Meanings are socially constructed...
Napenda sana kuvaa cheni mguuni lakini kila nikiomba opinion ya mume wangu anakataa kata kata...
Sasa nina rafiki wa kiganda aliniona siku moja nimetupia pete nyingi vidoleni mikono yote miwili...
Huwa tuko free with each other akanambia NK hizo pete zinakufanya uonekane cheap...hivyo ndio waganda wanavyo judge wanawake...nilicheka saaana....
Nikamwambia pete Tz siyo issue ; issue uvae kikuku mguuni...wacha ashangae...akaniuliza kwani kuvaa cheni mguuni si urembo tu,,,
Nkamwambia ndio maanake...yani jamii inakulimit uhuru wa kufanya kitu roho inataka....
iwe cheni au pete ni vitu ambavyo wala havibadili ngozi wala nini lakini watu wame define wanavyotaka wao...and the definiton is widely acceptable...
Ila nimegundua ni Tz tu ndio tuna define hizi cheni this way...kwa wengine ni urembo tu...
Namlaani huyo aliyeanzisha hii definition...kwa sababu nina hamu kweli ya kuvaa kikuku...ila ndio hivyo tena....na ujanja wangu wote nimekuwa limited na hii definition...