Urasimu Bandari ya Dar, wafanyabiashara wa Parachichi wakimbilia Mombasa

Hapo bandarini Dar wanashindwaje ku-handle mzigo wa ku-export Parachichi? Yaan Parachichi litoke Njombe likasafirishwe Mombasa port?
Parachichi zinazo pita Mombasa, ni za wafanya biashara wa Kenya. Huzi nunua Tanzania na kuziweka label ya produce from Kenya.
 
Hizo kazi zinafanywa na Mawaziri wenye akili,sasa awa Wakina January, Mwigulu,Bashe na Ashantu akili kubwa kama hizi wazitoe wapi!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
 

Hapo ndio umeshawatonya kama kuna dili Holland, sasa baadala ya wao kuwaza kuwasaidia wafanyabiashara watanzania na watanzania baadala yake watatafuta namna ya kuhodhi hiyo biashara kwa kuwatumia ndugu zao na facilitity za umma kama shirika la ndege.
 
Bandari fanyen kazi. Acheni kukwamisha raia wenzenu. Wasio na uwezo wa kutoa peSa za wazee
 
Hapa hii taarifa ina ukakasi kidogo..

Bandari wawe na cold room kwa ajili ya Parachichi kutoka Njombe! How? Kwani zimetoka vipi Njombe hadi Dar Port?

Kuna container special zinazotunza baridi kwa ajili ya bidhaa za kuharibika. Hizo container wako nazo shipping line. Ukishapata container unaenda weka mzigo wako na shughuli za usafirishaji zinaendelea.

Na kawaida iwe import au export lazima mambo ya documentation yaanze kabla ya process nzima kuanza. Lazima uhakikishe documents zipo Sawa na permit zote zipo.

Bandari sio store ya mizigo, waweke cold rooms za nini wakati kuna special containers kwa kazi hiyo?

Cold rooms zipo airport huko maana hawana special units za kuwekea hiyo mizigo ambayo ni rahisi kuharibika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…