Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Mkuu Mshana Jr kwa jinsi nchi ilivyo sasa ni heri tukarudi tu Misri hata kama Membe anaonekana anamguu mdogo kuliko viatu vyetu, yaani kama tu vile Mkwere alipofanya ile potelea mbali liwalo na liwe na kuamua kumzawadia KITI bwana Jiwe kuliko Mamvi basi na sisi wengine tunasema potelea mbali liwalo na liwe Membe atatutoa porini.

Ila tuwe makini tunaenda kwenye uchaguzi mgumu labda kuliko hata ule wa 2015, watu wengi sana watapoteza maisha maana kumbuka haiba ya weji na DAB ilivyo, ni watu ambao wanaamini zaidi ktk kupoteza na kufuta kabisa.

Mungu atutangulie.
Mungu hawezi tangulia watu wanaotaka kurudi misri hata siku moja, zaidi sana, atawaadhibu zaidi kama alivyowaadhibu wana wa israel walivyotaka kurudi misri.
Kwa iyo ninaamuru ibilisi aliyekujaa, atoke!
 
Mungu hawezi tangulia watu wanaotaka kurudi misri hata siku moja, zaidi sana, atawaadhibu zaidi kama alivyowaadhibu wana wa israel walivyotaka kurudi misri.
Kwa iyo ninaamuru ibilisi aliyekujaa, atoke!
Au sio?
 
Hili shindano la timu mbili. kila timu pinzani inapopoteza point timu nyingine inanufaika. Upande wa Membe unanufaika upande mwingine unapopoteza pointi. Kubalance ni upande unaolalamikiwa kujisahihisha na si kupiga nyundo! Diplomatic means!
 
kwa hali ilivyo sasa hivi hata wewe mshana ukionesha kumpinga mzee wetu ndani ya chama 2020 utapata sapoti sana humu mtandaoni lakini kwenye box la kura hutapata kitu. hivi nikuulize kitu unajua 2020 zitatumika kadi gani kupigia kura
 
Hii lugha ya kijuha ndo inanishinda kuelewa inamsaidiaje huyo mkuu wenu wa malaika!! Kila anayekosoa utendaji mbovu na wa kutafuta sifa binafsi wa bosi wenu mnambatiza alikuwa anafaidi ufisadi, mbona mnaounga mkono ndo wengi mlikuwa mnafaidi ufisadi? Chenge anampinga malaika? Ndugai anampinga malaika? Asas anampinga malaika?
Wewe mwehu umesoma vizuri na kuelewa maelezo ya post niliyo ijibu na ya kwangu?
Au umezoea kurukia mambo ovyo ukiendeshwa na hisia binafsi?

Je unafikiri lugha kama hizi tutaelimishana kitu ktk mijadala?
 
Kumbe bado wapo watanzania wenzangu wenye mawazo chanya kama haya! Nilidhani hatuzidi 1000 tunaofikiri kama we we.

Kibaya zaidi hata wale wanao jiita Great Thinkers wengi wameingia mtego wa mafisadi uchwara wa CCM na upinzani wanaotaka aondoshwe Magufuli awekwe mtu atakae waacha wafilisi nchi kama enzi za JK.
Watanzania hawajui ni nini wanakitaka ..huo ndo ukweli
 
