Swala si kuelewa tu, swala ni kutumia maneno sahihi pia.
Kutumia maneno sahihi ili iweje zaidi ya kuelewana?
Ndege wa angani na wanyama wengine hawana "maneno sahihi," kama wana maneno, na bado wanakaribia kuelewana. Fahari la ngo'mbe linafahamishwa na jike kwamba sasa ni wakati wa kuumba ndama. Na katika zizi zima, fahari huwa halifati-fati jike lolote ambalo halina mpango wa kupata ndama kwa wakati huo. Mhusika linamjua bila "maneno sahihi." Linajuaje?
Kama mimi nilielewa inawezekana wengine wasingeelewa...
"Kama mimi nilielewa inawezekana wengine wasingeleewa..."
Hebu rudia tena? Umeseje hapo? Angalau aliyesema "kikukuu" alieleweka!
maana ya kuwa na lugha ni nini kama si kutumia maneno yaliyokubalika?
Maneno yaliyokubalika na nani? Maneno mapya yanaingiaje kwenye msamiati?
Kwa msingi wako ukisalimiwa jambe au jamba instead of hujambo itakuwa poa tu?
Lugha haina ukamilifu. Atakaesema "hujambo" na atakaesema "jamba" wote wawili hakuna mwenye uhakika wa kueleweka. "Jamba" lina maana nyingi, ya kwanza si neno la kupendeza, na la pili ni neno la kitaalam, yani nafasi yenye hewa iliyoko tumboni. Hujambo ni salaam, na pia ni jina la mtu. Nikikupa mkono nikasema "Hujambo," naweza kuwa najitambulisha, wewe ukaanza kunipa historia ya afya yako kumbe hata sijauliza, maana ninakotoka mimi "Hujambo" ni jina la mtu!
Sasa anayechemsha atajuaje kama wewe utaelewa au hutaelewa?
Vyovyote iwavyo kamwe hawezi jua. Lugha si timilifu. Nikipayuka "BLURAY..." utageuka kukurupuka kuitikia au utaangalia kwanza kama nashangilia kuokota sahani ya kisasa ya kurekodia muziki? Utajuaje kilicho mawazoni mwangu? Lugha inaweza kuwakilisha fikra?
Kama huwezi kusema na/au kuandika Kiswahili kubali kujifunza au tumia lugha nyingine, lakini kamwe usitetee mmomonyoko wa lugha.
Kila mmomonyoko hupelekea mkusanyiko. "Kikuku" likimomonyoshwa linaweza kuzaa "kikukuu" na "kikuu" katika msamiati mpya. Ukiliangalia kwa mapana, unaweza kuanza kuelewa kidogo ninachoongelea.
Tusiwe vichwa ngumu tunapokosolewa, tutakuwa hatujifunzi.
Kweli, tusiwe vichwa ngumu. Na tusiwe vichwa panzi kukubali kubali vitu bila kuvichuja. Nikisema nimeelewa bila kukubaliana nacho ina maana nimeamini. Sitaki kuamini, nataka kujua: kama haeleweki umejuaje ni kikuku na sio kikukuu au kikuukuu?