chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Huu mwaka utakumbukwa has a kwa tukio la makosa ya kisiasa aliyofanya Tundu Lissu.
Kosa hilo ni kuibomoa kabisa taasisi kisha anatarajia akalale humo. Hatapata pa kulala kwa kuwa jengo amelibomoa. Lissu amekata mti, baada ya kuukata, sasa anasema anataka aukwee mti huo.
Hii ni moja kati ya blunder kubwa kabisa ya kisiasa kwa takribani miaka 20 iliyopita, ambayo pia inamtafuna Lissu kuanzia miguuni, na sasa iko ngazi ya kiuno.
Mfumo wa siasa za Lissu ni sawa na mfumo wa kujenga nyumba kwa tofali za barafu. Akinasa kwenye joto anayeyuka na kukimbilia baharini, ambako atapotea kabisa kwa kuwa itakuwa ngumu kutofautisha maji ya bahari na barafu iliyoyeyuka.
Kilichobaki ni kumpigia akiwa baharini, maana huko hata sauti haitatoka, Samaki wenye meno makali watakuwa wananyofoa vipande vya nyama wakifaidi utamu wa maamuzi ya hovyo ya kisiasa.
Hata kama akirudi, atakuwa si Lissu yule, kwa kuwa sasa kila upande atakuwa kazungukwa na watu wanaosubiri kumsukuma ateleze. Baadhi atabaki nao akiamini ni wake, lakini wako pale kusubiri kumpiga dafrau, blackmail, uzandiki, na kila aina ya michezo michafu ya kisiasa.
Amepasua mtumbwi katikati ya bahari halafu anajiaminisha kwamba mtumbwi uko salama. Maji yameingia (Msigwa na Dk Slaa) pamoja na watu wa mfumo ambao alikuwa akiwatusi mchana na usiku.
Ni zamu yao kumuhenyesha mpaka macho yamtoke pima. Wata -infilitrate mambo yake yote kwa kuwa robo tatu ya taasisi ya chadema haimuamini, wako pale kumtega miba.
Ni mwanzo wa mwisho? Ndio, kila zama na kitabu chake, tumefunga kitabu cha James Mapalala, Kasanga Tumbo, Mti kila, Lamwai, Mbatia, Lipumba.
Naona kijana anamalizia kusoma kurasa za mwisho, kwa mafikara makubwa anataka kulifunga kava gumu la kitabu cha Ziwa Kindai.