Zanzibar 2020 Urais Zanzibar 2020: Barua kwa Balozi Ali Abeid Amani Karume (Barua ikilenga kumchafua)

Zanzibar 2020 Urais Zanzibar 2020: Barua kwa Balozi Ali Abeid Amani Karume (Barua ikilenga kumchafua)

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Urais Zanzibar 2020: Barua kwa Balozi Ali Abeid Amani Karume

Ndugu yangu Ali, As-salamu alaykum. Nakuandikia barua hii ya wazi kwa upendo wangu wa kikamaradi kwako. Nafsi yangu imenisukuma kufanya hivyi kwa muda mrefu lakini msukumo zaidi uliniingia jana tulipokutana Kisiwandui.

Nimekufahamu kwa miaka mingi na mara nyingi tumeshauriana mambo kadhaa japo siku za karibuni umekuwa ukinikwepa. Hata jana nilipotaka kuzungumza nawe ulipotoka kuchukua fomu kuomba ridhaa ya CCM kugombea Urais Zanzibar bado ulinikwepa na kwenda zako.

Nafahamu kwa nini unanikwepa na bahati mbaya kutokana na hilo tunashindwa kukutana na kuzungumza haya, nami sina budi kujaribu kukuandikia kwa njia hii ili yakufikie.

Unanikwepa kwa sababu mara zote nimekuwa mkweli, na ukweli una gharama zake, umenigharimu urafiki wetu japo naamini iko siku tutarudisha ukamaradi wetu. Unanikwepa kwa sababu mimi sijawa kama wengi wa wanaokuzunguka mitaani na sehemu za chupa za mvinyo na starehe wakikupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Ndugu yangu, mimi kama Mzanzibari na mtu ambaye nimekufahamu tangu ujana wako nimejitahidi sana kukusitiza kuwa huna faili zuri kutosha hata kujaribu nafasi yoyote ya uongozi wa umma Zanzibar. Katika barua hii nataka tena kukumbusha kwa nini nimekuwa nasema hivyo na kwa nini kitendo chako cha kuchukua fomu ni hatua ya kiwango cha juu kabisa kujidhalilisha mbele ya kadamnasi (majuma machache yajayo utaamini hili).

Ali, katika kujinadi kwako kwenye Urais Zanzibar unasema unao uzoefu wa kidiplomasia, lakini wafahamu ni uzoefu wa namna gani? Wakumbuka umeingiaje katika dunia ya diplomasia na yepi umefanya katika eneo hilo? Ngoja nikukumbushe. Mwaka 1982 ulipofika New York Marekani kusoma unakumbuka ilikuwaje? Uliondoka Zanzibar kwa kesi ya kubaka na kumuua uliyembaka.

Baada ya Marekani ukenda Ubelgiji kuwa Naibu Balozi. Kukuondoa Zanzibar na kukutupa ughaibuni ilikuwa mbinu kukunusuru na hasira na kisasi cha Wazanzibari.

Hivyo hukuingia katika eneo la diplomasia kwa vigezo vya weledi (merit) bali ni kwa mfumo kukuficha kwa heshima ya wazazi wako, huku ukiacha huzuni na majonzi kwa familia ya mhanga wa tukio lile baya zaidi la ukatili wa kijinsia kuwahi kutokea hapa Zanzibar.

Kwamba ulimbaka binti wa watu na kama hiyo haitoshi ukamuondolea uhai na kwenda kumtupa ufukweni. Naandika kukumbusha kwamba jamaa zake bado wako hai, na nyaraka za jinai ile bado zipo. Wasiotaka kukumbusha hili hasa wakati kama huu unapojaribu kwenda mbele ya umma kuomba uuongoze hawakutakii mema.

Hili peke yake lingetosha kukutuliza nyumbani jana Juni 16 lakini ukajisahaulisha na kwenda Kisiwandui. Nakuhakikishia hakuna Mjumbe wa CCM mwenye akili timamu (na naamini kwa dhati kabisa wote wana akili timamu) atakayekupitisha popote pale ndani na nje ya Zanzibar.

Kama ambavyo jana ulitoka na kufanya dua kwenye kaburi la babako, ni vyema pia ungekwenda kufanya dua kwenye kaburi la binti yule mbichi uliyekatisha uhai wake badala ya kupoteza muda kwenye siasa za uwakilishi wa wananchi eneo ambalo huna nafasi yoyote kufanikiwa. Nakusihi ukweli huu uutafakari kwa kina, uupokee kwa unyenyekevu na kuuishi.

Ndugu Ali, naamini hujatumia muda wa kutosha kutafakari aibu hii uliyojibebesha jana, ambayo ni anguko lako la mwisho kwenye siasa Zanzibar. Wakati huu unapozitazama fomu ulizochukua jana, pembeni ukiwa na kinywaji chako pendwa cha Konyagi, nataka kukukumbusha namna ambavyo uliingia katika utumishi SMZ ukiwa na umri wa miaka 19. Katika umri huo, wenzako wakiwa shuleni wewe kwa nguvu za babako ukapewa Ukurugenzi ZSTC. Pale ZSTC ukazidisha ulevi lakini hilo likawa si tatizo, ukapandishwa cheo ukiwa hufanyi kazi yoyote ya kuonekana ukapewa Unaibu Waziri.

