Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Habari za muda mabibi na mabwana!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza nawashauri wanachama wenzangu na wananchi kwa ujumla. Mwaka 2020 tusipoteze tena kama ilivyotokea mwaka 2015. Haya yote ni kwa sababu hatukutulia vizuri katika mchujo wa kumpata kiongozi bora.

Karibuni kwa maoni yenu.

Huu ni uchochezi nani kwa kwambia Membe anataka uraisi 2020. Mnataka kumzubaisha baba Jesca a-concentrate na upuuzi huu ache fanya mambo ya msingi. Jamaa yupo yupo mpaka 2025.Mtapata tabu sana.
 
Hakuna mwana CCM wa kumpindua Magufuli,,, tusipoteze muda kujadili hili lipo wazi,,, REJEA MABADILIKO ALIYOYAFANYA ,,,,anamejipanga kwa ubabe,,ameshajenga territory yake,,
 
Umekunywa maji ya wapi siku hizi mkuu,,,
Huyo waitara kahogwa fedha na wenzake walio wengi mimi ULAGHAI WA CCM umenichosha kiasisi cha kuwalaani double standards NAPE KAFUKUZWA KAZI BILA YA SABABU HUYU MAKONDA ALIYESHIKWA AKIKWEPA KODI ANAKENULIWA HALAFU TUENDELEE KUMUHESHIMU MYU ANAYEJIITA CHIZI WAKATI ANAMSIMIKA CHIZA HUKO BUYUNGU WANANCHI CHOZI LILIWATOKA.
 
Lowassa alitumia miaka 10 kujitangaza mitandaoni na kuwatumia viongozi wa dini eti wanamuomba kugombea urais na zaidi ya yote lowassa alikuwa kila mtu mwenye harambee lowassa anaomba awe mgeni rasmi na kutoa mafedha kedekede , akaanza kupanga safu yake ya uongozi kwenye jumuiya za ccm kuanzia vijana, UWT, jumuiya ya wazazi , wajumbe wa NEC , wajumbe Wa mkutano mkuu.
Kikwete akiwa rais akawa anamchora tu akijua wapi atakapomfyekelea mbali, kikwete yeye akaanza kupanga safu ndogo sana ya kamati ya maadili Kwa kuwaweka watu wake na kuhakikisha watu wenye damu ya lowassa hawapo,ilipofika muda kikwete akiwa na kamati isiyozidi watu 10 akamfyekelea mbali.
Shikamoo kikwete
Kuna watu wanajidanganya sana. Membe atafute kitu kingine cha kufanya...
Mpaka 2025 labda
 
Naomba niwaambieni kwa wale wambao mnafikiri ndani ya CCM hapawezi kua na mabadiliko yeyote ni kujidanganya kwa ssbabu ya mazoea ya nyuma, kwa vijana mliokua juzi yawezekana hamjui kitu ndio maana mnajipa matumaini kwa msilolijua. Hamuelewi na hamwezi kujua.

Siasa sio ubabe wala vitisho bali ni ufundi wa mtu kulingana na utashi wake. Ndani ya CCM kuna wanachama wenye kadi na katiba ya chama, wameisoma katiba na wanaelewa yaliyomo ndani yake na yanayoendelea hivi sasa. Ili kuepusha mgogoro ndani ya CCM ya sasa ni bora watu waachwe wateme nyongo zao kiliko kutumia mabavu na kukaa na mambo nyoni.

Kwa msiojua ni kwamba haya ya utawala huu wa sasa ni kwa sababu ya siasa za Bernard Membe ndani ya CCM, anajua ni wapi alijisahau na aliteleza na sasa anajiweka sawa asirudie makosa. Katiba ya chama inamruhusu kufanya hivyo, hayo mengine ya mwenyekiti wa sasa kurudi kugombea tena ni taratibu ilizo nje ya katiba na sio lazima.Waliofikiri asingeweza sasa wameina ni bora ngekua yeye kuliko tulikofikia.

Vijana wenzagu mkae mkitafakari kua Bernard Membe haya mawazo ya kutaka kua kiongozi wa taifa hili 2020 sio yake peke yake,atakua ameshauriwa na wazalendo wakongwe ambao tayari hawaridhishwi na upepo wa siasa za sasa. Mtu wa aina hii kutajwa sana sio kitu kidogo, kutakua na msukumo Mkubwa sana tena wa watu wanaojua ni wapi tupo hivi sasa.

Naona mumetumwa naona nyuzi kibao kuhusu Membe. Mmekubariana isipite week bila kutupia uzi unamuhusu Membe na uraisi. Baada ya kufatilia post zenu za nyuma hakuna hata mmoja mwenye nasaba na CCM. Ni uchochezi wa kutaka kumzubaisha Magufuri akomae na kulinda uraisi wake 2020 ili mpate nafasi ya kufanya yenu. Mnataka kufarakanisha Watu ili yenu yatimie. Magu amesha wastukia.
 
Hivi mnafikiri kwa safu aliyoipanga JPM ndani ya utawala wake kuna ambae anaweza kushindana nae,

Kwanza kapangua pangua wakuu wote wa idara ya jeshi, na ile ya ulinzi na usalama kaweka watu wake ambao wanamtii kwa kila kitu,

Pili upande wa mahakama kaweka watu wake ambao kwa hakika hakuna anaeweza kwenda kinyume nae,

Tatu kapanga safu yake tupu pale meza kuu ya CCM na pia kaweka vilaza ambao anajua watampigania kwa hali na mali ili nao wasikose ulaji mfano;Bashite, pole pole,gambo na yule RC wa iringa,


Wewe kama mwanaccm kindaki ndaki usitegemee maajabu yeyote kutoka kwa membe kwamba anaweza kushinda tiketi ya kuwania Uraisi kwa bendera ya chama cha mapinduzi,

JPM ni Man Action anajua kipi anafanya maneno na chokochoko zenu siyo kwamba hazisikii ila anajua haziwezi kumtisha yeye kunywa maji.

Cc Zero IQ.
 
Back
Top Bottom