona fedha za miradi toka serikali kuu alikuwa anapeleka kwenye halmashauri. Mwambie babako aliyemdanganya afuta LGCDG kwenye halmashauri hakumtakia afya njema, alimdanganya. Hizo fedha ndizo zilizo kuwa zinasaidia kusapoti miradi iliyokuwa inatekelezwa kwa nguvu za wananchi.leo hii mamiradi mengi yanabomokana tu huko vijijini
 
Siku ya mkutano mkuu wamuimbie "Tuna imani na Membe, Oya oya oya" .
Tuone kama atawapoteza wajumbe wote wa mkutano mkuu.
 
Siungi mkono hujuma dhidi ya kiongozi aliyeko madarakani. Namkubali kwa sasa kwa sababu ni rais wangu.

Nakukumbusha tu lolote lawezekana ikiwapo nia....na kamwe usichezee nguvu ya umma.

Jifunze kwa yaliyotokea Libya, Misri na kwingineko.

Watanzania tumpe support kiongozi aliyeko madarakani kutimiza ahadi zake.


Hata kukosoa nako kunasaidia kuyatambua madhaifu yetu
Kama hataki kukosolewaje ?!!
 
Ndoto za Alinacha hizo. #MagufuliTena2020 na 2025 atapita Rais anayemtaka yeye Mungu akimuweka.
 
Meza kupinduliwa kibabe itawezekana tuu, iwapo mabausa wake jk na bm watahamua kumuacha yatima, bila hivo usitegemee au hata yeye akistuka mapema hao mabausa wawili hawezi kufanya kitu.
 
Kazi iliyombele ya Membe ni kazi moja tu, ni kuling'oa Jiwe
Uwezo wa kuling'oa anao
Sababu za kuling'oa anazo

Aweke nia tu
Achukue fomu
Mengine atuachie sisi wananchi na wana CCM
 
Tehe tehe nafurahi kuona chadema wakijishughulisha zaidi na kumuimarisha Magufuli na ccm
 
Hivi bado mnaamini kuwa kina nyerere wangewaweza wakoloni kama wakoloni wenyewe wasingetaka.. Tatizo ukoloni ulishapoteza mzuka ulaya ndo maana waliamua kuacha hata Leo UK akitaka kuja chukua Tanzania... Anachukua kama utani tuu
 
Kelele za nini? Kama mtu amefanya yake akidhani anawatumikia ipasavyo na kumbe kashindwa kufikia matarajio yenu si kipindi kimoja kiki isha anakupeni mkono wa kwaheri kwa heshima na shukrani anaenda zake kula pension yake kwa amani?

Jambo hili liliwezekana kwa Raisi wa Zanzibar hayati Idrisa Abdul Wakili ambaye baada ya uongozi wake wa miaka 5 akaamua kwa hiari yake kuachiangazi na kutogombea tena ingawa alikuwa anajua kwa mfumo wa nchi hii ukitoka chama tawala kura wakitaka zitoshe zitatosha hata kama ziko mia tuu.

Nashangaa sasa hivi mjadala wa Magufuli VS Membe umepamba moto hasa kwa vile wanaccm wameonyesha kumchoka mwenyekiti wao naye kaonyesha mawimbi na ghoruba za bahari zimemzidi kama nahodha.

Mie namshauri bwana mkubwa kuwa aachane na wapambe wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili wale kwa ulaini, bahari imechafuka na dhoruba zaanza kuzamisha chombo chetu, 2020 akimuiga muungwana Abdul Wakili akamuachia unahodha mwingine kwa hiari kabla chombo hakijazama atajenga heshima.

Anaweza kuitumikia nchi hata kwa kutoa ushauri tuu.

Ya nini kubadilishana vijiti ionekane kama nongwa na kukasirikiana? Nyerere alisema hiyo kazi nzito sana, sasa kama mtu anataka kukupokea mzigo mzito kwa nini unanuna?
 
Kuua upinzani wa vyama ni kosa la kiteknikali la Magufuli. Upinzani wa ndani ya chama hauna afya kwa CCM ya Magufuli. Aliyasema haya Lema Godbless(Mb) kuwa akimaliza kwetu atahamia kwenu,hakuna aliyesalama.
 
Ukiangalia kwa jicho la tatu utaona mjadala wa kutaka au kuhakikisha Membe 2020 kwa njia za kidemokrasia ana geuza meza na kukabidhiwa kijiti na CCM umepamba moto baada ya kijana wao tegemezi January Makamba "kuhojiwa" masaa kadhaa na Polisi na mwishoni kuarifu umma kuwa pamoja na mahojiano hayo yuko "salama".

January, kiukweli ni moja ya vijana tegemeo ndani ya chama na sio siri kwamba anazidi value ya Mwenyekiti wa sasa kama utawathaminisha mbele ya wanachama.

Je, kitendo cha kusukwasukwa ndicho kilichowachokonoa wanaCCM kindakindaki kumkumbuka jasusi Ben Membe?

Lakini wanachama wanaelewa kuwa hili ni jambo la kawaida na sio uasi?
 
Kwahiyo mkuu unatushauri tuendelee kutawaliwa na hawahawa ccm?

Jitafakari upya tatizo siyo Magufuli ba li tatizo ni ccm, ukikaa na ukatuliza akili utaelielewa hili vizuri, Magufuli ana kura moja tu hata kama ni ya veto, veto huwa haina nguvu ya kushindana na kura nyingi.

Ccm ni mashetani akiwemo huyo Membe, mateso tunayopitia leo hayaletwa na Magufuli bali ni mashetani wa ccm kuikataa rasimu ya katibsa mpya ya Warioba.

Someni biblia mtaelewa vizuri Mungu aliwachapa Waisrael pale walipokengeuka, na Watanzania wanastahili kuishi maisha magumu ili akili ziwarudie.
 
mimi sijui lini watu wamejioganaizi kiasi hiki!
niwe mkweli, simkubali Magufuli kwa baadhi ya mambo lkn Membe simkubali kabisa, ataendeleza makundi, uhasama na JK atarejea kwa sura ya Membe.
Sitaki turejee tulikotoka milele
You have spoken my mind.
Bravo.
 
Back
Top Bottom