Habari Mabibi na Mabwana!!! Natumai muwazima wa afya njema,.kwa ndugu zangu waislam mwenyezi Mungu azidi kuwapa wepesi mmalize salama funga yenu inshaallah..
Jamani warembo wenzangu na watanashati mm kwa sasa nimekuwa mpenzi wa nywele fupi,huwa natumia wave au dawa laini kulainisha nywele zangu na kuzipaka curl activator sio siri napendeza na kuvutia mnoo[emoji4] [emoji4]
Sasa tatizo linakuja nikiwa naweka dawa nywele zangu yaani dawa haikai hata dakika 10 kichwani yaani inauma sana na nikisema nivumilie vumilie naweza ungua so unakuta muda mwingine haishiki vile ninavyotaka,tofauti na wengine anaweza kukaa na dawa kichwani hadi lisaa....hivyo naombeni ushauri nitumie wave/dawa gani ili nisisikie Maumivu upesi au nifanye nn kabla kuepuka Maumivu na kuu gua??? Shukrani.
Mumu.