Ninyi watatu, wewe, Amani na babako mkaiibia Zanzibar zaidi ya dola za Kimarekani milioni 20 wakati huo na mzee alipofariki zikabaki katika akaunti zenu binafsi ughaibuni. Mambo haya si siri Ali, wala hamjawahi kuyatolea maelezo, twafahamu na tunakusitirini tu, ila ukijitokeza kujifanya mwenye uchungu, haki na sifa ya kujaribu kutuongoza Wazanzibari tutakukataa waziwazi. Wengi watasema hutoshi na wanaishia hapo lakini mimi naona ni busara kukumbusha kwa nini hutoshi kama ili ukae ukikumbuka na kutojaribu tena kujiabisha kwa kudhani watosha.

Nataka kukumbusha kuwa sisi hapa Zanzibar hususani Unguja hatujasahau fujo zako za ujanani na umajinuni wako utu uzimani. Twafahamu pia kwamba kesi ile ya kubaka na kuua pale Gongoni haikuwa ya kwanza kwako na hata sasa zipo nyengine ambazo vyombo ya ulinzi na usalama vinazo kumbukumbu zake na zitatumika wakati unaofaa.

Ali, unapoomba nafasi ya juu ya uongozi lazima kuonesha kwamba umefika ulipo kwa uwezo wako. Nakushauri jioni hii unapokaa kunywa (nakusihi punguza pombe na tazama afya yako) chukua peni na karatasi andika chini nyadhifa zote ulizowahi kuwa nazo kisha tazama kama ipo yoyote uliyopewa kwa uwezo wako mwenyewe. Ipo? Jibu unalo, na jibu wanalo Wazanzibari na wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu CCM, na watalitumia jibu hilo vizuri siku si nyingi.

Ali, wakati umekaa na fomu hiyo ya Urais jaribu kuiscan nafsi yako na matendo yako ya kihuni toka ukiwa mwanafunzi pale Aga Khan, mpaka kulala kwenye pub jijini New York ukiwa chuoni Columbia. Kumbukumbu zinakujia sawa? Simama mbele ya kioo, jitazame, vuta kumbukumbu. Je unadhani kwa historia hiyo unafaa kuiongoza Zanzibar?

Unakumbuka Lumumba College ulikuwa na marafiki wawili wa kiume uliowaingilia pasi utaratibu? Unakumbuka hii ilivuma hadi babako Mzee Karume kukucharaza bakora hadharani Unguja? Unafahamu baadhi ya tabia hizo uliendelea nazo hata ulipokuwa kwenye balozi zetu mbalimbali na kumbukumbu zipo? Ukijipima kwa hili unajiona unatosha kuwatumikia Wazanzibari katika nafasi yoyote ile? Jibu unalo, nasi tunalo.

Ndugu yangu, staili hii ya maisha yasiyo na maadili wala staha imekuletea matatizo mengi. Si nia yangu kuyataja lakini nitataja yale tu ambayo naamini yoyote anayetaka nafasi ya uongozi hapaswi kuwa nayo. Moja ni tatizo la kudumu ulilo nalo la ulevi licha ya kwenda rehab mara nyingi kupata tiba. Wafahamu swahiba zako kwenye kinywaji Zanzibar wanakuita Mwenyekiti wa Walevi? Kijiweni pale Bar ya Maisara nyuma ya Jengo la CCM na mara nyingi umekunywa hadi kupoteza fahamu. Je, ukijipima unahisi unatosha kuongoza? Mie nakukumbusha tu. Naamini majibu unayo na utajibiwa zaidi siku za karibuni.

Ndugu yangu Ali, wewe unafahamu fika kwamba taarifa za kiafya toka kwa madaktari zinasema sasa una ugonjwa wa nerves disorder uitwao Alzheimer. Maradhi hayo huathari ubongo na kusababisha kushindwa kufanya kazi sawa sawa na kupoteza uwezo wa kukumbukumbu. Naamini taarifa iko kwa Kamati Kuu ya CCM na ile ya Usalama na Maadili (suala la afya ya akili ya Mgombea ni la kiusalama). Ukiongeza hili na mengine hayo bado unadhani unatosha?

Mie na Wazanzibari wengi tunaamini hukufanya tafakuri nzuri ama wako wanaokupotosha ili wapate vijisenti japo wanafahamu hufiki popote lakini si haba.Nasikitika kwamba sikupata nafasi ya kukutana nawe kukushauri usijitwishe aibu hii lakini natumaini kwa mara nyingine tena utajifunza marafiki wa kweli ni kina nani.

Huu ni wakati wako kuondoka si tu katika siasa ambazo daima zimekukataa lakini pia katika utumishi wa umma ambako nako umeishi kwa hisani. Huu ni wakati wa wewe kupumzika na kutazama afya yako, si wakati wa kujidhalilisha na kukubali kuongopewa na wachache huku sote tukifahamu kwamba huna nafasi yoyote kuweza kuteuliwa na CCM si tu kugombea katika nafasi ya Urais bali katika nafasi yoyote nyeti.

Alamsiki.
Ndimi
Abdallah Juma Mserembwe
Zanzibar
 
Back
Top Bottom