Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Binadamu hawana wema walimtusi kikwete sana tuu ila sasa wanamkumbuka, magufuli ataondoka hakai milele ikulu akija mwengine mtasema heri magufuli... Membe hana jipya wala hana mvuto wowote kisiasa na aliyemshauri kuanzisha harakati zake saahizi basi timing hajui maana ndo anapotea rasmi kwenye siasa kama lowasa.
Mh bora ya Magufuli? Duh sipati picha atakuwaje huyoo???
 
Bernard Kamilius Membe akifanya mazoezi makali sana ya kukimbia. Nikawaida yake kujiweka fiti kimwili na kiakili kwa kula kiafya na kufanya mazoezi hili awatumikie watanzania walioshakata tamaa kwa itawala mbovu wenye choyo ufusidi na wakuwagawanya wananchi kwa matabaka.

View attachment 914322
Kuna uzi humu nimeona unaelezea CV ya Bernad Membe nikawaza kidogo.!
Je ile CV kaiweka humu yeye mwenyewe? Au kaiweka mtu mwingine kwa niaba yake.
Kama kaiweka yeye mwenyewe lengo lake hasa mahsusi ni nini?

Nikawaza zile kelele za uchaguzi 2015.
Nikakumbuka kuwa alikuwa ni mmoja kati ya wapiga mbio wa Urais.
Nikatafakari tumebakiza muda gani kabla ya uchaguzi ujao 2020 nikagundua ni mwaka mmoja tu,! Nikaonanisha vuguvugu la korosho na wabunge wa kusini. Nape Nnauye na Hawa Ghasia.!
Nikakumbuka pia kujiuzulu kwenye moja ya kamati kwa Bi Hawa ghasia.!

Kisha nikarejea bei ya korosho na kususa ama kugoma kwa wakulima kuuza korosho zao. Nikachanganya na hotuba maelezo ya Ziito Kabwe na wale wanaojiita akina shangazi.
Nikachanganya na kuweweseka kwa upinzani kwa kukosa mtu mahsusi wa kusimama katika uchaguzi 2020.
Kisha nikamuona Bernad Membe anachungulia Dirisha la fursa 2020.

Anao mtaji wa Mtandao wa timu yake ambayo bila shaka haujafa kumbuka alikuwa anatumia magari meusi.! Akiwa wizarani. Anao wafuasi watiifu kwake kama kaka mkubwa katika taaluma ile muhimu aliyo ama anyoitumikia kwayo.
Ambao bila shaka wanaweza kumsaidia kupata taarifa muhimu anazohitaji kuzipata.! Anayo base aliyotengeneza nje ya Nchi akiwa Waziri ya mambo ya Nje.

Anayo nguvu ya watu wa upinzani ambao ni majeruhi wa utendaji wa serikali ya JPM.

Mtu huyu kamwe si wa kupuuzwa mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.!
Lisemwalo lipo kama halipo laweza kuwa njiani laja.
 
huyu membe vipi jamani mbona ameanza kusemwa kwa kasi ya ajabu!!
Mkuu, watu wamechoka, wanataka yeyote mwny uthubutu wamuunge mkono ang'oe jiwe..

Sultani Mbowe kafuta Uchaguzi chadema, hiyo ndo habari ya mujini!
So what?? Kwanza huo uchaguzi unatakiwa na wana lumumba kwa hila zao ili wapandikize mamluki wao kama lipumb wa Kafu.

Kwa sasa habari ya mujini ni hii:
"MEMBE4PRESIDENCY"
 
Mkuu, watu wamechoka, wanataka yeyote mwny uthubutu wamuunge mkono ang'oe jiwe..


So what?? Kwanza huo uchaguzi unatakiwa na wana lumumba kwa hila zao ili wapandikize mamluki wao kama lipumb wa Kafu.

Kwa sasa habari ya mujini ni hii:
"MEMBE4PRESIDENCY"


Yeah G. Membe + CCM for presidency, chadema bado hawawezi kuongoza hata hawajiamini ndo maana wanaipigia Kampeni CCM!
 
Kwani sasa hivi haruhusiwi kufanya mazoezi ?
Umeambiwa hiyo ni picha ya zaman kwa mantiki hii ni kwamba hizi ni propaganda tu.Hivi ushahama chadema?Au Membe ni chadema?Na unachukuliaje kauli ya ccm kutawala milele na ukizingatia saizi unamshabikia Membe ambaye ni ccm?
 
hili vugu vugu ni kutoka hapo hapo lumumba kwa maana membe sio mwanachadema yaani si kamanda, magufuli kaa tambua vita vya ndani ya chama ni vibaya kuliko ukimwi. anguko lako laja wanaokupigia makofi leo kesho watakurushia makopo.
Fuatilia wanamshambikia Membe ndio utajua ni bavicha au nani.
 
1.Mwanadiplomasia mzoefu.
2.Mwanakitengo mstaafu
3.Msomi aliyeelimika
4.Ana busara na hekima
5.Mzalendo
6.Mbunifu
7.Mediator mzoefu

Nimalizie tu hapo, ni jinsi tu ninavyomfahamu. Ni hivyo tu basis.
Mnaanza mapema propaganda za kutuuzia mbuzi kwenye gunia.Haya tuliyoyabeba mgongoni hayajatupa pumzi mnaongeza mzigo mwingine was gunia? Ama kweli Mungu tuokoe watz.
 
Wewe inaonekana umeanza kufuatilia siasa juzi
Unaendeshwa kwa hisia!Mahakamani unatoka kapa!JF kila mtu ana utashi wa kuwa na maoni yake!Sio kila anayetoa mawazo usiyopenda basi ni mpinzani,na si kila anayetoa maoni unayopenda ni CCM!
Hili kundi la wasio na vyama mnawanyima haki ya kuwa huru kutoa maoni bila kuwaweka kwenye makundi ya upinzani au uccm!
 
mimi sijui lini watu wamejioganaizi kiasi hiki!
niwe mkweli, simkubali Magufuli kwa baadhi ya mambo lkn Membe simkubali kabisa, ataendeleza makundi, uhasama na JK atarejea kwa sura ya Membe.
Sitaki turejee tulikotoka milele
Brother unaona mbali, naona watu wanafumuka fumuka tu bila kusoma alama za nyakati.
 
Back
Top Bottom