WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
- Thread starter
- #21
Katika mavazi au mapambo yeyote kuna wale wanaovaa kwa kujifurahisha wao au wenzao na wale wanaovaa ili kutuma ujumbe kwa wale wanaoelewana lugha. Ubaya ni kuwahukumu wote kwa matendo ya wachache. Mwanamke ana uhuru wa kuvaa anavyotaka na kujipamba atakavyo ili mradi conscience yake haimshtaki. Sisi wengine inabidi tuangalie na kushukuru Mungu kuwa ameumba watu wa jinsia tofauti. Kama tunaona wafanyavyo hakutufurahishi, basi tugeuze macho na kupitia kwengine. Mimi sijali hizo maana zinazosemekana bali nafurahi kuona mguu ulioumbika umerembwa ipasavyo. Hayo mengine nawaachia nyie.
Amandla.....
I salute you!
Kama tutaendekeza kujali nani atasema nini basi maisha yatakuwa ya tabu sana maana kila mtu afanyacho kinaweza kutafsirika vibaya.
Afterall who has the right to judge others?
Kama ni suala la secret societies na secret symbols basi "WAHUSIKA" waachiwe wajitafsiri na kuelewana wenyewe kwa wenyewe kuliko kudhani kila mtu ana maana hiyo hiyo mbaya.