Bernard Kamilius Membe akifanya mazoezi makali sana ya kukimbia. Nikawaida yake kujiweka fiti kimwili na kiakili kwa kula kiafya na kufanya mazoezi hili awatumikie watanzania walioshakata tamaa kwa itawala mbovu wenye choyo ufusidi na wakuwagawanya wananchi kwa matabaka.
View attachment 914322
Kuna uzi humu nimeona unaelezea CV ya Bernad Membe nikawaza kidogo.!
Je ile CV kaiweka humu yeye mwenyewe? Au kaiweka mtu mwingine kwa niaba yake.
Kama kaiweka yeye mwenyewe lengo lake hasa mahsusi ni nini?
Nikawaza zile kelele za uchaguzi 2015.
Nikakumbuka kuwa alikuwa ni mmoja kati ya wapiga mbio wa Urais.
Nikatafakari tumebakiza muda gani kabla ya uchaguzi ujao 2020 nikagundua ni mwaka mmoja tu,! Nikaonanisha vuguvugu la korosho na wabunge wa kusini. Nape Nnauye na Hawa Ghasia.!
Nikakumbuka pia kujiuzulu kwenye moja ya kamati kwa Bi Hawa ghasia.!
Kisha nikarejea bei ya korosho na kususa ama kugoma kwa wakulima kuuza korosho zao. Nikachanganya na hotuba maelezo ya Ziito Kabwe na wale wanaojiita akina shangazi.
Nikachanganya na kuweweseka kwa upinzani kwa kukosa mtu mahsusi wa kusimama katika uchaguzi 2020.
Kisha nikamuona Bernad Membe anachungulia Dirisha la fursa 2020.
Anao mtaji wa Mtandao wa timu yake ambayo bila shaka haujafa kumbuka alikuwa anatumia magari meusi.! Akiwa wizarani. Anao wafuasi watiifu kwake kama kaka mkubwa katika taaluma ile muhimu aliyo ama anyoitumikia kwayo.
Ambao bila shaka wanaweza kumsaidia kupata taarifa muhimu anazohitaji kuzipata.! Anayo base aliyotengeneza nje ya Nchi akiwa Waziri ya mambo ya Nje.
Anayo nguvu ya watu wa upinzani ambao ni majeruhi wa utendaji wa serikali ya JPM.
Mtu huyu kamwe si wa kupuuzwa mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.!
Lisemwalo lipo kama halipo laweza kuwa njiani laja.