Kumpamdisha JPM kwa sasa ni kazi sana, kosa kubwa alilolifanya ni kuchagua kuwa kila mahali. Katika uongozi hilo ni kosa kubwa mno. Kila jema linalofanyika mahali popote nchini wapambe walishauri ionekane ni yeye kafanya, na yeye kwa kupenda sifa akakubali na ikaonekana ni vema. Lakini kinyume chake hakiwezi kuwa sahihi, kanuni inakataa. Walitaka kuaminisha Umma kwamba wanapoona mazuri kwao wajue yameletwa na JPM, watu wakashangilia, wakataka kuaminisha kwamba mkiona mabaya kwenu basi mjue hao ni wapinga maendeleo; Hapo ndo watu wameshituka baada ya matukio matatu yaliyofuatana:-
1.Wabunge wa kusini kutetea fedha za korosho kwa maslahi ya wakulima wao na karipio walilopata toka kwa JPM mwenyewe hadi kutishiwa kupigwa shangazi zake Majaliwa.
2.Kuporomoka kwa bei ya korosho na maigizo ya JPM kujifanya kuwa mtatuzi pekee wa tatizo kiasi cha kukataa hadharani wanunuzi waluotafutwa na PM. Kwa hili wananchi wanajua chanzo cha tatizo ni yeye.
3. 25% Pensheni ni kanuni iliyowekwa na serikali ya JPM yenyewe na bunge kupitia Spika Ndugai lilikanusha kuhusika na kwa Mara ya kwanza Ndugai akamsifu waziri kivuli anayetokana na upinzani Esther Bulaya eti kwa kutoa ufafanuzi uliptukuka kuhusu kanuni ya 25% pensheni mkupuo.
***
Ukiangalia matukio hayo matatu tu mbali nabkwamba kuna mengine mengi, lakini haya yamesaidia kuwafumbua macho wananchi wengi hata waliokuwa vipofu kujua kuwa yule anayewaletea mazuri (machache/madogo) ndiye huyohuyo anayewasababishia mabaya (mengi/makubwa).
Kiongozi wa juu hapaswi kujiweka kila mahali Bali anapaswa kuwekwa kila mahali. Wengi humu tumesoma angalau kufikia elimu ya sekondari, mnajua hali ilivyokuwa kwenye shule ambayo Headmaster/mistress anaonekana katika kila tukio. Yaani kila asubuhi yupo paredi, mazingira anakagua yeye, shambani ni yeye, uwanjani timu ya shule anapanga yeye, adhabu - fimbo anachapa yeye; Halafu ETI heshima yake iliendelea kuwa juu hata timu ya shule ilipofungwa, mazao yalipoharibika shambani au shule iliposhuka kitaaluma.
**YEYOTE ANAYETAKA KUAMINISHA WATU MAZURI KALETA YEYE, ASICHUKIE ANAPOAMBIWA MABAYA PIA KASABABISHA YEYE**
Mkuu umenena vyema,huyu jamaa alitakiwa awe na mtu Wa kumdhibiti maana huwa anaamini yeye ni zaidi ya malaika,nadhani malezi yake hayakuwa mazuri,urais ni taasisi sio Mali ya mtu mmoja,tumemwona miaka mitano,he doesn't deserve to be given another opportunity,
 
Wapinzani,jikiteni kwenye issue za maana kama 25% ya mafao ,Madawa hospitalini,Ajira na maisha duni ya raia wa vijijini,Issue za Membe kugombea Uraisi,sijui maandamano,mtapata kura na Waandamaji wa kimjinimjini kama wa humu JF, afu mwisho wa siku mseme tulishinda kura milioni sijui ngapi,ohh tulifanya polisi wakaandamana,acheni kuwaza maslahi yenu binafsi la sivyo mkiwa na bahati magogoni mtaishia kupiga picha tu.
 
Shukurani kwa maelezo maana wengine na mie ya haya ya chama chao na Membe tunayasoma tu.. kuwaelewa nini haswa kinawasukuma kupiga ramli sana siku hizi na ni wao kwa wao wa ndani ya chama chao.

Kingine ni zile pesa walizoea pia kutumbua hawazioni tena.. matumbo motoooo..

JPM labda nae anatimu humu na kwingine.. inabidi washambulie kuwashushua kwa kuwajibu inavyotakiwa kwa nondo.. maana wanayoandika timu Membe kuvutia watu.. yanaweza pingika kirahisiiiii na kufanya watu wasivutiwe nao.

Na kumpaisha JPM kwa sanaaaaaa
Nikisoma maandishi yako yananipa tafakur juu ya uwezo wako mdogo wa kiuandishi na kimantiki,yaani unakoroga tu na hvyo kutoa picha halisi kwetu sis wasomaji kuwa wew ni mmoja kati ya mapopoma wanaoshabikia ujinga na ufedhuri wa jiwe kwakua tu mmepewa tuvyeo,mmesau mamilion yakiangamia kwa sera mbovu za kiimla!!!!
Masikini wanalalamika ambao wengi wao hawakuwai kushika vyeo vya kuiba lakini majibu mnayotoa yey na mapopoma wake ni mepesi mithili ya maneno mlevi wa pombe za kienyeji....!!!eti walizoea madili!!loh!!!The weakest defensive mechanism ever given by executive as leading organ!!!
 
