Uratibu mbaya wa makadirio ya kodi ndiyo sababu kubwa ya ukwepaji kodi

Kodi lazima ikadiriwe halafu wewe utaitetea kwa accounts zako kwa Sababu provisionally unakuwa ulijikadiria wewe mwenyewe

Tunza kumbukumbu zako vizuri


Kodi za mauzo hazitakiwi kukadiriwa kabisa. Kinachotakiwa na kutumia risiti na zitaonyesha kwa uwazi kabisa kodi ni kiasi gani. Utabiri ndiyo umetuletea matatizo yote
 



Mimi sikubaliaani kabisa na makadirio. Makadirio yalikuwa ni mihimu zamani kwasababu tulikuwa hatuna teknologia kwa sasa ni lazima utoe risiti na kutumia machine za kutoa risiti sasa kwa misingi hii makadirio ni ya nini? Hapo ndiyo kwenye tatizo. Kwanini nchi nyingine hawana makadirio?? Yaani huwezi kuweka machine za risiti halafu wewe uliyoweka usiziamini tena! na kuna risiti za makaratasi.

Kikubwa ni kufuata sheria na teknologia haya mambo ya makadirio rushwa haitaweza kuisha na serikali haitaweza kupata pesa halisi.
 
Kodi za mauzo hazitakiwi kukadiriwa kabisa. Kinachotakiwa na kutumia risiti na zitaonyesha kwa uwazi kabisa kodi ni kiasi gani. Utabiri ndiyo umetuletea matatizo yote
Mkuu,Kukadiria Maana yke ni nini?Kukadiria maana ni kufanya Makisia ambayo yanakaribia Uhalisia.Kwa nin serikali inataka Kukadiria ni kwa sababu hata yenyewe inapopanga Mapato na matumizi huwa ni Makadirio.So Makadirio kama Makadirio Sio tatizo,Tatizo ni namna na usimamizi wa makadirio na utaratibu wote unaohusisha Ukadiriaji wa Mapato kwa Malengo ya Kikodi.
 
Mkuu Makadirio hayana SHida na ni Utaratibu wa Kawaida kabisa ambazo sioni shida yake Kabisa?Swali langu ni Je wewe ni Mlipa KODI?Umewahi kufanya au kufanyiwa Makadirio?Tatizo lilikuwa ni nini hasa ili TRA Tanzania wakuelewe vizuri.
 
1. Siyo wafanyabiashara wote wana mashine za risiti. Sheria inamtaka mtu ambaye mauzo ya ni 11m kwa mwaka kutoa risiti. Kama mauzo yako hayafiki 11m hulazimiki kutoa risiti. Kodi yako itakadiriwa kulingana na aina ya biashara unayofanya.

Hapa ndo tatizo linaanza. TRA wameweka viwango kwa aina ya biashara kwa Mfano Duka la mangi, Glocery ya vinywaji, Stationery etc. Katika kundi hili wote mnalipa.sawa bila kujali volume ya mauzo.

Ili kuondokana na tatizo la makadirio basi unaondoka kwenye hilo kundi la presumptive taxpayer unaanza kutunza hesabu.

2. Kunawafanyabiashara wanatoa risiti lakini hawatumzi hesabu. Hawa pia wataangia kwenye kundi la kukadiriwa kodi. TRA watatumia data za mauzo yako kutoka kwenye mashine kukukadiria kodi. Kama unataka kuepukana na tatizo hili tunza hesabu na ulipe kile tu unachotakiwa kulipa.

Pia mfumo ulivyo ni kwamba utakadiriwa kulipa say laki 3 kwa robo mwaka. Lakini mwaka unapoishia unapeleka hesabu. Kama umelipa zaidi wanakurudiahia. Kama umelipa kidogo unamaliza kiasi kilichobaki.

Sasa matatizo makubwa yako kwa wafanyabiashara.
1. Hawatoi risiti hata kama wana mashine
2. Hawatunzi hesabu.

Hivyo.afisa wa TRA atakachofanya ni kukuhoji maswali, kuomba daftari kukadiria mzunguko.wa biashara na kukudiria kodi.
 
Hii mkuu unaizungumzia wewe kama mtaalam ila ukija kwenye Biashara kama Kkoo kunakuwa na uhalisia mwingine.

MFanya biashara mkubwa anauzia wafanyabiashara wadogo bila risiti, mfanya biashara mdogo anapata faida ndogo ila mauzo makubwa hii ina inflate kodi anayotakiwa kulipa sababu hana risiti ya manunuzi, at same time kuna machinga na mawinga wanachukua mzigo kule kule anapochukulia mfanyabiashara mdogo mwenye Efd, wanauza kwa margin ndogo hivyo inabidi mwenye duka arespond, hapa ndo unakuta bidhaa ya 98,000 inauzwa 100,000 faida 2,000 tu, kule Tra inasoma ulipe kodi 18% ya 100,000 lakini mfanya biashara kapata 2000 tu inabidi mfanya biashara atafute alternative.

Ushauri wangu ni kila mtu alipe kodi haijalishi ni Machinga, winga, Page ya insta Etc watengeneze database watoe mambo ya 18% kwa wafanyabiashara wadogo bali kuwe na kodi fixed kwa kila bidhaa, mfano Box la wall tiles linajulikana linanunuliwa 13,000 inauzwa 15,000 basi inakadiriwa kodi maybe 300 kila box, ukiuza box 10 kuwe na 3,000 ya Tra na iandikwe kwenye risiti ama mahala husika wote mfanya biashara na mteja wajue.

Then kuwe na wallet unamalizana na Tra instant, umeuza box 10 una generate control no hapo hapo unalipia ama mwisho wa siku unalipa like that, mfanya biashara kulipa 5000 ama 10,000 Tra kila siku na kuja kutoa 500,000-1M kwa awamu ni tofauti.
 


Ninarudi palepale suluhisho ni kila mmoja kutoa risiti. Ukiwa na mfumo ambao kuna watoa risiti na wasiotoa risiti apo una tatizo. Cha kwanza kabisa kila waazaji watakiwe kutoa risiti bila hivyo mfumo mzima wa kodi matatizo hayataisha. Machinga akiuza kitu kwenye bei inatakiwa kuwepo kodi na hiyo kodi sio pesa ya machinga bali ni pesa ya serikali.
 
Mbona wanasema control number unaweza kutengeneza wewe mwenyewe tu ofisini kwako? Ile kwenda ofisi za TRA ni kupenda tu.
 
Haiwezekani kila mmoja atoe risiti wakati kuna loophole ya Machinga na winga, njoo field utaona hio issue haitekelezeki.
 
CC: TRA Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…