Kuna mkorogano mkubwa sana mbele ccm asili wafia chama wasugua gaga vs ccm chotara wafia tumbo ccm maslai
 
Mshana huezi changanya tunguli hapo tukarudi kwenye mjadala wa mafao..25% haitoshi
 
Ishu inakuja hivi vipi mwenyekiti akimfukuza uanachama atapenyea wapi.
Ni mtazamo binafsi lakini wenye kuakisi ukweli... CCM inaandaliwa kuingia kwenye wakati mgumu tena, ni mtifuano wa ndani kwa ndani
. Urais 2020
. CCM asili dhidi ya CCM makinikia(mabaki)
. CCM kindakindaki dhidi ya CCM maslahi (wakuja)
Bernard Camilius Membe diplomat na jasusi wa muda mrefu, mshindwa wa kinyang'anyiro cha urais ngazi ya chama bado hajakubali kushindwa, bado ana ndoto ileile ya kukalia kiti kikubwa na amekamia hasa
Haiba ya Membe ni reincarnation ya haiba ya Kikwete (carefree) ni tofauti kabisa na haiba ya mzee baba KUKAZA hasa.... Membe ni expert mzuri sana kwenye mahusiano ya kimataifa, na pengine kwenye ushushushu lakini si kwenye siasa tena kukalia kiti kikubwa
Kipindi kile wakati wa kutafuta nafasi ya kuteuliwa, hakuonesha tofauti na wanaccm wengine, hakuongea cha ziada, wote walifanana... Hakutupa dira na maono ya tulipotoka, tulipo na tunapoelekea.. Wote katika ujumla wao ndani ya CCM walifanya mahubiri ya kisiasa
Akiwa shina moja na JK, ana sehemu kubwa ya lawama nchi ilipokuwa imefikia kipindi kile, kumpa usukani na kuendelea kuchanja mbuga kuelekea maporini

Sasa basi kwanini nasemwa asibezwe?! Huyu ni tarumbeta ya kupaza sauti ya wanaccm wengi wanaougulia kimyakimya na kushindwa kuongea kwa uwazi, kwa sauti
Huyu ni sauti ya manung'uniko ya wanaccm wengi ambao hawaridhishwi kabisa na mwenendo wa chama kwenye kila kitu lakini kubwa kuliko yote ni kule kuwapa wahamiaji (haramu) madaraka na nafasi za upendeleo... Wanapatwa na hisia kuwa kuna CCM mpya inaundwa taratibu ndani ya CCM halisi (CCM ya mwenyekiti dhidi ya CCM ya wote)
Ni kupitia hayo kwa uchache ndani ya mengi chamani, Membe ananijenga kwa kasi ya ajabu, na harakati zake hizo zilianza mara baada ya uchaguzi mkuu.... Membe ana kundi kubwa nyuma yake.. Ni vigumu kumdhibiti kama walivyodhibitiwa kina Makamba Jr, Lameck, Nape nk.. Huyu ni kada mzoefu chamani na wa muda mrefu... Ametumwa...!!

2019 hiyoo bado siku chache tu, Membe yuko nje ya nchi anakotuhumiwa kupanga mambo yasiyowapendeza watu fulani.. Huku wengine wakiona ni sawa... Hapa ni swala la mizania.. Nani ana wafuasi wengi zaidi wa hiari...
Membe anarudi kukanusha/kujibu tuhuma,.. Anajipanga kisawasawa, ameshaanza kusafishiwa njia na timu zake mitandaoni .... Ni yeye tu ndio anasikika na kujadiliwa... Na kwa sehemu kubwa akisemwa vizuri na akitabiriwa vema... Hivi vitu havifanyiki kwa bahati mbaya... Ni mipango inayosukwa kwa ustadi sana..

Hivyo basi pamoja na kwamba hatoshi kukalia kiti kikubwa, lakini ni tishio kubwa... Akiamua (kwa nguvu ya wapambe wake) ataiteka December yote.... Atavuruga hasa... Atawavuruga.... Na CCM itaingia 2019 ikiwa mapande makubwa matatu
. CCM mwenyekiti
. CCM Membe
. CCM wengine
Ujumbe huo wa Nape unabeba siri kubwa nyuma ya kinachoendelea sasa chamani... Muda utasema.. View attachment 952923
 
Kete kubwa atakayotumia ni kuwafuta uanachama kwa kigezo cha usaliti wote wanaowashwa washwa. Ndo madhara ya Kofia Mbili kwa hali ya sasa haifai kuwa na Kofia Mbili.Kila mmoja abaki na nafasi yake ili waweze kudhibitiana raisi abaki raisi na mwenyekiti abaki mwenyekiti kma ili ANC ya South Africa.
Mshana,Miaka tayari imeisha

Au miaka ina miguu au ugumu wa Maisha yaani tayari 2019

Manunuzi yamepita,Maigizo yamepita bado upinzani tena ndani ya chama

Wasiojulikana ?
 
Back
Top Bottom